Si kila kitu kinastahili kutamkwa hadharani vingine ni vya siri!

Blue G

JF-Expert Member
Jun 20, 2012
5,213
2,000
Sijui sana labda ndio kwenda na wakati au mimi ni mshamba.

Kuna tabia imezuka sana kwa sasa tabia ya kutaja hadhrani viungo vya siri au sehemuza siri au matendo yanayopaswa kufanywa sirini bila yeyote kujua isipokuwaninyi wawili mnaoyafanya.

Siku hizi imekuwa ni kawadia ya watu kuongelea vitu au mambokama hayo hadharani tena bila tafsida wala kificho chochote,tena wakatimwingine hata mbele ya watoto zao au hata wa majirani,huenda kuna ugomvi umetokea na hivyo watu kuanzakurushiana maneno makali kama hayo au stori zinapigwa watu wanajisemea tu kilakitu bila tafsida,utakuta k**a wewe m** wewe au kama ni stori utakuta jamaa ana***a huyo au binti ana*****wa huyohapo ni stori zinapigwa na mtu anaonakawaida kabisa wala haoni taabu na hata ukithubutu kumuuliza au kumwambiamwenzangu vipi anakujibu kwani nini usichokijua?nini cha ajabu?au nini kigeni? wehufanyagi hayo mambo?

Na mimi nasema sawa hata kama tunayafanya au viungo hivyotunavyo tunavitaja ili iweje na pengine hata mbele za watoto jiulize haya:

1.Kwa nini hujawahi kufanya mambo unayoyafanya sirinibarabarani tena mchana kweupe?unaogopa nini kama ni vitu vya kawaida?

2.Kwa nini tunavaa nguo basi kama viungo hivyo ni kawadia nakila mtu anavyo,si tutembee uchi sasa kama ni kawaida?tunaficha nini?

3.Mbona basi tafsida ziliwekwa?ziliwekwa ili iweje ikiwaviungo au mambo hayo ni ya kawadia kabisa na yanafaa kutamkwa hadharani?

4.Ukimkuta mwanao anayatamka maneno kamahayo,utajisikiaje?utamwacha?kama ukimchapa kwa nini umchape wakati ni yakawaida sana?

5.Kwa nini tunapotaka kujisaidia,kustarehesha miiliyetu(wakubwa mnanielewa)tunatafuta sehemu iliyo tulivu na isiyo na watu nakufanya mambo hayo?wakati mwingine hatutaki hata watoto wawepo,tunasubiri wawewamelala au wameenda shuleni?kwa nini hatufanyi hadharani mbele za wageniwaliotutembelea au hata mashosti wetu tunaopiga nao stori?

Kama kuongea ni kawaida basi na kuyafanya tuwe tunayafanyahadharani basi kila mtu awe anatushudia na tusiwe tunavaa nguo basi ilituviache viungo vyetu vionekane na kila mtu,si ni kawaida na si kila mtu anavyo?
Wana mmu mnasemaje manafikiri ni sawa kufanya hivyo?kwamisingi ipi?mnafikiri nini kinaweza kufanyika kuepusha kizazi kinachokuja kuwakibaya zaidi kwa kujiongelea chochote bila haya wala kusutwa na nafsi?

Ni hayo tu wana MMU nawasilisha karibuni tujadili kwa pamoja.
 
SURUMA

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
2,901
1,250
Unavyosikia KUPOROMOKA KWA MAADILI katika JAMII ulikuwa hujui viashiria vyake ????
 
Blue G

JF-Expert Member
Jun 20, 2012
5,213
2,000
viashiria ndo hivyo lakini je basi tunastahili kukaaa tu kimya na kuacha watoto wetu waharibike bila kuchukua hatua yeyote kwa kuacha viashiria vitawale na kuharibu watoto wetu kirahisi tu?
Unavyosikia KUPOROMOKA KWA MAADILI katika JAMII ulikuwa hujui viashiria vyake ????
 
Blue G

JF-Expert Member
Jun 20, 2012
5,213
2,000
ni kweli mbalu lakini je hiyo ni sababu tosha ya kuacha tu watoto wetu waharibike sababu tu maadili yameporomoka?hatupaswi kuchukua hatua yoyote ile?
Siku za mwisho maadili kuporomoka.
 
Last edited by a moderator:

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
148,680
2,000
kuna baadhi ya vyombo vya habari hasa magazeti ya udaku yanaongoza kuandika upuuzi na mambo ambayo ni ya faraghani kuyaanika hadharani
 
Mtoto halali na hela

JF-Expert Member
Aug 10, 2012
30,656
2,000
Tushachelewa, nenda kwenye baadhi ya makampuni wanayofanya kazi nzito utasikia yakutisha. Utadhani ni watu wa rika moja, wakati kuna hadi baba na babu zao. Ila ndio kinogesha kazi, wakikaa kimya kazi haiendi.
 
Blue G

JF-Expert Member
Jun 20, 2012
5,213
2,000
hujakosea mshana jr lakini je hiyo ni sababu tosha ya hata wewe kukaa tu na kuruhusu mwanao asikie na kutumia maneno hayo kisa tu vyombo vya habari vinayaweka hadharani?utajisikaje ikiwa mwanao anayatumia maneno hayo?
kuna baadhi ya vyombo vya habari hasa magazeti ya udaku yanaongoza kuandika upuuzi na mambo ambayo ni ya faraghani kuyaanika hadharani
 
Last edited by a moderator:

Blue G

JF-Expert Member
Jun 20, 2012
5,213
2,000
Mtoto halali na hela kweli unaamini tumeshachelewa?kwa maana nyingine hata mtoto wako utamnyamazia tu na kumwacha asikie hata maneno yaisyofaa kwa kigezo tumesha chelewa?
Tushachelewa, nenda kwenye baadhi ya makampuni wanayofanya kazi nzito utasikia yakutisha. Utadhani ni watu wa rika moja, wakati kuna hadi baba na babu zao. Ila ndio kinogesha kazi, wakikaa kimya kazi haiendi.
 
Last edited by a moderator:

illuh

JF-Expert Member
Mar 17, 2014
1,259
1,195
Mbona ktk movies za kidhungu na hata ktk chanel ya E- entertainment wanakuwa wanaongea wanatamka A*** hamzimi tv? au sababu kile ni kizungu ? Utamsikia mtu anasema F**K ma A**...watu mnachekelea
 
Ennie

JF-Expert Member
Jan 15, 2011
7,140
2,000
Mtoto halali na hela kweli unaamini tumeshachelewa?kwa maana nyingine hata mtoto wako utamnyamazia tu na kumwacha asikie hata maneno yaisyofaa kwa kigezo tumesha chelewa?

Unamaanisha nini by kumwacha asikie?
Watoto hatuwalelei ndani tu,anaenda shule anayasikia,anapanda daladala anayasikia,akienda kucheza anayasikia na pengine hata hapo nyumbani yanasemwa kama hupo.
Ukisikia anatamka badala ya kumpiga mdadisi kwanza ujue anafahamu kiasi gani then from there utajua cha kumwambia ukizingatia umri wake pia.
 
Asprin

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
61,727
2,000
hujakosea mshana jr lakini je hiyo ni sababu tosha ya hata wewe kukaa tu na kuruhusu mwanao asikie na kutumia maneno hayo kisa tu vyombo vya habari vinayaweka hadharani?utajisikaje ikiwa mwanao anayatumia maneno hayo?

Sasa bluu jii, viungo na vitenzi tangu lini vikawa matusi. Kuvidhalilisha viungo ndo matusi bhana. yani ukisema mbo.o yako mbaya hapo ndo tusi. lakini mbo.o kama mbo.o sio tusi bhana. Na kitenzi pia sio tusi hata siku moja. kama ambavyo kulima siyo tusi kwa kuwa ni kitendo, basi hata kunya, kujamba na kutomba haipaswi kuwa tusi.

Samahani kuna mtu nilimwazima pasiwedi yangu, sijaandika mimi hapa.
 
Last edited by a moderator:

Simplicity.

JF-Expert Member
Dec 19, 2013
2,645
2,000
There is nothing you can do to change this course. The Second Law of Thermodynamics (Entropy) explained (Psalm 102:25-26) states that, everything in the universe is running down, deteriorating, constantly becoming less and less orderly. Entropy (disorder) entered when mankind rebelled against God – resulting in the curse (Genesis 3:17; Romans 8:20-22). The world cannot be restored, and is constantly growing old like a garment (Hebrews 1: 11).
 
Mtoto halali na hela

JF-Expert Member
Aug 10, 2012
30,656
2,000
Mtoto halali na hela kweli unaamini tumeshachelewa?kwa maana nyingine hata mtoto wako utamnyamazia tu na kumwacha asikie hata maneno yaisyofaa kwa kigezo tumesha chelewa?

watoto kwa asilimia kubwa tunaishi nao kwa muda mchache sana, wanasikia mengi wawapo mashuleni na barabarani. Ila mtoto mwenye maadili hutokaa umsikie akiyatamka mbele yako, endapo umri wake ushavuka miaka mitano
 
Last edited by a moderator:

Asprin

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
61,727
2,000
Unamaanisha nini by kumwacha asikie?
Watoto hatuwalelei ndani tu,anaenda shule anayasikia,anapanda daladala anayasikia,akienda kucheza anayasikia na pengine hata hapo nyumbani yanasemwa kama hupo.
Ukisikia anatamka badala ya kumpiga mdadisi kwanza ujue anafahamu kiasi gani then from there utajua cha kumwambia ukizingatia umri wake pia.

umbuje wa hommie, unajua kuna watu wanahisi kutamka ni mbaya sana kuliko kutenda. Mtu anashtuka zaidi akisikia tusi kuliko akishuhudia matusi. Na huu utandawazi utawazuiaje watoto matusi wakati anaona vitu hadharani. Anaweza asitukane mbele yako lakini kumbe ni mtukanaji aliyekubuhu. Mungu atunusuru.
 
mbalu

JF-Expert Member
May 18, 2012
551
195
ni kweli mbalu lakini je hiyo ni sababu tosha ya kuacha tu watoto wetu waharibike sababu tu maadili yameporomoka?hatupaswi kuchukua hatua yoyote ile?

Wazazi wa sasa ni Dot.Com hivyo kuona ni maendeleo, zamani tulipokuwa tukikosea tuliadhibiwa hata na mpita njia leo hii jaribu utafatwa na PF 3.
 
Ennie

JF-Expert Member
Jan 15, 2011
7,140
2,000
umbuje wa hommie, unajua kuna watu wanahisi kutamka ni mbaya sana kuliko kutenda. Mtu anashtuka zaidi akisikia tusi kuliko akishuhudia matusi. Na huu utandawazi utawazuiaje watoto matusi wakati anaona vitu hadharani. Anaweza asitukane mbele yako lakini kumbe ni mtukanaji aliyekubuhu. Mungu atunusuru.

Ulezi umekuwa na changamoto sana na huu utandawazi hommie wake.
Umakini unahitajika sana tena bila jazba hata kidogo.
Mungu atunusuru tu na vizazi vyetu!!!
 
Blue G

JF-Expert Member
Jun 20, 2012
5,213
2,000
nani wanaochekelea wewe au?kwa hiyo kwa kuwa channel hizo zinataja mambo waziwazi basi ndo sababu ya kutufanya na sisi tuige tu kuongea upuuzi hata mbele za watotot?
Mbona ktk movies za kidhungu na hata ktk chanel ya E- entertainment wanakuwa wanaongea wanatamka A*** hamzimi tv? au sababu kile ni kizungu ? Utamsikia mtu anasema F**K ma A**...watu mnachekelea
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom