JUMAPILI, MACHI 24, 2013 08:52 NA MWANDISHI WETU
SIKU moja baada ya Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, kupinga malalamiko yaliyotolewa na wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kuwa hawashirikishwi, akisema ni ya ajabu na hayana ukweli, majibu hayo yameonekana kumchefua kiongozi wa wabunge hao.
Akijibu kauli hiyo ya Sitta kupitia taarifa yake aliyoitoa kwenye vyombo vya habari jana, Katibu wa Bunge la Afrika Mashariki, Shy-rose Bhanji, aliitaka Wizara ya Afrika Mashariki kuacha ubabaishaji kwa kutoa kauli za uwongo kwa Watanzania na badala yake akaitaka iongeze kasi ya uwajibikaji.
Juzi Sitta aliitwa mbele ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje iliyotaka kupata ufafanuzi kuhusu malalamiko yaliyotolewa na Katibu wa Bunge la Afrika Mashariki, Shy-rose kuwa Wizara hiyo imekuwa ikiwatenga na haiwashirikishi katika masuala mbalimbali.
Katika majibu yake, Sitta alisema malalamiko hayo hayana ukweli wowote na kumshutumu waziwazi Katibu wa wabunge hao, Shy-rose kuwa ndiye anayeongoza kwa kutohudhuria mikutano anayoalikwa kutokana na kuwa na mambo mengi.
Jana Shy-rose katika majibu yake kwa Sitta, alimtaka Waziri huyo pamoja na Naibu wake kutoa vielelezo dhidi ya madai yao.
Kama nilivyosema kwenye kikao cha Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara imejitenga sana katika kutoa mwongozo na vile vile katika kuwafikia Watanzania walio wengi kwa kigezo kwamba Wizara haina fedha, alisema Shy-rose.
Nimekuwa nikiwasiliana moja kwa moja na Naibu Waziri Abdullah Juma Sadallah kuhusu masuala mengi, kwa maana ya kushirikiana na kupeana mwongozo, lakini majibu ya Naibu Waziri daima yamekuwa ni ya ubabaishaji na ya kukatisha tamaa, akisema kwamba Wabunge wa EALA hawako chini ya Wizara, alisisitiza Mbunge huyo.
Shy-rose amemtaka Waziri Sitta kukaa na viongozi wa wizara yake ili apate ukweli wa mambo kuliko kurukia kujibu hoja kwa ubabaishaji, kwani nia ni kuweka maslahi ya nchi mbele na si binafsi kama alivyofanya juzi yeye na Naibu wake, kwenye kikao cha Kamati.
Kuhusu suala la posho, Shy-rose alisema walialikwa mara moja tu Bungeni, lakini waliambiwa kila mtu ajigharamie malazi na usafiri.
Hivi inaingia akilini kweli ualikwe kwenda safari halafu unaambiwa ujigharimie? Yeye Sitta na Naibu Waziri kwa vile wanatumia magari ya Wizara na kuwekewa mafuta na kupewa posho kufika Bungeni ndio maana inamwia rahisi kuongea kiubabaishaji.
Hii hoja ya posho si ya kweli hata kidogo, kilichoongelewa ni vipi tunafika Dodoma iwapo hatujui tutalala wapi na tutakula nini .sijaomba gharama hizi kama Shy-rose, bali kama Katibu wa Wabunge, alisema.
Akizungumza na Kamati hiyo, awali kabla ya majibu hayo ya Sitta, Shy-rose alisema wabunge hao wa Afrika Mashariki wamekuwa kama watoto yatima, kwani hawajui waende wapi baada ya Wizara ya Afrika Mashariki kuonyesha kutowajali.
Hawa wakubwa hawawezi kuwasiliana ila kwa kulaumiana magazetini? Makubwa haya! Nadhani hata mimi nikipewa ukubwa kama wa kwao nitafanya vizuri zaidi!
Tatizo huyu dem akili zake zimejiset kutafuta umaarufu tu alikuwa anataka ea time tuu sasa alivyofanya ivyo ndo anatatua tatizo au ? Tena inabd izo posho nao watolewe tu ?Sitta hakujibu magazetin, alijibu ktk kamati ya mambo ya nje na magazeti yalimnukuu huko ktk kikao ila shy ndo kaenda kujibu magazetini.nadhan amepitiliza..
Jadili hoja za Shy-rose kama ni kweli au sikweli badala ya kumshambulia bila hoja! Binafsi huwa nampenda huyu bint siyo mnafiki kama maccm wenzake,anakupa live ukiingia ktk anga zake,naweza mlinganisha na Hussein Bashe naye huwa hasiti kusema ya moyoni badala ya kukaa kimya kama wachumia tumbo kibao waliojazana CCM na serikalini!Tatizo huyu dem akili zake zimejiset kutafuta umaarufu tu alikuwa anataka ea time tuu sasa alivyofanya ivyo ndo anatatua tatizo au ? Tena inabd izo posho nao watolewe tu ?
Wanasiasa kwa kutafuta umaarufu si kitu cha kushangaza. Huyu Shy-Rose sijui anachokitafuta. Wabunge Mara zote ni wawakilishi wa wapiga kura wao siyo wawakilishi wa Serkali. Wabunge wa EALA wapiga kura wao ni Bunge la Jamhuri ya Muungano nilitarajia angelalamika kuwa jhawapati nafasi ya kukutana na Bunge Hilo kwa maelekezo! Ugomvi na manung'uniko yaliyopo ni pale wabunge wetu wanapokuwa na kujifanya wawakilishi na watetezi wa Serkali badala ya wananchi. Hatutarajii kuwa hawa wabunge wa EALA wataenda kuwajulisha mawazo ya Serkali badala ya maslahi yetu ya wananchi amabayo ninatarajia watayapata kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano.
Kwa Mh Sitta sikutarajia naye kujiingiza katika suala hili kwa hoja dhahifu ya posho. Anaweza kuitetea hoja hii vipi ikiwa ni mfumo rasmi ndani ya Serkali yetu posho kuwa mstari wa mbele. Jaribu tu kupeleka mafunzo/semina kwa wabunge Dodoma utagundua jinsi posho ilivyo rasimi!
Kwanza Sita na Rose si bure wako makundi mawili tofauti ya kugombea Urais. Haya yote ni kuonyeshana ubabe kati ya Sita na Lowasa.Rose anakuwa kama mpiga filimbi na mipasho,nafikiri hata mwenyekiti wa Kamati alichaguliwa ili kumuharass na kumvunja nguvu . Pili wanawake hawana mtima wa kumezea , ndio maana UWT, Chaneta,bungeni nk vurugu tupuVIONGOZI wanawake wanaonekana kuwa ni JANGA LA KITAIFA wanapenda sana mipasho badala ya kazi.angalia yule wa bunge la jamhuri, huyu aibu rose, mwingine yule aliye under perform UN, Hawa ghasia n.k ni kero ni kero kwa kwenda mbele.ndio maana baba wa Taifa aliwapa madara wachache sana
Huyu mtoto naye. khaaa!
Huyu mtoto naye. khaaa!
Mboka ezangaka mwasi kitoko te. (Lingala)
Kijiji hakikosi kamwe msichana mrembo. (Swahili)
Il ne manque jamais une belle fille dans un village. (French)
A village never lacks a beautiful young woman. (English)
Huyu mtoto naye. khaaa!
Ninakubaliana 100% na majibu ya hon. Shyrose Bhanji. Hii wizara ni ubabaishaji mtupu hasa kwa vile watendaji wake akiwemo waziri na Katibu wake walitupwa huko baada ya Ku fall out on kikwetes favor. pia ni Kweli kwamba watu hawa wanahpuhusiano aw muda mrefu na kujua na kwa vilemba. Wizara hii imeshindwa Kabisa kufanyakazi imebakia danadana na usanii. Ukiangalia swala la integration Tanzania ya mwisho Kabisa sijui hata wanafanyakazi na nani consultants hawana access hata na shillings Moja watanzania wameachwa nyuma Kabisa Kwenye kutumia fursa za soko hili hata kazi za consultancy hakuna wizara Hiyo wanafanyakazi ni wakenya hii mizimwi imekalia ubinafsi tu. thank you shyrose