Kilimo na matumizi ya bidhaa za tumbaku upigwe Marufuku

Tony Laurent

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
3,121
2,000
Ikiwa madhara ya matumizi ya tumbaku/sigara ni makubwa kwa kiwango tunachoambiwa na wataalamu wa afya; kwanini Serikali isichukue hatua za kupiga marufuku kabisa uvutaji na ulimaji wa zao la tumbaku ili kuwanusuru Watanzania na vifo vinavyotakana na matumizi yake?

Kama tumepiga marufuku matumizi ya bangi, tunashindwa nini kupiga marufuku matumizi ya tumbaku?

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani, matumizi ya sigara/tumbaku husababisha vifo vya watu zaidi ya MILIONI NANE kwa mwaka. Kiwango hiki ni kikubwa sana kusababishwa na jambo linaloweza kuepukika.
 
Times9

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
3,147
2,000
Sigara zina hela sana, Sidhani ka sirikali watakuelewa kwa hili.

Ila ni bora wapige marufuku sigara afu waruhusu cannabis kwa sheria na utaratibu maalumu. Ukweli sigara zina haribu sana watu.
 
tony92

JF-Expert Member
Jul 17, 2013
1,151
2,000
Sigara zina hela sana, Sidhani ka sirikali watakuelewa kwa hili.

Ila ni bora wapige marufuku sigara afu waruhusu cannabis kwa sheria na utaratibu maalumu. Ukweli sigara zina haribu sana watu.
Sigara zinaharibu watu kweli kweni unalazimishwa kuvuta?
 
Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
10,270
2,000
Watu milioni NANE tu ni wachache mno kwenye dunia hii, hivyo acha waendelee kufa tu hadi akili [kama wanazo] ziwakae sawa.

Tumbaku haina faida yoyote KIAFYA, na kwenye sigara kuna ONYO lakini wapi…. ni bora BANGI ina proved benefits kuliko tumbaku.
 
jiwe angavu

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
4,826
2,000
Hivi unajua TCC inachangia pato kiasi gani nchi hii..acha washiriki kukuza uchumi mana hata wavutaji wanajua madhara wameamua wenyewe..kwani nikuulize kuna faida gani ukifa na mapafu mazima.?

Mimi naomba serikali ianze kutoza kodi pia kwa wadangaji mana hii biashara ni kubwa na ina mzunguko mkubwa wapesa...na wateja wapo wa uhakika mana nyege haziishi na kil siku watu wana balehe so ni biashara endelevu.

#MaendeleoHayanaChama
 
tony92

JF-Expert Member
Jul 17, 2013
1,151
2,000
Situmii sigara wala cannabis ila mazingira nilipo kuna wavuta sigara vijana wengi sana na baadhi naona wanalalamika vifua vinawabana na wanakohoa sana usiku.
Tatizo bado ni la hao vijana wenyewe maana madhara ya uvutaji sigara yanajulikana sasa kama waliendelea kuvuta walikua wanategemea nini?
 
Mtukutu wa Nyaigela

JF-Expert Member
Sep 4, 2018
3,867
2,000
Ikiwa madhara ya matumizi ya tumbaku/sigara ni makubwa kwa kiwango tunachoambiwa na wataalamu wa afya; kwanini Serikali isichukue hatua za kupiga marufuku kabisa uvutaji na ulimaji wa zao la tumbaku ili kuwanusuru Watanzania na vifo vinavyotakana na matumizi yake?

Kama tumepiga marufuku matumizi ya bangi, tunashindwa nini kupiga marufuku matumizi ya tumbaku?

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani, matumizi ya sigara/tumbaku husababisha vifo vya watu zaidi ya MILIONI NANE kwa mwaka. Kiwango hiki ni kikubwa sana kusababishwa na jambo linaloweza kuepukika.
bangi imepigwa marufuku wapi mkuu
njoo hapa tarime ujionee au arumeru
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom