Si bure kuna roho ya ubahili inanifuatilia

Si bure kuna roho ya ubahili inanifuatilia

doppla2

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2014
Posts
1,393
Reaction score
1,462
Salaam wakuu.....

Niende kwenye mada tajwa moja kwa moja

Kwa siku napokea simu zisizopungua 10 kutoka kwa marafiki, ndugu na hata wafanyakazi wenzangu.

Kati ya hizo 4 hadi 6 lazima ziwe zimejaa matatizo na kwa namna moja au nyingine zinahitaji msaada wangu na hasa wa pesa.

Mwanzoni nilijitahidi kweli kuhakikisha napambana japo niitwe problem solver na nifanyike ndg, au jamaa ninayejari na kuwepo wakati wa shida na raha.

Ila kadri nilivyojitahidi uhiitaji uliongezeka hadi kufikia nikaanza kuhairisha mambo yangu na familia yangu ili wengine wanione ni mtu wa kushirikiana na watu.

Kilichoniuma ni juzi nikiwa narudi toka kazini nikamfuma wife na watoto wangu wakiongea katika simu kuwa baba amekua bahili na wala hawana furaha na kipato changu, kwani niko radhi kuwanyima furaha wao ili wapendendwa kanisani, wachungaji na marafiki wanione mtu bomba.

Kiukweli toka that day najiona looser ....hali iliyopelekea nmechange hata namba za simu na kuna roho inanishawishi atleast niitwe bahiri lakini familia yangu inione mshua.

Lakini kimtindo inside my heart najiona lm not real me, coz najilazimisha kuwa bahili wakati my heart inanishuudia lm a Generous person


Wakuu hii hali ni yakawaida au kuna kanuni nazikihuka katika maisha ya familia?
Leteni uzoefu ili tujifunze....

Regards
 
mkuu uwezi mlizisha kila mmoja nazan umesahau kwamba familia kwanza then wengne wafate hao wanao kuomba wana option ingne kma utawanyima ila familia yako ni kazma
 
familia yako ni bora kuliko chochote.......muonyeshe ng'ombe njia ya kwenda mtoni sio kumletea maji......
 
Mbona hali ya kawaida sana hiyo mkuu. Na kama unataka kuwa na maendeleo makubwa hakima lazima u save pesa kwa maendeleo ya baadae . Hivyo endelea ku save pesa kwa ajili ya familia yako
 
Vitu vingine ni ngumu kubadilisha kabisa. Labda upunguze na sio kuacha kabisa ili undelee kuwa wewe.
Na kama ni tabia yako kuwa mkarimu jitahidi jali watu usiowajua maana wao hawarudi na wala zile sifa ambazo unazitengeneza kwa wanaokujua hutazipata, utaridhika na utapunguza matumizi.
 
Jali familia yako kwanza.. Hiyo kujifanya una moyo wa huruma kuliko Bwana Yesu itakuja kukucost.. Kati ya hao unaowasaidia ukija kufikwa na tatizo kuna uwezekano mkubwa asitokee wa kukusaidia zaidi ya mkeo..
 
Money is the energy,people will want to drain your Energy.,be aware of energy vampires.... mi nmekuwa bandidu htr
 
Mtu yeyote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.

1Tim5:8
 
Kuna tatizo linaitwa "development fatigue". Yani ni pale ambapo mtu anayesaidia ili kuleta maendeleo anapochoka kusaidia kwa kuona kila anavyosaidia, hali haibadiliki.

Kuna dada mmoja wa kizungu alikuwa na bwana wake Muafrika, huyu dada alimpenda sana yule mwanamme, akawa tayari kumsaidia sana. Mwanzoni akawa anampa hela sana kwa sababu alijua Africa kuna matatizo mengi. Lakini mwishowe akachoka, akasema huyu jamaa sasa naona kanifanya kama ATM.

Kuna njia nyingi za kuondokana na hali hiiya kuchoka au kusaidia isivyostahili.

1. Ongeza kipato uweze kusaidia watu wengi bila kujihisi unakosa fedha/mali zako kwa sana. Hili si rahisi.

2. Punguza marafiki na ndugu tegemezi. Ukiwa nao wengi hawa, kukulilia njaa ni lazima.

3. Saidia watu kwa vitu ambavyo vitawapa maendeleo endelevu kiasi cha kwamba wasiweze kuhitaji msaada wako kwa sana tena. Binafsi nimesaidia cousin mmoja kumsomesha kuanzia shule ya sekondari, A Level mpaka Chuo Kikuu. Leo hii ni daktari. Nimekuja kupata habari kwamba kuna siku baba yangu alipata haja ya kusaidiwa katika mambo ya afya, huyu Daktari wetu mpya niliyesaidia kumsomesha, akamsaidia sana. Pengine hapa ningetakiwa mimi kutoa msaada tena kwa Baba yangu,lakini nilikuwa nimeshatengeneza mazingira ya familia kuwa na daktari wa karibu atakayeweza kusaidia ushauri na hata mali kama msaada wa karibu utahitajika. Tangu dogo awe daktari hajawahi kuniomba msaada wa fedha, sanasana tunazungumzia mikakati ya maisha tu.

4. Saidia watu wenye kuweza kusaidika. Si kila mtu anasaidiaka, wengine ni "bottomless money pit". Mfano, huyo dogo tangu shule ya sekondari alionekana ni bright, ila kazaliwa kwa ndugu fulani ambao walikuwa hawajiwezi sana kiuchumi. Unaona kabisa hapa tuna mtu ana talent lakini anaweza kukosa maisha mazuri na hata familia/ nchi ikakosa daktari mzuri kwa sababu ya investment ndogo tu ya miaka michache.

5. Wachina wana msemo, ukimpa mtu samaki, umemlisha mara moja, ukimfundisha kuvua samaki, umemsaidia kuweza kujilisha maisha yake yote. Msaada wangu huo wa daktari ulikuwa wa kumfundisha kuvua samaki.A skill to earn a living, a marketable one, a useful one. Sio kila mtu anayekuomba hela ya kuweka mafuta ya nywele anafaa kusaidiwa.

6. Saidia watu wanaokuhusu. Waswahili walisema "Mtaka nyingi nasaba, hupata mwingi msiba". Tunapenda kuwa na msaada kwa watu wengi sana, wengine hata hawatuhusu hivyo. Ukitaka kuisaidia dunia nzima utakufa masikini.

7. Weka bajeti ya kusaidia watu. Halafu ukiona imeisha, hata pale unapotaka kusaidia, waambie watu jamani eeh, nilikuwa na bajeti ya kusaidia watu, kwa sasa nimeimaliza mpaka baadaye labda. Kwa anayejua habari zako, hawezi kukulaumu. Huwezi kuwa wewe ndiye unayesaidia watu kila siku bila kuangalia bajeti.

8. Saidia kwa priority. Jiwezeshe wewe mwenyewe na familia yako kuweza mambo makubwa zaidi kwanza, halafu saidia, ama sivyo, utashindwa kabisa kusaidia yeyote na hata wewe mwenyewe utakuwa mzigo kwa wengine.

9. Saidia kwa kutojionesha sana. Kusaidia kwa kujionesha sana kunaalika waomba misaada ambao wengine hata hawana shida ya kustahili kupata misaada. Wanaona tu hapa kuna hela zinatoka kirahisi, na sisi tutengeneze shoida ya uongo nakweli tu,tupate hela.

10. Saidia bila kufuata mkumbo. Saidia kwa sababu zako, zinazo make sense kwako, sio umeona mtu anatoa sadaka sana kanisani hujui hata mpango wake na mchungaji kama anarudishiwa baada ya misa, anatoa kama chambo kuwanasa wengine wamuige, na wewe unashindana naye kutoa sadaka.

Hayoni machache kutoka kwangu.

Nilishaambiwa katika list zangu nisizidi mambo kumi, kwa maana hata Mungu amri zake zikokumitu (joke)

Zaidi wengine wataongezea.
 
Kuna raha gani ya kuitwa mkarimu wakati Mke na watoto wako wanakuona bahili kwao?

Cha kwanza mshirikishe Mkeo hayo mapato yako itakusaidia kutotoa ovyo pesa lakin atakukumbusha matumizi ya lazima kabla ya kutoa pesa.

Pili Wekeni pasent labda 7% ya mapato Kwa mwezi ndio itatumika kutoa msaada ikiisha hiyo basi isitoke nyingine.
 
Aisee, katika kitu kikubwa nilichojitahidi ni kuepuka kubeba mizigo ya watu.

Kila mtu apambane na hali yake
 
Kuna raha gani ya kuitwa mkarimu wakati Mke na watoto wako wanakuona bahili kwao?

Cha kwanza mshirikishe Mkeo hayo mapato yako itakusaidia kutotoa ovyo pesa lakin atakukumbusha matumizi ya lazima kabla ya kutoa pesa.

Pili Wekeni pasent labda 7% ya mapato Kwa mwezi ndio itatumika kutoa msaada ikiisha hiyo basi isitoke nyingine.
Nimekuelewa sana mkuu
Asante
 
Kuna tatizo linaitwa "development fatigue". Yanini pale ambapo mtu anayesaidia ilikuleta maendeleo anapochoka kusaidia kwa kuona kila anavyosaidia, hali haibadiliki.

Kuna dada mmoja wa kizungu alikuwa na bwana wake Muafrika, huyu dada alimpenda sana yule mwanamme, akawa tayari kumsaidia sana. Mwanzoni akawaanampahela sana kwa sababu alijua Africa kunamatatizo mengi. Lakini mwishowe akachoka, akasemahuyu jamaa sasa naona kanifanya kama ATM.

Kuna njia nyingi za kuondokana na hali hii.

1. Ongeza kipato uwezekusaidia watu wengi bila kujihisi unakosa fedha/mali zako kwa sana. Hili si rahisi.

2. Punguza marafiki na ndugu tegemezi. Ukiwa nao wengi hawa, kukulilia njaa ni lazima.

3. Saidia watu kwa vitu ambavyo vitawapamaendeleo endelevu kiasi cha kwamba wasiweze kuhitaji msaada wakokwa sana tena. Binafsi nimesaidia cousin mmoja kumsomesha kuanzia shule ya sekondari, A Level mpaka Chuo Kikuu. Leo hii ni daktari. Nimekuja kupata habari kwamba kuna siku baba yangu alipata haja ya kusaidiwa katika mambo ya afya, huyu Daktari wetu mpya niliyesaidia kumsomesha, akamsaidia sana. Pengine hapa ningetakiwa mimi kutoa msaada tena kwa Baba yangu,lakini nilikuwa nimeshatengeneza mazingira ya familia kuwa na daktari wa karibu atakayeweza kusaidia ushauri na hata mali kama msaada wa karibu utahitajika. Tangu dogo awe daktari hajawahi kuniomba msaada wa fedha, sanasana tunazungumzia mikakati ya maisha tu.

4. Saidia watu wenye kuweza kusaidika. Si kila mtu anasaidiaka, wengine ni "bottomless money pit". Mfano, huyo dogo tangu shule ya sekondari alionekana ni bright, ila kazaliwa kwa ndugu fulaniambaowalikuwa hawajiwezi sana kiuchumi. Unaona kabisa hapa tuna mtu ana talent lakini anaweza kukosa maisha mazuri na hata familia/ nchi ikakosa daktari mzuri kwa sababu ya investment ndogo tu ya miaka michache.

5. achina wana msemo, ukimpa mtu samaki, umemlisha mara moja, ukimfundisha kuvua samaki, umemsaidia kuweza kujilisha maisha yake yote. Msaada wangu huo wa daktari ulikuwa wa kumfundisha kuvua samaki.A skill to earn a living, amarketable one, a useful one. Sio kila mtu anayekuomba hela ya kuweka mafuta ya nywele anafaa kusaidiwa.

6. Saidia watu wanaokuhusu. Waswahili walisema "Mtaka nyingi nasaba, hupata wingi msiba". Tunapenda kuwa na msaada kwa watu wengisana, wengine hata hawatuhusu hivyo. Ukitaka kuisaidia dunia nzima utakufa masikini.

7. weka bajeti ya kusaidia watu. Halafu ukiona imeisha, hata pale unapotaka kusaidia, waambie watu jamani eeh, nilikuwa na bajeti ya kusaidia watu, kwa sasa nimeimaliza mpaka baadaye labda. Kwa anayejua habari zako, hawezi kukulaumu. Huwezi kuwa wewe ndiye unayesaidia watu kila siku bila kuangalia bajeti.

8. Saidia kwa priority. Jiwezeshe wewe mwenyewe na familia yako kuweza mambo makubwa zaidi kwanza, halafu saidia, ama sivyo, utashindwa kabisa kusaidia yeyote na hata wewe mwenyewe utakuwa mzigo kwa wengine.

9. Saidia kwa kutojionesha sana. Kusaidiakwa kujoinesha sanakunaalika waomba misaada ambao wengine hata hawana shida ya kustahili kupata misaada. Wanaona tu hapa kuna hela zinatoka kirahisi, na sisi tutengeneze shoida ya uongo nakweli tu,tupate hela.

10. Saidia bila kufuata mkumbo. Saidia kwa sababu zako, zinazo make sense kwako, sio umeona mtu anatoa sadaka sana kanisani hujui hata mpangowake na mchungaji kama anarudishiwa baada ya misa, anatoa kama chambo kuwanasa wengine wamuige, na wewe unashindana naye kutoa sadaka.

Hayoni machache kutoka kwangu.

Nilishaambiwa katika list zangu nisizidi mambo kumi, kwa maana hata Mungu amri zake zikokumitu (joke)

Zaidi wengine wataongezea.
Dah...mkuu madini yako haya natumaini yatakua msaada kwa wengi

Shukria....
 
Karibu kwenye kamati ya roho mbaya. Friendship is for fool it's family or nothing.
 
Back
Top Bottom