Siamini kama uvutaji wa sigara unasababisha Kifua Kikuu

JFK wabongo

JF-Expert Member
Aug 11, 2015
3,887
3,187
Nimefikia msimamo huo baada ya kutafakari haya:
1. Kiwango kikubwa cha matumizi ya tumbaku. Nimebahatika kutembelea mikoa mbalimbali hasa maeneo ya stendi za mabasi na baa na kujionea kiwango cha utumiaji wa tumbaku.
2. Kampeni ya kutokomeza TB. Wote mnajua kuwa serikali inaendesha kampeni ya kutokomeza TB kwa kutoa matibabu bure kwa wagonjwa.
Swali lililoniijia ni kama uvutaji wa sigara ungekuwa miongoni mwa visababishi vya TB mbona serikali haikigusi? Kwa nini serikali inaruhusu matumizi holela ya sigara ili baadae iingie gharama za kuwatibu waathiriwa?
Mpaka nitakapopata ushahidi tofauti ntaendelea kuamini kuwa uvutaji wa sigara hausababishi TB.
 
Ulishawahi ona semi au pulling la sigara?
Hata wakiweka kwenye mkokoteni zinalindwa.
Btw wanataaluma mkuje mtoe ufafanuzi wa kina.
 
Nimefikia msimamo huo baada ya kutafakari haya:
1. Kiwango kikubwa cha matumizi ya tumbaku. Nimebahatika kutembelea mikoa mbalimbali hasa maeneo ya stendi za mabasi na baa na kujionea kiwango cha utumiaji wa tumbaku.
2. Kampeni ya kutokomeza TB. Wote mnajua kuwa serikali inaendesha kampeni ya kutokomeza TB kwa kutoa matibabu bure kwa wagonjwa.
Swali lililoniijia ni kama uvutaji wa sigara ungekuwa miongoni mwa visababishi vya TB mbona serikali haikigusi? Kwa nini serikali inaruhusu matumizi holela ya sigara ili baadae iingie gharama za kuwatibu waathiriwa?
Mpaka nitakapopata ushahidi tofauti ntaendelea kuamini kuwa uvutaji wa sigara hausababishi TB.
Uvutaji wa sigara sio kwamba unaambukiza tb hapana ila unatakiwa utambue kuwa sigara ina athiri mapafu kwa asilimia 80-90% hivyo mapafu yanapokua yamechoka hushindwa kufanya kazi hasa ya usafishaji wa damu ikiwa ni kuiondoa carbondioxide na kuirudisha oxgen mwilini. Tatizo linakuja kwa wavutaji wa sigara ni kwamba atakapo pitia karibu na mtu mwenye tb kutokana na tayari mapafu yake yanakua yameathiriwa na moshi wa sigara basi inakua ni rahisi sana kuambukizwa kwa kupumua na kuvuta hewa na matone madogomadogo ya mate ambayo mtu mwenye vimelea vya tb huvikohoa sasa kama wewe unaendelea kuvuta sigara wewe endelea ila athari zake utaziona kipimdi mwili unahitaji hewa ya kutosha na wewe cells zako asilimia kubwa zimepunguza ufanyaji kazi ok
 
Kama ni hivyo kwa nini uvutaji wa sigara umeachwa ufanyike kiholela?
 
Uvutaji wa sigara hausababishi TB moja kwa moja (directly) ila una weka mazingira wezeshi kwa bacteria wa TB na magonjwa mengine kama vile pneumonia kuzaliana hadi dalili za ugonjwa zinajitokeza. Kwa kifupi ni hivyo
Umesomeka mkuu!
 
Kama ni hivyo kwa nini uvutaji wa sigara umeachwa ufanyike kiholela?
Unajua hata ngono hamna anae kuzuia kufanya ila anakuambia fanya ngono salama maana tunajua kuna ukimwi na ukiupata ukimwi utakufa tuu kwasababu utaanza maisha mapya ya kunywa dawa maisha yako yote

Ndivyo ilivyo uvutaji wa sigara kwa sasa hamna anaeweza kuzuia kuvuta ila siku utakapo kuja kupata kansa ya mapafu au tb vile vidonge vyake ndivyo vitakavyokuja kukufanya kuwa mwalimu mzuri wa somo hilo

Serikali haizuii uvutaji wa sigara kabisa kwasababu sigara ndio inaliingizia taifa mapato makubwa na hata ulinzi wake sio wa kawaida wa sigara na tumbaku ya kujazia vichungi

Ila tayari kuna onyo umepewa kwamba uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako basi sababu kuna onyo pale wewe endelea kutumia hauzuiliwi na yeyote yule
 
Sigara haisababishi TB,TB ni ugonjwa unasababishwa na bakteria aina ya Mycobacterium Tb. Sigara ni kichocheo au kisababishi cha kansa ya mapafu.
 
i
Nimefikia msimamo huo baada ya kutafakari haya:
1. Kiwango kikubwa cha matumizi ya tumbaku. Nimebahatika kutembelea mikoa mbalimbali hasa maeneo ya stendi za mabasi na baa na kujionea kiwango cha utumiaji wa tumbaku.
2. Kampeni ya kutokomeza TB. Wote mnajua kuwa serikali inaendesha kampeni ya kutokomeza TB kwa kutoa matibabu bure kwa wagonjwa.
Swali lililoniijia ni kama uvutaji wa sigara ungekuwa miongoni mwa visababishi vya TB mbona serikali haikigusi? Kwa nini serikali inaruhusu matumizi holela ya sigara ili baadae iingie gharama za kuwatibu waathiriwa?
Mpaka nitakapopata ushahidi tofauti ntaendelea kuamini kuwa uvutaji wa sigara hausababishi TB.
"EMPHYSEMA" una uhusiano mkubwa na uvutaji wa sigara , bangi ,Hewa yenye kemikali pamoja na mavumbi.
Ungonjwa huu huathiri vifuko vya hewa kwenye mapafu "alveoli / air sacs" ,vifuko hivi hupasuka na kutengeneza eneo/maeneo makumbwa yanayokuwa na hewa kwenye mapafu badala ya vifuko vidogo vidogo jinsi tulivyoumbwa,unaweza kuwa na tatizo hili kwa muda mrefu na bila kuoonyesha dalili zozote hatarishi ,na ishara kubwa ni kupungiwa hewa "shortness of breath" .
Ingia google soma ugonjwa huo utapata mengine ya ziada.
 
Back
Top Bottom