Siasa basi Mchungaji Rwakatare

Siasa basi Mchungaji Rwakatare

Hana jipya huyo, anajua kina mama wa morogoro hawatamchagua tena. Aliwaahidi kila mjumbe atampa gari na kumjengea nyumba akipata ubunge. Baada ya kupata ubunge hajarudi jimboni mpk saiv tunavyoongea. Halaf eti ni mtumishi wa mungu. Mtumishi wa mungu my foot!!

Wazushi na wasengenyaji kwao ni.ziwa la moto.

Kwa taarfa yako,Lwakatare ni mbunge viti maalum,hana jimbo,tubu dhambi kwa Yesu na usirudie tena chuki binafsi!
 
Mama Rwakatare (Mchungaji Rwakatare) alisema amebaini kwenye siasa kuna watu wanataka kutumia nafasi hiyo kumchafua jambo ambalo linampa wakati mgumu ikizingatiwa kuwa ana watu wanaomwamini kiroho.
“Sifikirii kwa sasa kugombea ubunge mwakani, siasa ina mambo mengi sana, bora niendelee kumtumikia Mungu, kama wazo litanijia tena ni hapo baadaye,” amesema Mama Rwakatare

Una lipi la kumwambia Mchungaji huyu?



source
East Africa Television (EATV)
Pepo la CCM , Pepo la mama Rwakatare , huyu mama aliingia kwa rushwa , Muulize Dada Matha.
Mama wa madawa ya Kulevya muasisis wa zinaa
 
Angekutuambia ni MUNGU YUPI anamtumkia kwani matendo yake hayaendani na anayosema hata kidogo, mfano ni MPORAJI mzuri wa viwanja vya maskini! Ni Mlaghai!
 
wakuu hivi huyu mama kwanin hapingi maovu wakati ni kiongozi wa dini pia? na kwa kipindi chote cha ubunge wake kama mwakilishi wa wananchi atakumbukwa kwa yapi hasa(in positive impacts)?
 
Kwa mungu hayupo wala kwenye siasa hayupo huyu mama nitapeli kama matapeli wengine
 
Mhe.Mama Rwakatare anapima upepo wa kisiasa Moro kulingana na alivyowekeza mali/pesa kugombea ubunge;pia ajue adui zake!
 
Huyu mbona kajichafua mwenyewe miaka mingi tu!!! Asimtafute mchawi wake, mchawi ni yeye mwenyewe kwa kuendekeza ufisadi huku akijifanya ni mcha Mungu.
 
Ushauri kwa mama Rwakatare, atimize ndoto yake ya kugombea urais Tanzania;kwa kuunda sasa kamati yake ya ufundi kitaifa!
 
Hawa wachungaji wa mshahara ni shidaaa kwani kuchunga kondoo si kazi yao wao ni ufahari kwa kwenda mbele . Nilitegemea angesema pengine uhusiano wake na Muumba wake hauko sawa lkn mmmmhhhhhhh
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Yamekaa vema haya maswali, na ayajibu sasa! Vinginevyo hata akiwa madhabauni sisi hatutamsikiliza zaidi ya kuwaza maswali haya.
 
wakuu hivi huyu mama kwanin hapingi maovu wakati ni kiongozi wa dini pia? na kwa kipindi chote cha ubunge wake kama mwakilishi wa wananchi atakumbukwa kwa yapi hasa(in positive impacts)?

KTK Ukirsto Hakuna m
Mchungaji mwanamke. na hata angekuwa Mwanamme tayari alisha poteza sofa za kumutumikia BWANA kwani Biblia inasema usitumikie MABWANA wawili na vyakaisari mpe kaisari na VYAMUMGU mpe MUNGU
 
NAAMINI IPO SIKU WATOTO WANGU
WATANIULIZA, BABA KILE CHAMA CHA KIJANI
CHA NCHI YA AHADI KWANINI KILISHINDWA
KIPINDI KILE 2015?? " NITAWAJIBU
HIVI...WANANGU ::
1. KWANZA CHAMA CHA KIJANI KILIKUWA NA
WABUNGE WALIO TETEA WIZI MFANO NI
ASSUMPTA MSHAMA NA LUSINDE KWENYE
SAKATA LA ESCROW, WABUNGE WA CCM
WACHACHE KAMA MAGUFULI NA MWAKYEMBE
WALIKUWA NI UPINZANI KIMTINDO NA
WALIPINGWA SANA NA WANA KIJANI WENGI.
2. LAKINI PIA PESA YA RADA KIPINDI HICHO
WALIKULA WACHACHE MMOJA WAO KATIKA
KILA DILI LA WIZI WA MALI YA UMMA LAZIMA
AWEMO, YEYE ALIKUWA KAPTENI WA TIMU YA
MADILI, MBAYA ZAIDI MTUHUMIWA HUYO WA
WIZI AKAPEWA KUWA MWANDISHI WA KATIBA
YA CHAMA CHA KIJANI!!
3. KINGINE WANANGU NI KASHFA YA
RICHMOND, MAAZIMIO YA BUNGE JUU YA
KASHFA HIYO YALIPIGWA CHINI, WEZI
WAKAJIUZULU NA WAKAAMUA KUHONGA PESA
ZA WIZI MAKANISANI NA KWENYE SHUGHULI ZA
KIJAMII ILI WAPATE URAIS. eti baba wezi
walikuwa wanaiba alafu wanahamishwa vituo vya
kazi au kujiuzulu ili wale pesa vizuri?? NI KWELI
WANANGU, HIYO ILIKUWA NI DESTURI YA
VIONGOZI HAO.
4. KASHFA YA BOT TWIN TOWER ILITOKEA CHINI
YA SERIKALI ILIYO JIITA "SIKIVU" YA CHAMA
CHA KIJANI.
5. KASHFA YA EPA ILITOKEA PIA CHINI YA
UTAWALA WA JAMAA HAO HAO.
6. MWANANGU TWIGA ALIWEKWA KWENYE
NDEGE KAMA VILE BEGI LA NGUO NA
KUTOROSHWA CHINI YA SERIKALI ILIYO JIITA
SIKIVU YA CHAMA CHA KIJANI.
7. SASA KASHESHE IKAWA NI MGOMO WA
MADAKTARI,, YULE ALIYE ONGOZA MGOMO
ALIITWA DK ULIMBOKA ALITEKWA NA
"KUSULUBIWA VIZURI KABISA" ETI NA WATU
WASIO JULIKANA KATIKA UTAWALA HUO HUO.
WANANGU MNADHANI NANI ALIMTEKA, MIMI
NAHISI NI MAJAMBAZI TU, NYIE JE?? "mmmmhh
Baba we nae si unajua tena"!! HAYA TUENDELEE
WANANGU......
8. IKATOKEA KASHFA YA WIZI MKUBWA SANA
KWENYE BANDARI YETU HII YA HAPA DAR CHINI
YA HAO HAO.
9.KASHFA YA MIKATABA ISIYO NA MASLAHI
KWA TAIFA YA GESI NA MADINI ILITOKEA CHINI
YA CHAMA HICHO HICHO KILICHO JIPACHIKA
JINA LA CHAMA SIKIVU.
10. WANANGU MNAONA HII BENKI YA NBC, NA
HIZI NYUMBA ZA SERIKALI, WALIUZA WAO KWA
BEI YA MTUMBA KABISA.
HUYU JIRANI YETU ANA KILEMA ALIPIGWA
RISASI WAKATI ANAJITETEA ASIHAMISHWE
MJINI, ALIKUWA MACHINGA MWANZA PALE
SAHARA NA YULE MWENYE MAKOVU PALE
ALIPIGWA SANA ALIKATAA KUHAMA PALE
MAKOROBOI MWANZA NAYE ALIKUWA
MACHINGA, HATA MAMA NTILIE WALIPIGIKA
VIZURI TU CHINI YA HAO JAMAA.
11. KWA HIYO KWA UZEMBE WA MISAMAHA YA
KODI NA UKWEPAJI KODI, NCHI YETU
WAKAIFANYA OMBA OMBA, WAKATI TUNA KILA
KITU.
.12. AJIRA WATU WAKAPEANA KINDUGU NDUGU
KULE UHAMIAJI, UNAONA HAYA MAGOFU YA
VIWANDA,,, ndiyo baba... WALIVIMALIZA WAO NA
WAKASEMA WATATULETEA AJIRA NA MAISHA
BORA, NA WAKAANZA KUNUNUA VITU NJE YA
NCHI KAMA SUKARI NA MCHELE NA WAKAFANYA
UFISADI HUKO MPAKA WABUNGE
WAKASHANGAA.
13. MBAYA KULIKO YOTE, KATIKA UTAWALA WA
SERIKALI YAO SIKIVU KABISA, TUKASHUHUDIA
MACHAFUKO YA KIDINI AMBAPO WALISHINDWA
KUDHIBITI MAPEMA MPAKA WATU
WAKACHOMEWA NYUMBA ZAO ZA IBADA NA
KUKASHFIWA KILA KONA.
14. CHA AJABU ZAIDI NI ILE KASHFA "ESCROW"
WALITAFUNA BILIONI 306 VIZURI KABISA.. NA
WAKATOA HOTUBA NZURI SANA YA PESA ZETU
ZA "MADAFU".
"Baba uhuru tulipata mwaka 1961," sasa swali
langu ni kwamba..KAMA WANGEKUWA NA
MALENGO MEMA NA WATANZANIA KWANINI
WASINGE SOMESHA WATAALAMU WA MADINI
TOKA MIAKA YA 1970 MPAKA LEO TUNGEKUWA
TUNACHIMBA WENYEWE KAMA KULE ULAYA??
MWANANGU WALISEMA SERIKALI HAINA PESA
TUBAKI KUWA OMBA OMBA.
baba gazeti la ----------- lilifungiwa kwa
kufuatilia sakata gani?? MMMMHH!! ETI
UCHOCHEZI WA.....................................!!
hahhahaha baba malizia basi....
Eti baba kifo cha yule gavana Balali ilikuwaje?? na
kifo cha yule mtangazaji alikuwa anaitwa
eehhhhhh...... WE UNATAKA KUSEMA
MWANGOSI?? yes daddy,, ilikuwaje??
"baba nina swali la uzushi, eti na kesi ya babu
Seya je?? WANANGU HILO SWALI MUULIZE
MJOMBA WAKO. HAYA WANANGU TUTAONGEA
KESHO NGOJA NIWAHI KAZINI.
MIMI NITAWAJIBU HIVYO WANANGU WEWE
JE??

Mkuu hawa wanetu km ni under 18, usiwajibu hivo, nnahofu utawaua
 
Huyu mama anaweza kujibu maswali ya watanzania kweli?
Sakata la escrow ulikaa kimya huku ukijua dhambi mnayofanya.
Bunge la katiba ukaridhia dhuluma kwa wananchi.
Dhuluma kwa mjane
 
Ameganya nini
Bungengeni hasemi wala kikemea maovu. Lambda wanaujua watujuze mchango wake kisiasA
 
Huyu mama yuko busy kutafuta mali za dunia hii,hamtumikii Mungu yoyote labda miungu
 
Kwa mimi ningemshauri arudi madhabahuni amlilie Mungu wake amsahemehe kwa kutowatetea watanzania kama bunge ndani ya Bunge. Na kwa kufumbia maovu.
mchungaji gani asiye kemea hata ovu moja linalo fanywa na serikali badala yake anaunga mkono.Ni aina ya wachungaji wachumia tumbo
 
Utumishi wa Mungu ni kujikana nafsi.Watumishi wengi wa Mungu aghalabu walikubaliana na watawala.Tawala nyingi zilizo kuwa onevu kwa watu wao zilipingana vikali na watumishi wa Mungu.Sasa huyu ni aina gani ya mchungaji hata wizi wa Escro ambaohata kipofu ameuona yeye anautetea.Atubu au la ajue mbingu hawezi kuziona kwa aina ya uchungaji wake huo
 
Back
Top Bottom