Shy-rose: Sitta ni Mwongo!

Shy-rose: Sitta ni Mwongo!

Jadili hoja za Shy-rose kama ni kweli au sikweli badala ya kumshambulia bila hoja! Binafsi huwa nampenda huyu bint siyo mnafiki kama maccm wenzake,anakupa live ukiingia ktk anga zake,naweza mlinganisha na Hussein Bashe naye huwa hasiti kusema ya moyoni badala ya kukaa kimya kama wachumia tumbo kibao waliojazana CCM na serikalini!

Ni kweli mkuu....
 

JUMAPILI, MACHI 24, 2013 08:52 NA MWANDISHI WETU




“Nimekuwa nikiwasiliana moja kwa moja na
Naibu Waziri Abdullah Juma Sadallah kuhusu masuala mengi, kwa maana ya kushirikiana na kupeana mwongozo, lakini majibu ya Naibu Waziri daima yamekuwa ni ya ubabaishaji na ya kukatisha tamaa, akisema kwamba Wabunge wa EALA hawako chini ya Wizara,” alisisitiza Mbunge huyo.



Watu wengine bwana, yaani Shyrose Kumbe unawasiliana na Naibu waziri anakubabaisha unakaa tu kimya bila kumwona waziri! Kwanini unamng'ang'ania naibu wakati unajua waziri yupo? Kumbe hapa umemwingiza tu waziri kwa jazba zako! Au kwa sababu ni handsome!!!?? Hata huyu mwandishi wa hii habari kabla hajaiweka gazetini alitakiwa amuulize Shyrose kama anababaishwa na naibu waziri ni kwa nini asimuone waziri?
 
haah haa ha haa.. .hii ndo tanzania. siasa zetu kwa sasa zmekuwa kma ulimwengu wa kambale...baba sharubu watoto sharubu.kila mtu anaropoka anachojisikia.hatusemi watu wasiseme.ila tunataka watu wasme kwa kuangalia manufaa ya wananchi na si maslah yao binafs.
 
Watu wengine bwana, yaani Shyrose Kumbe unawasiliana na Naibu waziri anakubabaisha unakaa tu kimya bila kumwona waziri! Kwanini unamng'ang'ania naibu wakati unajua waziri yupo? Kumbe hapa umemwingiza tu waziri kwa jazba zako! Au kwa sababu ni handsome!!!?? Hata huyu mwandishi wa hii habari kabla hajaiweka gazetini alitakiwa amuulize Shyrose kama anababaishwa na naibu waziri ni kwa nini asimuone waziri?

Wapi Handsome... 4ft Naibu wa Waziri ni Handsome? au kwasababu ni Mweupe... yaani mtu mweupe ni Handsome? kweli tumeingiwa na kasumba za kikoloni yoyote yule Mweupe hana hasira za mtu mweusi na ni handsome...

Kama wewe ni rafiki ya Naibu Waziri Mweleze aache kununua Over Size Suites; Afanya Manucare and look Diplomatic
 
Kumekucha...

Cc Ritz
 
Last edited by a moderator:
Uyu Shy kama anaona issue zimezidi kimo si azilete humu JF tumsaidie hakuna rocket science kule.
Niko na jamaa yangu ni mbunge pande za kenya anasema hawa wa kwenu naona wanakujaga lamba posho tuu!
Kwa mtu mstaarabu na mwenye hekima huwezi enda kwa mtu mmoja alafu ukasema wizara nzima inashindwa kukupa ushirikiano
Pale kuna waziri kuna katibu mkuu kuna wakurugenzi sasa wote hao wameshindwa kukupa ushrikiano usikute ulileta zarau wakakupa kubwa.
Apo ndo utagundua tofauti ya mwanamke aliyeolewa na asiyeolewa busara na hekima wako tofauti
 

Wapi Handsome... 4ft Naibu wa Waziri ni Handsome? au kwasababu ni Mweupe... yaani mtu mweupe ni Handsome? kweli tumeingiwa na kasumba za kikoloni yoyote yule Mweupe hana hasira za mtu mweusi na ni handsome...

Kama wewe ni rafiki ya Naibu Waziri Mweleze aache kununua Over Size Suites; Afanya Manucare and look Diplomatic

Kusema kweli hata hilo jina la naibu waziri nimeliona leo kwenye hii habari. Mi mkuu nilikuwa nasema tu kama Shyrose anamuona naibu waziri kuwa handsome. Maana anasema anawasiliana na naibu waziri anambabaisha halafu anaendelea kuwasiliana naye!!!! Ili iweje? Kwa nini hakumuona waziri au katibu mkuu halafu anakuja kulalamikia wizara nzima!!! Mimi sina interest na wizara ila nimeona tu huo upungufu kwamba wizara haiwajali lakini kumbe anawasiliana na naibu waziri. Na pengine ni kwa SMS au kwa simu.
 
Mambo magumu sana hadi kufika mwaka 2015.

IMG_5436.jpg
 

JUMAPILI, MACHI 24, 2013 08:52 NA MWANDISHI WETU


SIKU moja baada ya Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, kupinga malalamiko yaliyotolewa na wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kuwa hawashirikishwi, akisema ni ya ajabu na hayana ukweli, majibu hayo yameonekana kumchefua kiongozi wa wabunge hao.

Akijibu kauli hiyo ya Sitta kupitia taarifa yake aliyoitoa kwenye vyombo vya habari jana, Katibu wa Bunge la Afrika Mashariki, Shy-rose Bhanji, aliitaka Wizara ya Afrika Mashariki kuacha ubabaishaji kwa kutoa kauli za uwongo kwa Watanzania na badala yake akaitaka iongeze kasi ya uwajibikaji.

Juzi Sitta aliitwa mbele ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje iliyotaka kupata ufafanuzi kuhusu malalamiko yaliyotolewa na Katibu wa Bunge la Afrika Mashariki, Shy-rose kuwa Wizara hiyo imekuwa ikiwatenga na haiwashirikishi katika masuala mbalimbali.

Katika majibu yake, Sitta alisema malalamiko hayo hayana ukweli wowote na kumshutumu waziwazi Katibu wa wabunge hao, Shy-rose kuwa ndiye anayeongoza kwa kutohudhuria mikutano anayoalikwa kutokana na kuwa na mambo mengi.

Jana Shy-rose katika majibu yake kwa Sitta, alimtaka Waziri huyo pamoja na Naibu wake kutoa vielelezo dhidi ya madai yao.

“Kama nilivyosema kwenye kikao cha Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara imejitenga sana katika kutoa mwongozo na vile vile katika kuwafikia Watanzania walio wengi kwa kigezo kwamba Wizara haina fedha,” alisema Shy-rose.

“Nimekuwa nikiwasiliana moja kwa moja na Naibu Waziri Abdullah Juma Sadallah kuhusu masuala mengi, kwa maana ya kushirikiana na kupeana mwongozo, lakini majibu ya Naibu Waziri daima yamekuwa ni ya ubabaishaji na ya kukatisha tamaa, akisema kwamba Wabunge wa EALA hawako chini ya Wizara,” alisisitiza Mbunge huyo.

Shy-rose amemtaka Waziri Sitta kukaa na viongozi wa wizara yake ili apate ukweli wa mambo kuliko kurukia kujibu hoja kwa ubabaishaji, kwani nia ni kuweka maslahi ya nchi mbele na si binafsi kama alivyofanya juzi yeye na Naibu wake, kwenye kikao cha Kamati.

Kuhusu suala la posho, Shy-rose alisema walialikwa mara moja tu Bungeni, lakini waliambiwa kila mtu ajigharamie malazi na usafiri.

“Hivi inaingia akilini kweli ualikwe kwenda safari halafu unaambiwa ujigharimie? Yeye Sitta na Naibu Waziri kwa vile wanatumia magari ya Wizara na kuwekewa mafuta na kupewa posho kufika Bungeni ndio maana inamwia rahisi kuongea kiubabaishaji.

“Hii hoja ya posho si ya kweli hata kidogo, kilichoongelewa ni vipi tunafika Dodoma iwapo hatujui tutalala wapi na tutakula nini….sijaomba gharama hizi kama Shy-rose, bali kama Katibu wa Wabunge,” alisema.

Akizungumza na Kamati hiyo, awali kabla ya majibu hayo ya Sitta, Shy-rose alisema wabunge hao wa Afrika Mashariki wamekuwa kama watoto yatima, kwani hawajui waende wapi baada ya Wizara ya Afrika Mashariki kuonyesha kutowajali.

kwanza tuwaulize waheshimiwa wabunge wa Africa ya mashariki waliomba ubunge huo kwa kufanya kazi gani na jee hawakupewa muongozo na kazi zao kabla na baada ya kuchaguliwa.Pili inaonyesha hii wizara ya africa ya mashariki ipo kisiasa zaidi na haina kazi ya kufanya na hawa wabunge wake hawana kazi ya kufanya na ndio maana wanalalamika kua hawashirikishwi.Kwa mtazamo wangu mbunge wa bunge la africa ya mashariki hangepaswa kulalamika eti hashirikishwi na wizara husika wakati wizara inahitaji ajenda kutoka kwa watanzania juu ya ushiriki wa watanzania kwenye mambo mbali mbali ya Africa ya mashariki.Lakini inaonyesha mhe Sita Na Shyrose ni wale watu wanaowatesa Watanzania kutokana na makundi yao ya kisiasa ndani ya chama chao.Mungu awaadhibu kwa madhambi yao.
 
Una mawazo ya hovyo sana..na akili zako timamu unasema wabunge wa east africa ni wawakilishi wa wabunge.?

Kwa hiyo wanawakilisha 'wananchi kupitia Serkali' ya Tanzania au wananchi kupitia Bunge (ambao ndio wapiga kura wao)?
 
Mbona Shy-Rose kakubali alichosema Sitta kwamba anadai posho tuuu??? Sitta alisema hahudhurii vikao akiulizwa anasema hakuna posho. Shy-Rose anasema alihoji fedha za posho ili waweze kwenda dodoma. SItta kasema wizara yake haina fungu la posho kwa Shy na wenzeka??? Mkweli nani?????????????????????????
 
Mh. Sitta ni Muongo na msaliti number moja alianza usaliti kwa ndugu yake CHIEF FUNDIKIRA akahamia kwa KAPUYA akaja akamalizia kwa LOWASSA na sasa anaendeleza uongo wake kwa SHYROSE , huyu mzee ni SNITCH.

You know exactly what is going on, BIG UP
 
Amealikwa mara moja tuu, ajabu kweli mara moja hiyohiyo ameshindwa kuwajibika kwa sababu ya posho,wabunge hawa wa EA ni janga kwa TZ.
 
Mwanamke hana aibu huyu yani Wabunge wa Afrika Mashariki wanalipwa milioni 17 mshahara kwa mwezi na vikao posho yake ni laki 9 kwa siku,leo anataka wabunge wa afrika mashariki kwenda dodoma wapewe posho! Kweli nchi hii hakuna mzalendo,watu wapo kwa ajili ya Posho tu!

Tena itakua ana laana ya watz, wala hawezi kushiba tena.
 
Back
Top Bottom