Siamini kama uvutaji wa sigara unasababisha Kifua Kikuu

Unajua hata ngono hamna anae kuzuia kufanya ila anakuambia fanya ngono salama maana tunajua kuna ukimwi na ukiupata ukimwi utakufa tuu kwasababu utaanza maisha mapya ya kunywa dawa maisha yako yote

Ndivyo ilivyo uvutaji wa sigara kwa sasa hamna anaeweza kuzuia kuvuta ila siku utakapo kuja kupata kansa ya mapafu au tb vile vidonge vyake ndivyo vitakavyokuja kukufanya kuwa mwalimu mzuri wa somo hilo

Serikali haizuii uvutaji wa sigara kabisa kwasababu sigara ndio inaliingizia taifa mapato makubwa na hata ulinzi wake sio wa kawaida wa sigara na tumbaku ya kujazia vichungi

Ila tayari kuna onyo umepewa kwamba uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako basi sababu kuna onyo pale wewe endelea kutumia hauzuiliwi na yeyote yule
Ngono ni hitaji la mwili mkuu, kwa mwanadamu aliyekamili ni ngumu kuishi bila yenyewe. Ila moshi wa sigara anaouvuta mvuta sigara hauna value yoyote kwenye mwili wake.
 
i

"EMPHYSEMA" una uhusiano mkubwa na uvutaji wa sigara , bangi ,Hewa yenye kemikali pamoja na mavumbi.
Ungonjwa huu huathiri vifuko vya hewa kwenye mapafu "alveoli / air sacs" ,vifuko hivi hupasuka na kutengeneza eneo/maeneo makumbwa yanayokuwa na hewa kwenye mapafu badala ya vifuko vidogo vidogo jinsi tulivyoumbwa,unaweza kuwa na tatizo hili kwa muda mrefu na bila kuoonyesha dalili zozote hatarishi ,na ishara kubwa ni kupungiwa hewa "shortness of breath" .
Ingia google soma ugonjwa huo utapata mengine ya ziada.
Kama hata vumbi linahusika basi watumiaji wengi bodaboda kwenye barabara za vumbi vijijini watapata shida ya mapafu.
 
Kama hata vumbi linahusika basi watumiaji wengi bodaboda kwenye barabara za vumbi vijijini watapata shida ya mapafu.
Mkuu soma kwa utulivu upate maana, ni kweli unachokisema ila kuonekana kwa uzito wa athari hizo pia inategemea mtu na mtu na vilevile kupata athari kutokana na kisababishi (causing factors) fulani kuna "factors" nyingi tu ,ikiwemo uimara wa mwili wa mtu mwenyewe na hata kiwango (dose) cha kisababisha tatizo na vitu vingine vingi vya kuzingatia .Mfano tukitumia gm 50 za sumu ya panya mimi na wewe na tukainywa kwa wakati mmoja kiwango sawa mie naweza kuathirika vibaya na nikapoteza maisha au kinyume chake.Ila ukiingia google ukapitia kidogo utapata maana halisi ya hilo tatizo nililolisema.
 
Kama ni hivyo kwa nini uvutaji wa sigara umeachwa ufanyike kiholela?
Ndiyo maana makampuni ya sigara wamelazimishwa kuandika ktk packet uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako.Sasa hapa utashi wako unatakiwa kuutumia vema....
 
Ndiyo maana makampuni ya sigara wamelazimishwa kuandika ktk packet uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako.Sasa hapa utashi wako unatakiwa kuutumia vema....
Hiyo kauli ya uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako ni upotoshaji mkubwa. Tafiti zinasema kuwa secondary smokers wana hatari kuliko mvutaji mwenyewe. Yaani ukikaa karibu na anayevuta sigara unaweza kuwa katika hatari kubwa ya kuathiriwa na sigara kuliko mvutaji mwenyewe. Mimi ningewaona wa maana kama wangeandika usivute sigara kwenye mikusanyiko ya watu.
 
Madhara ya uvutaji sigara ni makubwa kuliko faida inayopatikana kwa mvutaji. Miongoni mwayo ni pamoja na kifua kikuu au hata wakati mwingine saratani ya mapafu. Pichani hapa chini ni aina mbili za watu. Mmoja ambaye anavuta sigara na amepata maambukizi ya saratani na mwingine ambaye havuti sigara.
 
Madhara ya uvutaji sigara ni makubwa kuliko faida inayopatikana kwa mvutaji. Miongoni mwayo ni pamoja na kifua kikuu au hata wakati mwingine saratani ya mapafu. Pichani hapa chini ni aina mbili za watu. Mmoja ambaye anavuta sigara na amepata maambukizi ya saratani na mwingine ambaye havuti sigara.
Kweli kabisa, jambo la kushangaza ni serikali japo inajua kuwa sigara zinaathiri wanaovuta na hata wasiovuta ila wanaacha zinavutwa kiholela maeneo ya mikusanyiko ya watu.
 
Back
Top Bottom