Shy-Rose aanza kuwatembelea mabalozi wa EAC Tanzania!!
- Ndio maana tunsema kuwapa nafasi Vijana ili wafanye mambo tofauti na yale tuliyoyazoea, ni muhimu sana kuwajua the players wa sekta utakayoiwakilisha taifa letu, huyu Balozi amewahi kuwa mbunge wa Kenya kwenye EAc, so ana a lot of experience na EAC na pia ndivyo modern politics zinavyotaka, uwajue the players wa yopur area ya uwakilishi.
- I hope na wabunge wengine wa EAc watajifunza, saafi sana Mheshimiwa Shyrose, anakuwa ni mfano wa kuigwa hapa! NA MUNGU AMBARIKIE NA KUMTANGULIA KWENYE SAFARI YAKE HUKO ARUSHA KWENYE EAC!
RESPECT!
William.
William, kama haya ndio maoni yako juu ya matembezi ya Shy-Rose basi nafurahi hukuchaguliwa kuwa EALA mbunge. Kwanza tuanze na Diplomatic protocol, Shy-Rose alienda pale na baraka za Foreign Affairs? Anafanya mazungumzo na balozi wa nchi nyingine kama nani?
Kila nchi mwanachama wa EAC ina interest zake, na kama wewe umefuatilia vizuri Tanzania inawindwa kwa udi na uvumba kutokana na rasilimali zake. Kabla Tanzania haijasema 'Yes', ni vizuri kama Taifa tukajaua/tukaamua ni wapi kunahitaji kuweka mambo sawa, wapi pa kulinda na wapi tufungue milango.
Mfano, huwezi kuwa legelege kwenye issue ya free movement of labour hivi hivi kwa sababu Tanzania tuna tatizo kubwa sana la ukosefu wa ajira. Pia huwezi kuachia ardhi wakati bado hatujaweka mambo sawa kwa watu wetu. Sasa, Shy-Rose ameenda kujifunza nini kwa balozi wa Kenya? Who is the right person to discuss with? Balozi wa Kenya?
Busara ya kawaida ingekuwambia sehemu nzuri ya kuaza kijifunza ilikuwa humu humu ndani, waziri Sitta, wabunge wa Tanzania hasa wenyeviti wa kamati za kudumu za bunge, Mawaziri au/na makatibu wakuu wa wizara ambazo ni strategic i.e Utalii na mali asili, Ardhi,Viwanda na Biashara, Home affairs, etc. Na kwa hakika ningeona anafanya la maana kama angekaa kitako na katibu mkuu wa wizara ya afrika Mashariki (kwa Tanzania).
Pia alitakiwa aende Zanzibar na kuonana na wakuu wa idara/wizara. Kwa kifupi Shy-Rose anatakiwa ajue msimamo wa Tanzania ni upi kwenye mambo yote muhimu. Na mtu wa kumuambia Tanzania inataka nini sio Balozi wa Kenya. Lakini kubwa zaidi nilitegemea Shy-Rose afanye 'tuition' akiwa na wenzake. Napata shida sana kuelewa analenga nini huyu binti kutoka kwa balozi wa Kenya. Balozi anamwakilisha Rais wa nchi, sasa yeye anataka nini toka kwa Kibaki? Na kama kuna kitu anataka toka kwa Kibaki protocol zinasemaje? Unless ameenda pale kama yeye lakini kwa level ya mbunge? sio sahihi.