Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.

Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.

Wanabodi,

Shurti la Mgombea Uongozi wa Umma, Kudhaminiwa na Chama cha Siasa ni Sheria Mbovu, ni...
Kinyume cha Katiba,
Kinyume cha Universal Declaration of Human Rights
Kinyume cha The United Nations Human Rights Committee,
Kinyume cha African Chatter of People and Political Rights
Inaminya Haki na Kulitia Hasara Taifa, Ibadilishwe!.

Declaration of Interest
Mimi ni miongoni mwa Watanzania wazalendo wa nchi yangu, ambaye ni mwanachama wa chama cha siasa, kwa sababu ni lazima uwe mwanachama ndipo ushiriki siasa za vyama za vingi Tanzania
na bado unataka ukagombee ubunge kupitia ccm. au umeahirisha?
Hili shurti la kudhaminiwa na chama cha siasa ni shurti batili, lilikuwa kinyume cha katiba, kisha ubatili huu ukaingizwa kwenye katiba kiubatili!.

Shurti hilo limefanya mtu kuwa kiongozi ni kutegemea hisani ya chama, mfano nilipogombea EALA, nilijitathmini nikajiona naweza, nikaomba, nikashindwa kwa kuzidiwa sifa na wengine, lakini pia hata hao walionizidi sifa, nao walikatwa na kutuletea baadhi ya kokoro na makorokocho!.

Hivyo ili mtu uwe kiongozi, ni lazima upate hisani ya chama!, hii sii haki, hivyo sasa najikita kwenye lobbying na advocacy ya kumlobby Mama, atutendee haki Watanzania, ili 2025 Watanzania tugombee kwa uhuru, na merits na sio kwa hisani ya chama. Hili likifanyika, amini usiamini pale mahali, ule mkono wa bauncer unapigwa chini kama kumsukuma mlevi!.

Mzizi wa fitna ni sheria yetu ya uchaguzi Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law! Kuendelea Kuitumia ni Ujinga? Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!

Lobbying na advocacy kwa Mama, zimeisha anza hivi Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
Na Je, jicho la Rais Samia litauangazia Ubatili huu ndani ya Katiba yetu unaopora Haki ya Msingi, uliochomekewa kibatili ili kuuhalalisha? na Samia Mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa Hili, Atabarikiwa!, Taifa Litabarikiwa!. Asante Mungu kwa Samia, Mungu Mbariki Samia, Mungu Ibariki Tanzania nahttps://www.jamiiforums.com/threads/haki-huinua-taifa-rais-samia-kwa-kauli-na-matendo-ameonesha-ni-mtu-wa-haki-akitekeleza-hili-kama-alivyosema-atabarikiwa-tanzania-itabarikiwa.1998748/ na Samia Mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa Hili, Atabarikiwa!, Taifa Litabarikiwa!. Asante Mungu kwa Samia, Mungu Mbariki Samia, Mungu Ibariki Tanzania na Mgombea Kudhaminiwa na Chama ni Ubatili Uliochomekwa Kiubatili na Bunge Letu Ndani ya Katiba Yetu!. Tuache Ubatili Huu Uendelee Ndani ya Katiba Yetu https://www.jamiiforums.com/threads/je-wajua-kuna-fupa-fulani-la-dhulma-kwa-watanzania-liliwashinda-nyerere-mwinyi-mkapa-kikwete-na-magufuli-jee-mama-samia-ataliweza-fupa-hili.1993393/

Kama ilivyo haki ya kupiga kura ni haki ya kila Mtanzania aliyetimiza (the age of the majority), umri wa miaka 18, vivyo hivyo haki ya kuchaguliwa ni haki ya kila Mtanzania, kugombea na kuchaguliwa.

Haki hii ya kuchaguliwa kwa sasa imekabidhiwa kwa chama cha siasa, hivyo ili Mtanzania aweze kuchaguliwa, anatakiwa kuomba hisani ya chama cha siasa, apitishwe ndipo agombee!, haki haipaswi kuwa hisani!.

Kipengele hiki cha kudhaminiwa na chama cha siasa, ni kipengele batili!, kimetungiwa sheria batili, kisha ubatili huo ukachomekewa kwenye katiba yetu kiubatili!.

Kwa vile Rais Samia, ni mtu wa haki, ubatili huu hakuuchomeka yeye, japo na yeye alikuwepo wakati unachomekwa kwenye katiba yetu, wakati huo, hata kama yeye alikuwa hakubaliani nao, lakini alibanwa na kipengelele cha " a collective responsibility clause", lakini sasa ni yeye ndiye aliyepo na anaweza kuwatendea haki Watanzania.

Tuungane kumuomba Mama atutendee haki Watanzania ili Watanzania wenye karama ya uongozi, na moyo wa kuwatumikia Watanzania, wawe huru kuomba kuwatumikia Watanzania, na sio kutegemea hisani ya chama cha siasa.
Mfano pale Tandale, yule Mtoto wa Tandale, akiomba kuwatumikia wana Tandale, CCM haiwezi kumpitisha kwasababu tuu ametoboa masikio na kuvaa hereni, lakini Wana Tandale, yule ni mtoto wao, hivyo akisimama independently bila kutegemea chama chochote, wana Tandale wanamchagua mtu wao!.

Tunakuomba Mama yetu, fanya ufanyalo ili uchaguzi wa 2025, Watanzania wote wawe na haki ya kuchagua na kuchaguliwa, utabarikiwa sana, Tanzania Itabarikiwa!.

Wasalaam

Paskali.
 
Samia Mtakatifu Mama wa Mungu.
Utuombee sisi wakosefu...
 
Wanabodi,

Shurti la Mgombea Uongozi wa Umma, Kudhaminiwa na Chama cha Siasa ni Sheria Mbovu, ni...
Kinyume cha Katiba,
Kinyume cha Universal Declaration of Human Rights
Kinyume cha The United Nations Human Rights Committee,
Kinyume cha African Chatter of People and Political Rights
Inaminya Haki na Kulitia Hasara Taifa, Ibadilishwe!.

Declaration of Interest
Mimi ni miongoni mwa Watanzania wazalendo wa nchi yangu, ambaye ni mwanachama wa chama cha siasa, kwa sababu ni lazima uwe mwanachama ndipo ushiriki siasa za vyama za vingi Tanzania, zinaendeshwa na Tume ama sio huru, na kama ni huru, sio shirikishi. Siasa zetu hazichezwi katika uwanja ulio sawa, zinachezwa katika uwanja tenge, wa kugombea kisu cha makali kuwili, huku mmoja ameshika mpini!. Hivyo ushindi katika chaguzi zetu, hupatikana kwa mbinu zaidi kuliko kwa kura, ninaziita ni siasa za demokrasia changa, au demokrasia ya Kiafrika, African Democracy. Hivyo kwenye mada hii, haya ni mawazo yangu, kila mtu anao uhuru wa mawazo yake, ambao unapaswa kuheshimiwa hata kama hukubaliani nayo. Kwa wale ambao hawakubaliani na mawazo yangu, rukhsa tutofautiane kwa hoja, kwa kupangua hoja zangu na kuleta hoja mbadala.

Watanzania Tufanye Siasa za Ukweli, Tuachane na Siasa za Uongo, Ulaghai na Siasa za Hovyo Hovyo!.
Tufike mahali sisi Watanzania, wazalendo, wenye nia njema na maendeleo ya kweli ya taifai letu hili masikini, tuwe wakweli kwa kuusema ukweli wa siasa zetu sio siasa za ukweli, ni siasa za hadaa, ulaghai na siasa za hovyo hovyo. Hatuwezi kukaa kimya kwa kuendelea kukumbatia Tume ya Uchaguzi isiyo tume huru kwa kutokuwa shirikishi, huku tukiendesha uchaguzi wetu kwa kutumia sheria mbovu za uchaguzi, na kuendelea kuwawabesha masikini wa Tanzania, mzigo mkubwa wa gharama za uchaguzi wa marudio, unaosababishwa kwa sababu za kujitakia, ambazo mimi nimeziita ni sababu za kijinga, zinazotokana na siasa za hovyo hovyo!.

Kitendo hiki cha wananchi masikini wa kutupwa wa Tanzania, wanaoishi kwenye lindi la umasikini uliotopea wa kipato cha chini ya dola moja kwa siku, halafu kuja kubebeshwa mzigo mkubwa wa gharama za kugharimia chaguzi za marudio zinazotokana na sababu za kisiasa za kijinga na kujitakia ikiwemo wawakilishi halali wa wananchi, waliochaguliwa na wananchi wa eneo husika, kupoteza uwakilishi halali wa wananchi kwa sababu tuu ya kuhama vyama, halafu kuwagharimisha wananchi wote wa taifa hili kugharimia gharama za uchaguzi wa marudio wa kujitakia, sio kuwatendea haki masikini hawa wa nchi hii. Kuwalipisha masikini gharama za uchaguzi wa marudio kwa sababu za kujitakia, ni kuwatendea dhambi masikini hawa!.

Kwa Nini Sheria Yetu ya Uchaguzi ni Sheria Mbovu, Bad Law.
Kifungu 21 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kinatoa haki ya kila Mtanzania mwenye sifa, kuwa huru kushiriki katika siasa na uongozi kuanzia serikali za mtaa hadi serikali kuu, bila ubaguzi wowote.

Sheria hiyo inasema hivi na hapa ninanukuu

Uhuru wa kushiriki shughuli za umma
21.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.

Lakini kukatokea kikundi fulani cha watu, kwa maslahi yao, na kwa vile serikali ni yao, wakaipindua katiba kwa kuinyofoa haki hiyo ya kila mtu kushiriki siasa, iliyotolewa na katiba, na kupachika shurti la kudhaminiwa na chama, hivyo kujenga ubaguzi katika kushiriki shughuli za uongozi umma kwa watu kulazimishwa kwanza kujiunga na vyama vya siasa, ndipo upate haki ya kugombee nafasi yoyote ya uongozi wa umma, huku sio kuwatendea haki Watanzania wengine wote, wasiotaka kujiunga na vyama vyovyote vya siasa, kutokana na kuviona karibu vyama vyote ni vyama vya hovyo hovyo, lakini wana uwezo wa uongozi. Hii ni haki muhimu iliyotolewa na katiba, kitendo cha kuingiza shurti la kudhaminiwa na chama cha siasa ni kinyume cha katiba. Hivyo sheria hii ibadilishwe ili kukidhi kile ambacho katiba ilidhamiria ilipoitoa haki hii, hivyo baada ya mabadiliko hayo ya mlango wa nyuma, kipengele hicho sasa kinasomeka hivi

Uhuru wa kushiriki shughuli za umma Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 Sheria ya 1994 Na.34 ya ib.4
21.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya 67 ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.

Ule uhuru uliotolewa na Katiba wa kila mtu kuwa huru kushiriki shughuli za uongozi, kupitia ibara ya 21, umekuja kunyofolewa na ibara ya 39 na 67 (b)(c) kwa kuweka sherti, ili mtu kuweza kugombea nafasi yoyote ya uongozi wa umma, ni lazima awe ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa hivyo lazima adhaminiwe na chama cha siasa!, Haki zinatolewa na ibara moja halafu zinaporwa na ibara nyingine ya katiba hiyo hiyo!.

Mchungaji Mtikila (Mungu amuweke mahala pema peponi), mwaka 1993, alifungua kesi No. 5 ya 1993, alifanya kuhudi kubwa kukipinga kifungu hiki na Mahakama Kuu kupitia kwa Jaji Lugakingira, (Mungu amuweke mahala pema peponi), ikatamka wazi na bayana kipengele hicho ni batili na kinakiuka katiba ya JMT ya mwaka 1977, hivyo kifutwe, na kutoa haki kwa kila Mtanzania ana haki ya kushiriki kugombea Uongozi

Baada tuu ya Mtikila kushinda kesi serikali ikafanya mambo mawili makubwa ya ajabu!, kwanza ilikata rufaa!. Hivi kwa uamuzi kama huu, serikali ilikata rufaa kwa maslahi ya nani?. Pili serikali ilipeleka bungeni kwa hati ya dharura, sheria No. 34 ya mwaka 1994, kufanya marekebisho ya 8 ya Katiba ya JMT na kukichomeka kipengele hicho ndani ya katiba, hivyo kuibatilisha ile hukumu ya Jaji Lugakingira!. Hapa ndipo ujinga unapoanzia katika siasa zetu kwa serikali kufanya kazi kwa maslahi ya kisiasa ya watu fulani, hivyo kupoteza haki ya wengi kwa ajili ya kuwanufaisha wachache.

Kuhusu haki ya kila Mtanzania kugombea nafasi yoyote, ibara ya 21 ya Katiba ya Tanzania ilisema hivi na hapa nina nukuu
“Kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au wa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria”.

Lakini baada ya kufanywa marekebisho, ibara hiyo ilisomeka hivi, na hapa ninanukuu
“ Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ya 39, ya 47 na ya 67 ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchaguwa na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi”

Hiki kilichofanyika, mimi nakiita ni kitendo cha kihuni!, Watanzania tulifanyiwa uhuni na serikali yetu, kwa kuinajisi katiba yetu!, kitu kimeelezwa ni kinyume cha katiba, kinatoa haki zilizotolewa na katiba, halafu serikali hiyo inakuja kuihalalisha haramu hiyo kwa kuiingiza rasmi kwenye katiba!, huku ni kuinajisi katiba yetu!.

Mchungaji Mtikila, licha ya kuwa ni mwanasiasa, Mwenyekiti wa chama cha siasa cha DP, (Democratic Party), lakini alikuwa ni mtu wa Mungu kiukweli kabisa, kwa sababu hakukubali kabila yetu inajisiwe!, hivyo akafungua kesi nyingine No. 10 ya mwaka 2009 kupinga marekebisho hayo ya 8 ya katiba na kuyaita ni ubatili!.

Katika kesi hiyo, Mchungaji Mtikila aliomba mambo mawili makuu

(a) Mahakama itamke ibara 39 na 67 za katiba zilizorekebishwa na marekebisho ya 8 kwa sharia No. 34 ya mwaka 1994, ni batili na kinyume cha katiba.

(b) Kutamka wazi kuwa Kila Mtanzania ana haki ya kugombea kwa mujibu wa ibara ya 21 ya Katiba, bila kulazimishwa kudhaminiwa na chama cha siasa, hivyo mtu anaweza kugombea kama mgombea binafsi.

Mahakama Kuu chini ya majaji watatu, (majaji watatu kisheria inaitwa Half Bench), Manento, Masati na Mihayo, wakayakubali mambo yote ya Mchungaji Mtikila na kumpa ushindi tena kwa kutamka marekebisho hayo ya katiba ni batili!. Lakini serikali yetu ilivyo ya ajabu, ikakata tena rufaa, na safari hii Mahakama Kuu ikakaa Full Bench ya majaji 7, chini ya Jaji Mkuu Mwenyewe, Agustino Ramadhani, akisaidiwa na Jaji Munuo, Jaji Msoffe, Jaji Kimaro, Jaji Mbarouk, Jaji Luanda, na Jaji Mjasir, ambapo tarehe 17 mwezi June, mwaka 2010 ikatoa hukumu ya ajabu kabisa kuwa kutokea Tanzania!. Tena Mahakama haikuwa peke yake, bali iliwaita mabinga wabobezi wa sheria na katiba kuisaidia, hawa ni wanaitwa marafiki wa mahakama, kwa kiingereza ni friends of the Court, kisheria wanaitwa Amicus Curiae, hivyo ma Amicus Curiae hawa, Mr. Othman Masoud, Prof. Palamagamba Kabudi, na Prof.Jwan Mwaikusa(Mungu Aiweke Roho yake Mahala Pema Peponi)

Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Rufaa uliamua kitu cha ajabu sana na hapa naomba ninanukuu
“So as to let the will of the people prevail as to whether or not such [independent] candidates are suitable. We are definite that the Courts are not the custodian of the will of the people. That is the property of elected Members of Parliament”.

Hii kiukweli ni kauli ya ajabu sana kutolewa na mahakama yetu kwenye jambo zito na muhimu kama hili!. Kitendo cha Mahakama kujivua jukumu la kuwa the custodian of the will of the people!, ni kitendo cha ajabu sana na kushangaza sana!. Hakuna will of the people kubwa kuliko katiba!, kama katiba imetoa haki Fulani, halafu Bunge likatunga sheria ya ajabu kabisa kuifuta haki hiyo, halafu mahakama ikatamka haiwezi kuliingilia Bunge!, where is the doctrine of separation of powers, checks and balance?.

Kwa ajili ya kulinda heshima ya Mahakama Kuu, naomba niweke ilichokisema bila kukitafsiri.

“In our case, we say that the issue of independent candidates has to be settled by Parliament which has the jurisdiction to amend the Constitution and not the Courts which, as we have found, do not have that jurisdiction. The decision on whether or not to introduce independent candidates depends on the social needs of each State based on its historical reality. Thus the issue of independent candidates is political and not legal However, we give a word of advice to both the Attorney General and our Parliament: The United Nations Human Rights Committee, in paragraph 21 of its General Comment No. 25, of July 12, 1996, said as follows on Article 25 of the International Covenant on Civil and Political Rights, very similarly worded as Art 23 of the American Convention and our Art 21: The right of persons to stand for election should not be limited unreasonably by requiring candidates to be members of
parties or of specific parties. Tanzania is known for our good record on human rights and particularly our militancy for the right to self determination and hence our involvement in the liberation struggle. We should seriously ponder that comment from a Committee of the United Nations, that is, the whole world.
DATED at DAR ES SALAAM this 17th day of June, 2010”

Mahakama Kuu ya Rufaa ikaamua kuwa Mahakama haina mamlaka ya kuliingilia Bunge, katika vipengele vya katiba, kumaanisha kwa vile marekebisho hayo ya 8 yamefanywa na Bunge, hivyo ni Bunge ndio lirekebishe kipengele hicho!, kiukweli kabisa, kwa maoni yangu, uamuzi huu sio utii wa mhimili wa Mahakama kwa mhimili Bunge, bali huu ni ukondoo wa hali ya juu kwa Mhimili wa Mahakama kwa serikali kwa manufaa ya watu wachache!.

Uchaguzi wa Mwaka 2015 ukalithibitisha hili, kumbe baadhi ya majaji wetu ni makada!, Jaji Mkuu Mstaafu aliyeongoza jopo hilo, alichukua fomu kugombea urais!, for what my God?!. Baadhi ya wale ma amicus curiae naamini tunawajua na tunawaona na ukada wao!. Unategemea nini kama sheria za nchi hii zitafinyangwa finyangwa kwa manufaa ya wachache?!. This must stop!.

Japo Lengo la Kudhaminiwa na Chama ni Nini, Huu Sii Ujinga Tuu?!.
Katiba ilisema kila Mtanzania ana haki ya kushiriki uongozi, hili sherti la kudhaminiwa na chama lilitoka wapi, na kwa kwa nini watu walazimishwe kuwa wanachama wa vyama ili wadhaminiwe, ndipo waweze kugombea?. Mfano mimi, sina chama kwa sababu naziona siasa za vyama ni za hovyo hovyo, ikitokea nina uwezo wa kuwatumikia wananchi wa eneo langu na kuwaletea maendeleo bila kupitia chama chochote, kwa nini nizuiliwe?!. Kiukweli kabisa, kwa maoni yangu, huu ni ujinga!, it is nonsense!.

Watanzania tusikubali ujinga huu uendelee hadi 2020!, tupiganie milango ya wagombea binafsi ifunguliwe, 2020, watu wenye nia ya kugombea, kuwaletea wananchi maendeleo, bila kupitia hizi nonsense za vyama waingie, washindane kwa hoja na sio kushindana kuhonga, kama hali inavyoendelea sasa!. Hili shurti la vyama likiondolewa, mnaweza kushangaa watu wazalendo wa kweli wan chi hii, kama kina Reginald Mengi, Ali Mfuruki, Yogesh Manek, SS Bakhresa, Pascal Mayalla, and the like, wenye uchungu wa dhati na umasikini wa taifa hili, wakajitokeza kuwatumikia wananchi!.

Kiongozi Akiishachaguliwa, Anakuwa ni Kiongozi wa Watu, na Sio Kiongozi wa Chama, Kwa Sababu Anachaguliwa na Watu na Sio Chama!.
Kiukweli kwenye hili jambo, kuna ujinga mwingi!, ujinga mwingine mkubwa kabisa ni huu, hata kama mgombea amedhaminiwa na chama cha siasa kugombea, akiishapitishwa na Tume ya Uchaguzi kuwa Mgombea, japo anatambulika kama ni mgombea wa chama fulani, lakini akiishachaguliwa, mwenyekiti wa mtaa, diwani, mbunge au rais, anakuwa sio kiongozi tena wa chama kilichomdhamini, bali sasa anakuwa ni kiongozi wa umma, kiongozi wa wananchi. Mfano baada ya rais Magufuli kuchaguliwa kuwa rais kwa tiketi ya CCM, lakini hakuchaguliwa na wana CCM pekee, amechaguliwa na Watanzania wote, yeye anakuwa sio kiongozi wa CCM bali kiongozi wa Watanzania wote, vivyo hivyo kwa wabunge, madiwani na viongozi wa serikali ya mtaa, kitendo cha mtu ambaye ni kiungozi wa umma, kujitoa chama na kupoteza ubunge, udiwani au uongozi wa umma, ni ujinga ambao haupaswi kuvumiliwa. Nini muhimu kati ya umma na chama?. Kuukosesha umma kiongozi wao waliemchagua kwa sababu za chama, sio tuu sio haki kwa wananchi waliomchagua, bali pia ni dhambi, kuwalipisha masikini hawa gharama za uchaguzi wa marudio kwa sababu za kijinga!.

Nini Kifanyike, A Way Forward.
Kama nilivyowahi kushauri humu, ukosoaji wenye kujenga, huandamana na ushauri wa nini kifanyike kurekebisha kasoro hizi ili kuundoa ujinga huu unaoendelea nchini mwetu kwa sasa kwa viongozi wa umma kuhama vyama na kupoteza uongozi wa umma.

1. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amri Jeshi Mkuu, Dr. John Pombe Magufuli, akemee huu mtindo wa kuhama vyama unasababisha hasara kwa taifa, kwa kuwashukuru kumuunga mkono na kuunga mkono juhudi zake, lakini wabaki huko huko kwenye vyama vyao, hadi 2020, wakiishamaliza muhula wao, ndipo wajitoe na kuhama vyama.

2. Rais wa Nchi, akili Ikulu yetu, atenganisha kofia zake mbili za rais wa nchi na Mwenyekiti wa chama cha CCM. Ikulu ni mahali patakatifu, akiwa ikulu, rais wetu afanye kazi takatifu, hili la kuwaita watu ikulu yetu na kuwaomba wajiunge CCM, asilifanyie patakatifu pale, hili akalifanyie ofisi ya CCM Lumumba. Halileti picha nzuri kwa rais wetu, kwa sababu yeye sio rais wa CCM ni rais wa Watanzania wote.

3. Iwekwe faini maalum kwa kila kiongozi wa umma, atakayejiuzulu nafasi yake kwa sababu za kuhama chama, ikiwemo kukatwa mafao yake na ikibidi kufilisiwa ili kugharimia gharama za uchaguzi wa marudio kwa kulitia hasara taifa.

4. Viongozi wote wanaojiuzulu, wasiruhusiwe tena kugombea nafasi walizojiuzulu,kitendo cha kujiuzulu, kasha kugombea tena nafasi hiyo hiyo uliojiuzulu, ni kuwafanya wajinga, wale waliokuchagua.

5. Na kama vyama vimewaruhusu watu hawa waliotufanya wajinga kugombea tena, then natoa wito kwa Watanzania wenzangu, tusikubali kufanywa wajinga!. Tutangulize mbele maslahi ya taifa kwa kuwakataa, kama adhabu ya kutukataa na kulitia taifa letu hasara ya uchaguzi wa marudio.

6. Ila kama mapenzi yako kwa mgombea wa chama chako ni kitu cha muhimu zaidi kwako kuliko kutanguliza mbele maskahi ya taifa, hivyo chochote unacholetewa na chama chako hata kama ni ujinga, wewe utakichagua tuu, hivyo hapo, utakuwa umefanya chaguo lako, hivyo ni kuthibitisha Watanzania bado tunaweza kuletewa ujinga wowote na sisi tukauchagua ujinga huo!, na labda ndio maana mpaka sasa Watanzania tuko hapa tulipo!.

7. Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kwa kufuta chaguzi zote ndogo, na tuanzishe proportional representation kwa mwenye kura nyingi ndiye mshindi, lakini likitokea lolote, akasita kuwa rais, mbunge au diwani, yule aliyemfuatia katika uchaguzi uliopita ndio anatangazwa mbunge, kama hayupo anachuliwa mtu wa tatu, hadi wa mwisho, kama wote hawapo, ndipo uchaguzi mdogo unafanyika.

8. Kile kipengele cha kudhaminiwa na chama kiishie kwenye uteuzi tuu, kiongozi akiishachaguliwa, anakuwa kiongozi wa watu, anaweza kuhama chama bila kupoteza uongozi wake kama ilivyo nchini Kenya na nchi nyingine zenye kuheshimu demokrasia ya kweli na sio hii demokrasia fake ya vyama!.

9. Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kwa kuondoa kipengele cha kudhaminiwa na vyama ili kila Mtanzania mwenye sifa za kugombea uongozi wa nafasi yoyote, aruhusiwe, ila kwenye urais, tuweke vigezo vya ziada, ili asijetokea tajiri mmoja mwenye ukwasi wa kuwanunua watanzania wote, tukajikuta tuna rais wa kununuliwa. Ila kwenye ubunge, udiwani na serikali za mtaa, kila mtu awe free kugombea, hivyo tuwe na wagombea huru, na hili likifanyika hata sisi tusio na vyama tutashiriki, mfano mimi, naweza kabisa kugombea jimbo fulani na kulitwaa kama kuokota embe dodo lililojiangukia, ambapo mbunge wa hapo, nitamsukuma kama nimesukuma mlevi!.

10. Tuibadili Tume yetu ya Uchaguzi iwe Tume Huru zaidi na Shirikishi, tujenge uwanja sawa wa ushindani wa haki kwa vyama vyote, uchaguzi uendeshwe kwa transparency ya hali ya juu kwa kuruhusu mawakala hadi kwenye tallying, na vyama au taasisi zozote ziwe free kuwa na tallying centers zake, kitu ambacho hakitaruhusiwa na talling centers hizo ni kutangaza matokeo, kama matokeo yote ya uchaguzi hadi wa rais yanahesabiwa kituoni na kubandikwa ukutani, kama hakuna jambo lolote la kificho, yaani nothing to hide, kwanini uzuie independent tallying?!. Uchaguzi wa 2020, kila mwenye uwezo wa kufanya tallying aruhusiwe afanye ila sitangaze matokeo, hii itazuia bao la mkono!

Hitimisho.
Tanzania is too poor spend billions on by elections for foolish and nonsense reasons, nikimaanisha nchi yetu Tanzania ni masikini wa kutupwa, kuhalalisha matumizi ya mabilioni haya ya fedha kuendesha chaguzi ndogo kwa sababu za kuhama vyama. Ili Taifa letu lipate maendeleo ya kweli, ni lazima sisi Watanzania tukubali kuwa wakweli toka ndani ya nafsi zetu, kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa na kufanya siasa za ukweli, tusiukubali huu ujinga wa kuhama vyama, uendelee kutugharimisha sisi masikini wa kutupwa, tunaishi kwenye lindi la umasikini uliotopea, halafu kuendelea kugharimishwa.

Nawatakia Ijumaa Njema.

Paskali
pascomayalla@gmail.com
Rejea.
Rev. Mtikila ashida kesi ya kuruhusu mgombea binafsi mahakama ya ...
Mtikila: Shujaa wa Demokrasia, Mwanamapinduzi halisi na Shujaa ...
Mgombea binafsi Tanzania: Tatizo ni nini? | Page 9 | JamiiForums ...

Hukumu ya mgombea binafsi hii hapa (AG vs Mtikila)
P kwenye ubora wako, asante kwa elimu ya bure kabsaa,
 
P kwenye ubora wako, asante kwa elimu ya bure kabsaa,
Mgombea binafsi ana matatizo yafuatayo.
1. Anaweza akafa, nchi haifi na taasisi zake zote hazifi, yaani TRA, BoT, JWTZ, Bunge, UDOM, Tume ya Uchaguzi, Msajili, vyote ni CORPORATES, not individuals. Succession ni lazima iwepo, Magufuli alipokufa akaingia Samia, Uhuru aliposhindwa akaingia arap Ruto. Bila CHAMA cha siasa kuwajibika na succession, nchi itayumba.
2. Anaweza akaiuza nchi. Mwarabu tajiri petrodollars au Mo na billions zake, wabaweza wakanunua Urais, hakuna atakayewajibika akikosea au akichoka au akiamua vibaya. Wasaidizi wake hawana kiunganishi chochote naye, hawathibitiki.
3. Nchi tajiri kama US zinaruhusu kwa masharti maalum.
HILI SI SWALI LA USHABIKI, IT GOES TO THE VERY CORE OF A NATION'S SOVEREIGNTY
 
Hili shurti la kudhaminiwa na chama cha siasa ni shurti batili, lilikuwa kinyume cha katiba, kisha ubatili huu ukaingizwa kwenye katiba kiubatili!.

Shurti hilo limefanya mtu kuwa kiongozi ni kutegemea hisani ya chama, mfano nilipogombea EALA, nilijitathmini nikajiona naweza, nikaomba, nikashindwa kwa kuzidiwa sifa na wengine, lakini pia hata hao walionizidi sifa, nao walikatwa na kutuletea baadhi ya kokoro na makorokocho!.

Hivyo ili mtu uwe kiongozi, ni lazima upate hisani ya chama!, hii sii haki, hivyo sasa najikita kwenye lobbying na advocacy ya kumlobby Mama, atutendee haki Watanzania, ili 2025 Watanzania tugombee kwa uhuru, na merits na sio kwa hisani ya chama. Hili likifanyika, amini usiamini pale mahali, ule mkono wa bauncer unapigwa chini kama kumsukuma mlevi!.

Mzizi wa fitna ni sheria yetu ya uchaguzi Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law! Kuendelea Kuitumia ni Ujinga? Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!

Lobbying na advocacy kwa Mama, zimeisha anza hivi Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
Na Je, jicho la Rais Samia litauangazia Ubatili huu ndani ya Katiba yetu unaopora Haki ya Msingi, uliochomekewa kibatili ili kuuhalalisha? na Samia Mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa Hili, Atabarikiwa!, Taifa Litabarikiwa!. Asante Mungu kwa Samia, Mungu Mbariki Samia, Mungu Ibariki Tanzania nahttps://www.jamiiforums.com/threads/haki-huinua-taifa-rais-samia-kwa-kauli-na-matendo-ameonesha-ni-mtu-wa-haki-akitekeleza-hili-kama-alivyosema-atabarikiwa-tanzania-itabarikiwa.1998748/ na Samia Mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa Hili, Atabarikiwa!, Taifa Litabarikiwa!. Asante Mungu kwa Samia, Mungu Mbariki Samia, Mungu Ibariki Tanzania na Mgombea Kudhaminiwa na Chama ni Ubatili Uliochomekwa Kiubatili na Bunge Letu Ndani ya Katiba Yetu!. Tuache Ubatili Huu Uendelee Ndani ya Katiba Yetu https://www.jamiiforums.com/threads/je-wajua-kuna-fupa-fulani-la-dhulma-kwa-watanzania-liliwashinda-nyerere-mwinyi-mkapa-kikwete-na-magufuli-jee-mama-samia-ataliweza-fupa-hili.1993393/

Kama ilivyo haki ya kupiga kura ni haki ya kila Mtanzania aliyetimiza (the age of the majority), umri wa miaka 18, vivyo hivyo haki ya kuchaguliwa ni haki ya kila Mtanzania, kugombea na kuchaguliwa.

Haki hii ya kuchaguliwa kwa sasa imekabidhiwa kwa chama cha siasa, hivyo ili Mtanzania aweze kuchaguliwa, anatakiwa kuomba hisani ya chama cha siasa, apitishwe ndipo agombee!, haki haipaswi kuwa hisani!.

Kipengele hiki cha kudhaminiwa na chama cha siasa, ni kipengele batili!, kimetungiwa sheria batili, kisha ubatili huo ukachomekewa kwenye katiba yetu kiubatili!.

Kwa vile Rais Samia, ni mtu wa haki, ubatili huu hakuuchomeka yeye, japo na yeye alikuwepo wakati unachomekwa kwenye katiba yetu, wakati huo, hata kama yeye alikuwa hakubaliani nao, lakini alibanwa na kipengelele cha " a collective responsibility clause", lakini sasa ni yeye ndiye aliyepo na anaweza kuwatendea haki Watanzania.

Tuungane kumuomba Mama atutendee haki Watanzania ili Watanzania wenye karama ya uongozi, na moyo wa kuwatumikia Watanzania, wawe huru kuomba kuwatumikia Watanzania, na sio kutegemea hisani ya chama cha siasa.
Mfano pale Tandale, yule Mtoto wa Tandale, akiomba kuwatumikia wana Tandale, CCM haiwezi kumpitisha kwasababu tuu ametoboa masikio na kuvaa hereni, lakini Wana Tandale, yule ni mtoto wao, hivyo akisimama independently bila kutegemea chama chochote, wana Tandale wanamchagua mtu wao!.

Tunakuomba Mama yetu, fanya ufanyalo ili uchaguzi wa 2025, Watanzania wote wawe na haki ya kuchagua na kuchaguliwa, utabarikiwa sana, Tanzania Itabarikiwa!.

Wasalaam

Paskali.
Mkuu ndiyo sababu kuna watu hata umpe pesa haendi kupanga mstari kupiga kura. kudai lazima udhaminiwe na chama cho chote cha siasa. Ili hali tume ya uchaguzi ni idara ya ccm, iliyoundwa na mwenyekiti wa ccm si haki kabisa. Kwa nini tume ya uchaguzi isijumuishe watu kutoka vyama vyote?
 
Wanabodi,

Shurti la Mgombea Uongozi wa Umma, Kudhaminiwa na Chama cha Siasa ni Sheria Mbovu, ni...
Kinyume cha Katiba,
Kinyume cha Universal Declaration of Human Rights
Kinyume cha The United Nations Human Rights Committee,
Kinyume cha African Chatter of People and Political Rights
Inaminya Haki na Kulitia Hasara Taifa, Ibadilishwe!.

8. Kile kipengele cha kudhaminiwa na chama kiishie kwenye uteuzi tuu, kiongozi akiishachaguliwa, anakuwa kiongozi wa watu, anaweza kuhama chama bila kupoteza uongozi wake kama ilivyo nchini Kenya na nchi nyingine zenye kuheshimu demokrasia ya kweli na sio hii demokrasia fake ya vyama!.

9. Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kwa kuondoa kipengele cha kudhaminiwa na vyama ili kila Mtanzania mwenye sifa za kugombea uongozi wa nafasi yoyote, aruhusiwe, ila kwenye urais, tuweke vigezo vya ziada, ili asijetokea tajiri mmoja mwenye ukwasi wa kuwanunua watanzania wote, tukajikuta tuna rais wa kununuliwa. Ila kwenye ubunge, udiwani na serikali za mtaa, kila mtu awe free kugombea, hivyo tuwe na wagombea huru, na hili likifanyika hata sisi tusio na vyama tutashiriki, mfano mimi, naweza kabisa kugombea jimbo fulani na kulitwaa kama kuokota embe dodo lililojiangukia, ambapo mbunge wa hapo, nitamsukuma kama nimesukuma mlevi!.

10. Tuibadili Tume yetu ya Uchaguzi iwe Tume Huru zaidi na Shirikishi, tujenge uwanja sawa wa ushindani wa haki kwa vyama vyote, uchaguzi uendeshwe kwa transparency ya hali ya juu kwa kuruhusu mawakala hadi kwenye tallying, na vyama au taasisi zozote ziwe free kuwa na tallying centers zake, kitu ambacho hakitaruhusiwa na talling centers hizo ni kutangaza matokeo, kama matokeo yote ya uchaguzi hadi wa rais yanahesabiwa kituoni na kubandikwa ukutani, kama hakuna jambo lolote la kificho, yaani nothing to hide, kwanini uzuie independent tallying?!. Uchaguzi wa 2020, kila mwenye uwezo wa kufanya tallying aruhusiwe afanye ila sitangaze matokeo, hii itazuia bao la mkono!

Paskali
Hili ni bandiko zamani, lakini hoja zake bado ni valid, ile siku Rais Samia anaruhusu mikutano ya siasa, alizungumzia kuziangalia baadhi ya sheria zetu kandamizi tuzifanyie mabadiliko, moja ya sheria hizo ni sheria hii ambayo mimi bado nalia nayo!. Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?
Hayo nilioita ni madudu ya ajabu ndio sheria hiyo!.
P
 
Wanabodi,

Shurti la Mgombea Uongozi wa Umma, Kudhaminiwa na Chama cha Siasa ni Sheria Mbovu, ni...
Kinyume cha Katiba,
Kinyume cha Universal Declaration of Human Rights
Kinyume cha The United Nations Human Rights Committee,
Kinyume cha African Chatter of People and Political Rights
Inaminya Haki na Kulitia Hasara Taifa, Ibadilishwe!.
Kwenye siasa kuna visasi vingi, chuki, husuda , usaliti, kiburi, jeuri , dharau, huko kumejaa huwa ni kutesa kwa zamu leo kwangu kesho kwako.
Wabunge hawa wameondolewa kwa chuki visasi na usaliti..Kuna baadhi waliojiharibia na kuna wengine chuki za waziwazi

Kwenye Siasa ni kuwa Macho kama upo choo cha Mlango wa Mbavu za mbwa (mlango wa kuamisha ) muda wowote mkono uwe tayari kuushikilia ili mtu akisukuma wewe ushindilie kwa nguvu.
Mkuu Kozi Kodineta Course Coordinator, bandiko lako hili GE2025 - Majina haya ya Wabunge waliokatwa majina kwa Visasi vya Mwenyekiti limenigusa sana
Haya ni matokeo ya Watanzania kuukubali ujinga wa kuingiza siasa kwenye katiba ya nchi kwa kuchomekewa kifungu batili cha kulazimisha wagombea wadhaminiwe na chama cha siasa.

Ibara ya 5 ya katiba imetoa haki kwa kila Mtanzania kumchagua kiongozi unayempenda, na ibara ya 21 imetoa haki kwa kila Mtanzania kugombea bila shurti la kudhaminiwa na chama cha siasa.

Hao wote waliokatwa na chama chao, kama ni vipenzi wa wananchi wao, walipaswa wasimame kama independent candidates na wangechaguliwa na wananchi wao.

Hiki kipengele cha mgombea kudhaminiwa na chama cha siasa ni dhulma kubwa kwa Watanzania.

Kuna baadhi ya laana nchi yetu inazipata kutokana na dhulma kama hizi!.

Nimekuleta ili uone jinsi tulivyopigia kelele dhulma hii.

Huyu naye alipoanza tulikuwa na matumaini makubwa kuwa atatenda, kumbe ....
Naomba nisimalizie ...!

Ila Mungu Yupo!.

Paskali
 
Back
Top Bottom