Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,640
- 729,670
Pale ndipo penye makazi ya wafu, watu waliokuwa hai na kuishi juu ya ardhi sasa wameshuka na kupumzika pale ! Ile ni miili tupu lakini tusisahau kuwa roho zao hazichezi mbali hata kama zitaenda kutangatanga huko na huko lakini ile energy ipo pale
Kujenga chochote juu ya makaburi ni kutafuta bifu na marehemu ni kuwaingilia kwenye makazi yao rasmi! Kwani huna pengine pa kujenga?
Makaburi ya zamani yalikuwa makubwa sana, mengi yalijengwa mfano wa nyumba milima nk angalia ma pyramid ya Misri nk...makaburini ni sehemu iliyoheshimika mno na kwa namna fulani kuogopwa
Wengi wetu tunajua kabisa kule vijijini tuna maeneo rasmi ya kifamilia ya kuwazika waliotutangulia na makabila mengi hufika makaburini mara moja au mbili kwa mwaka kuyafagilia kufanya ibada na matambiko! Kwa baadhi yetu hata mambo yanapoharibika kifamilia au kiukoo hurudi makaburini na kuomba rehema ulinzi na hata msamaha kwa wakubwa Waliolala pale
Kuna visa vingi vya makaburini vingine vya kweli vingine vya uongo na vingine vipo lakini vimekuzwa mno...pamoja na hayo yote bado makaburini panabaki mahali maalum penye kustahili faragha na heshima yake
Tunavyo visa vingi kwenye maeneo yote ambayo makaburi yaliondolewa ama kuhamishwa kiholela kwa ajili ya kufanya mambo mengine kama ujenzi wa shule hospitali barabara nk nk...maeneo hata yamekuwa yakikumbwa na matukio mbalimbali hasa ajali na vifo
Dunia yetu ya kisomi na maendeleo ya kiteknolojia inatupumbaza na kutufundisha ujinga mwingi...tusitekwe na mambo ya kisasa na kisayansi...makaburini kuna maisha ya wafu paheshimiwe