Siasa Inapoingilia Mambo ya Teknologia......!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa Inapoingilia Mambo ya Teknologia......!!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by STK ONE, Aug 26, 2012.

 1. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sina takwimu za kutosha, lakini naamini kuwa hadi sasa bado sehemu kubwa ya nchi yetu bado haijaunganishwa kwenye teknologia ya kutumia VING'AMUZI ambavyo ni muuimu kwa ajili ya kuhama kutoka analogue kwenda DIGITAL.

  Nina mifano michache, Huku kwetu Mpanda hata dalili hatuzioni, Kigoma hali kadhalika, Sumbawanga hali ndiyo hiyo....na sehemu nyingine, sasa Wanasiasa wanapotuambia kuwa tujiandae kuhama kutoka analogue kwenda digital, wanamaanisha wengine tutabaki bila ya Mawasiliano ya TV?

  Sielewi, maana nasikia madish yatakosa kazi na madukani yameshuka hadi bei, Sasa sisi tunaotegemea madish kuona japo taarifa ya habari itakuaje kama hizo STAR TIMES NA TING bado hatuzioni?

  Mwenye majibu ya maswali yangu tafadhali anisaidie.
   
 2. Pinokyo Jujuman

  Pinokyo Jujuman JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapa pana utata wa uelewa ambao hata mie wanisumbua sana, kwani kitu cha msingi ambacho wananchi inatupasa kujiandaa na hii transition ya kiteknolojia ni kwa namna gan?
   
 3. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #3
  Aug 26, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Na vilivyopo ni vya kulipia na havifikii viwango,wana channel za hovyo, na chache kwa bei kama ya kipindi cha tritel na mobitel,Adesem .Nashangaa wanacharge hadi TV za bure za Nchini.Yaani kam ahujalipia wanakata hata TV za kibongo.
   
 4. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #4
  Aug 26, 2012
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145

  Kama unatumia Analog TV set, basi unatakiwau uconnect kwenda digital-kwa kutumia Conveter na mara ukiuunganisha waweza ona kama vile una digital TV, Bei yake kwa Tz sina uhakika lakini yaweza kuwa kati ya 70,000 mpaka 100,000/=…angalia picha hapa chini

  [​IMG]
   
 5. L

  Liky Senior Member

  #5
  Aug 26, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 198
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Hiyo wanauza wapi?
   
 6. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,578
  Likes Received: 1,674
  Trophy Points: 280
  mbona unavmia lugha ngumu. Au somo hujalielewa. Ìcho unakisema ni decorder so inaweza kuwa satellite dish au hizo za startimes na ting.
   
 7. lm317

  lm317 JF-Expert Member

  #7
  Aug 26, 2012
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 452
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ving'amuzi = Decoders
  Nyie wa madish mbona mliisha hama zamani?!!! mnataka muhame mara ngapi?
  Madishi yote yanatumia Ving'amuzi (Decoders) sema labda sio vya Star times au Ting

   
 8. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #8
  Aug 26, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unazidi kunichanganya....mbona wanasema eti ni lazima uwe na ving'amuzi...haya madishi si hayalipiwi baada ya kuyanunua? Hawa nao bwana, sasa wanaotakiwa kuhama ni akina nani?
   
 9. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #9
  Aug 26, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  Kuna sheikh mmoja huku Nangurukuru alivyoambiwa ahamie kwenye Ving'amuzi yeye akaanza kupaki vitu vyake vya ndani. Sijui alifikiri ving'amuzi ni nchi.
   
 10. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #10
  Aug 26, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  hahahahhahaaa!! Aseeee
   
 11. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #11
  Aug 26, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,336
  Likes Received: 22,188
  Trophy Points: 280
  Sheikh Ponda naomba mwongozo wako kwenye hili swala la ving'amuzi
   
 12. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #12
  Aug 26, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Wacha kupotosha mtu kauliza kwa nia njema, dish ndio analog yenyewe kingamuzi na decoder ndio digital system. Kinachofanyika ni kuingiza tv Chanel zote kwenye digital zile zote za bure itakuwa zinalipiwa Kama super spot nk. Atakae kuwa analipia ni kampuni ya icho kingamuzi chako kupitia wewe kila mwezi au Mwaka Kama ilivyo cable kupata super spot, hbo nk. Madishi yatatumika mpaka Siku ya mwisho watakapo launch mtambo wao na hapo ndio itakuwa mwisho wa dish ila cable na vingamuzi utalipa kila mwezi bado unamuda wa kumalizia hasira dish lako Mkuu mpaka dec- baada ya hapo jiandae kulipia Kama bill zingine Maji etc
   
 13. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #13
  Aug 27, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Haya ni makosa makubwa sana, sioni kwa nini Serikali yetu haijalikemea hilo - kwa nini StarTimes inakata channel za humu nchini kama hujalipia inabakiza TBC peke yake?

  Mbona kuingia mkataba kati ya STARTIMES na TBC ilikuwa na madhumuni ya kusambaza mawimbi ya TV stations zote hapa Tanzania kwa mfumo wa Digital kwa wananchi. Nilishangaa baadae nilipo sikia kwamba ITV na StarTV wamehamua kuhungana na kujitegemea, in other words hawataki kujiunga na StarTimes na kusema kweli makampuni hayo yalikuwa yanapinga sana kulazimishwa kujihunga katika mfumo huo sijuhi kwa nini; nikawa najiuhuliza hivi Tanzania ina Serikali ngapi ? Kwani sababu ya Serikali yetu tukufu kusema itasambaza matangazo yote ya TV nchini kwa niamba ya makampuni yote ilihishia wapi? Je wanawaogopa wafanya biashara wa station za TV nchini au vije!

  Kuna mambo mengine huwa yananishangaza kuhusu nchi yetu wakati mwingine, mimi naona madhumuni ya Serikali yetu kuhusu kusambaza mawimbi ya matangazo TV stations zote nchini kwa mfumo wa Digital kwa kupitia TBC kulikuwa sahihi kabisa - sasa kama TBC imekwisha nunuwa mitambo na kuweka infrastructures za kufanikisha hilo inakuwaje tena Wachina wanakuwa na upperhand ya kuhamua ni station/channel zipi za humu nchini wananchi wanaweza kuziona bila malipo?

  Ubia wa bihashara kati TBC na Startimes ubaki kwenye channel za nchi za nje na siyo za humu nchini na hili ndilo wanataka kwenda kufanya nchini Kenya.

  Mimi ushauri wangu kwa Serikali yetu tukufu ni kwamba ni makosa sana StarTimes kulazimisha watu kuangalia channels za humu nchini kwa kulipia, hii hawezi kuwa ndio yalikuwa madhumuni ya TBC kuingia ubia na StarTimes, actually ningependekeza kwamba channel zote za East Africa ziwe clear wasizi-scramble. Jana nilimsikia Waziri mdogo wa IT na mawasiliano wa Kenya alipokuwa Uchina akisema StarTimes itafungua kituo kingine nchini Kenya mwezi hujao.
   
 14. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #14
  Aug 27, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Mkuu kazi ya dish ni kukusanya/kutuma mawimbi kwenye satellite, dish alijuhi kama mawimbi yanayo pokelewa/kutumwa yako kwenye digital au analog form, inayo tambuwa hilo ni decoder na transponder za satellite.

  Vile vile siyo kwamba satellite zote zinatuma na kupokea mawimbi in digital form, zipo zinazo tuma na kupokea mawimbi in analog form na decoder zake ziko hivyo. Hapa nilikuwa natoa angalizo mkuu.
   
 15. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #15
  Aug 27, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Mkuu, kwa nini inauzwa bei kubwa namna hiyo, hapa wanachezea lugha kwani hiyo si digital tuner tu ina nini cha ziada!!
   
 16. Wayne

  Wayne JF-Expert Member

  #16
  Aug 27, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 663
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkulu
  Samahani nikiandika kwamba hujui ulichoandika....naomba uwe mvumilivu ili upate elimu....
  Mfumo wa dish ni DIGITAL...
  kwa maana kwamba halifanyi kazi bila receiver or decoder
   
 17. Pinokyo Jujuman

  Pinokyo Jujuman JF-Expert Member

  #17
  Aug 29, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dah mie hapa naona bado mwanitingisha kwakweli, hata sikumbuki nliko sasa, but my loggic behind is,
  1. System ya DISH ni annalog au Digital?
  2. Kama ni Digital, Je tunahaja ya kufanya la ziada ili twende sawa na huo mpango wao mpya?
   
Loading...