Si sahihi kusema"kuoana" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Si sahihi kusema"kuoana"

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Kipilipili, May 22, 2011.

 1. Kipilipili

  Kipilipili JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2011
  Joined: May 25, 2010
  Messages: 2,204
  Likes Received: 477
  Trophy Points: 180
  Neno kuoana lipo katika kauli ya kutendana,hivyo tunenapo kuwa"wameoana jana"si sahihi kwani mke haoi bali anaolewa,na mume ndo anaoa.
   
 2. blackdog

  blackdog Member

  #2
  May 22, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  ohh,mkuu inategemea kuwa umelichukuliaje neno hilo,
  mimi ninaweza kukuelezea kutokana na uelewa wangu wana JF watanisaidia kama nimekosea nitafafanua kama ifuatavyo:-

  1. KUOA- Ni mwanandoa moja anatoa gharama kumchukua mwenzi wake,naye atakuwa na nguvu katika mahusiano yao kuliko mwingine (mfano Wahindi Mwanamke hutoa Mahari ndiye anayeoa,Waafrika vivyo hivyo)
  2. KUOANA;-wote wanachangia gharama za kuwa wanandoa(Mfano Wazungu wote anakuwa na uwezo sawa ndani ya ndoa)
  Neno kuoa linamfanya moja kuwa Bwana na mwingine Mtwana,neno Kuoana linafanya wote kuwa sawa (life partner sio Slave)
   
 3. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Athari za waziwazi za tafsiri sisisi ya sentenso ya kiIngereza, 'They got married.
  I married HIM.
  I married HER.
  Kwa kiIngereza ni 'kuoana' na inatofautisha na matumizi ya kiwakilishi tu.

  Naamini kwa utamaduni wetu ni sahihi kusema, 'Ameoa' kama ni mwanamume na 'Ameolewa' kama ni mwanamke. Naacha mjadala uendele katika 'wameoana'
   
 4. MAHENDEKA

  MAHENDEKA JF-Expert Member

  #4
  May 23, 2011
  Joined: Jul 9, 2010
  Messages: 257
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Lugha ni sauti za nasibu zinazozuka kibahati bahati tu na kutumika kwenye jamii bila makubaliano maalum..Hakuna fomula inayohakikisha kwamba tendo la "kuoa" lina uhusiano wa moja kwa moja na tendo la mwanamume kumtwaa na kummiliki mwanamke.Mimi naweza kusema hivi, kuoana ni kufanana tabia au sifa fulani fulani na bado nikawa sahihi vilevile, mfano nikisema,tabia za alex na musa zinaoana(zinafanana), au nikisema magari haya yanaoana(yanafanana)..je na hapa utasema nimekosea?
   
 5. Kipilipili

  Kipilipili JF-Expert Member

  #5
  May 25, 2011
  Joined: May 25, 2010
  Messages: 2,204
  Likes Received: 477
  Trophy Points: 180
  Nadhan turejee kwenye maana ya msingi niliyoikusudia,nayo ni ile ya mkataba wa hiari ya watu wa jinsi mbili kukubaliana kuishi pamoja wakiwa mke na mume/wenza{ndoa} kwa mujibu wa mila na tamaduni za tanzania,dhana ya kufanana ni maana ya ziada ambayo si ile niizungumzayo mm.kwa tamaduni za tanzania mume huoa na mke huolewa,hivyo tunaposema "kuoana" maana yake ni kuwa hawa watu wametendana yaani kila mmoja ameoa,kitu ambacho kwa utamaduni wetu c sahihi.lazma mfahamu kuwa lugha ni sehemu ya utamaduni,hvyo lazma ifate kaida za utamaduni.hivyo c sahihi kusema "wameoana"kwani mke haoi jamani.jifunzeni kiswahili acheni siasa.
   
 6. S

  Senior Bachelor Member

  #6
  May 28, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana kabisa na Pangu pakavu, Gurta na Mahendeka. Kuoa ni neno la kiswahili na sio la kiingereza. Kutafsiri "get married" kuwa kuoana sio sahihi. Kuoa ni kitendo cha mwanamume kumlipia mahari mwanamke na kumchukua kuishi naye kama mke na mume. Mwanamume huoa na mwanamke huolewa. Na kusema kuoa au kuolewa kwa namna yoyote haimaanishi kutokuwapo na usawa kati yao. Kama ilivyoelezwa lugha haina mantiki katika uchaguzi wa dhana gani ibebe maana gani. Kwa hiyo sio sahihi kujaribu kuchukua mantiki ya lugha moja na kuibambikiza kwenye lugha nyingine.

  Chukulia tena mifano hii.:
  1. Kiswahili: Baba mdogo
  Kiingereza: Uncle
  2.Kisw: Mjomba
  Kiing: Uncle
  3: Aunt (shangazi, mama mdogo) n.k

  Kwa hiyo kila lugha ina mpangilio na namna zake.
   
 7. Kipilipili

  Kipilipili JF-Expert Member

  #7
  Jun 6, 2011
  Joined: May 25, 2010
  Messages: 2,204
  Likes Received: 477
  Trophy Points: 180
  Swadakta senior bachelor,ulisemalo ni zaidi ya sahihi.ila kaka katika kudumisha lugha yetu adhimu unaonaje kama hilo jina lako likawa kwa kiswahili mf.MSEJA MWANDAMIZI badala ya senior bachelor?
   
 8. S

  Senior Bachelor Member

  #8
  Jun 7, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umenena mkubwa. Japo sio mseja mwandamizi kweli nitabadili kwa heshima yako. hahahah
   
 9. Kipilipili

  Kipilipili JF-Expert Member

  #9
  Jun 12, 2011
  Joined: May 25, 2010
  Messages: 2,204
  Likes Received: 477
  Trophy Points: 180
  Hahahahaha!mseja mwandamizi nimekukubali kaka.c unaona miye "pangu pakavu".usishangae kaka majina hubeba maana kubwa ndani yake.kiswahili hazina na urithi wa taifa letu.
   
Loading...