Shule zimelemaza wengi

Shule zimelemaza wengi

Unasema elimu sio kitu, halafu unataka ukiumwa uende hospital umkute daktari bingwa aliyebobea.

Unasema elimu sio kitu, halafu ukishapata hizo pesa ukataka kujenga upate mainjinia na architecture.

Unasema elimu sio kitu, halafu ukitaka kufuga unataka upate daktari wa mifugo.

Unasema elimu sio kitu, halafu ukishakuwa na pesa unataka kusafiri upate marubani na mainjinia wa ndege.

Sasa unafikiri hawa madaktari, architectures, pilots, seafarers, engineers wanapatikana vipi bila elimu?
Umemaliza kila kitu in this comment. BIG UP
 
Wewe ni kajitu kajinga sana,sijui ugumu wa maisha ndio umedumaza akili yako!

Unaipima elimu kwa kuwaangalia hao sijui Baba levo,Mwijaku,Niffer! Hivi bila elimu ungeweza kumwaga hayo matapishi yako hapa kwa kutumia simu na Internet ambavyo ni matokeo ya elimu?

Hizo nguo ulizovaa ni matokeo ya elimu,hao unaowataja kufanikiwa,wanamiliki Magari ambayo ni matokeo ya elimu,wanasafiri kwa Ndege ambazo ni matokeo ya elimu,ndege hazitengenezwi na fundi majiko,ukifungua office utahitaji Meza,Viti,Computer,AC...hivyo vifaa vyote ni matokeo ya elimu,ukienda Hosp utahitaji kumuona Daktari bingwa ambaye ana ujuzi kwa matokeo ya elimu aliyo ipata,

Ni mtu mpumbavu pekee asiyejielewa ndio anaweza kuibeza elimu,Dogo tafuta kazi ya kufanya,hizi nyuzi unazomwaga kila dakika haziwezi kukutoa kwenye umasikini,rudi Shule ukapate elimu,labda akili yako itaweza kufanya kazi japo kwa kiwango kidogo tu.
 
You can choose not to pursue an education and still end up struggling in life. Equally, someone can acquire an education and achieve remarkable success through the very same educational system. Therefore, you should never derive satisfaction from the misfortunes of educated people who graduate but struggle to secure employment.
You have made a sweeping generalisation by suggesting that everyone who has pursued higher education has failed to achieve success in life. That is simply not true. There are countless educated individuals earning exceptionally high salaries and enjoying financial stability without experiencing any significant economic difficulties.
Personally, I pursued education with the intention of becoming a teacher, specifically in the Arts disciplines. Surprisingly, I secured employment much earlier than many teachers specialising in Science subjects. I am living a reasonably comfortable life, and I have never looked down upon anyone because of their circumstances. I firmly believe that success in life is influenced by a combination of opportunity, timing, and sheer luck, rather than education alone.
 
Mm nadhan ipo haja kuwaona hawa watu waliohustle na kufanikiwa . Hasa hawa ambao hawana shule.
Kwamba wana IQ kubwa. Japo hawakuweza kwenda Shule rasmi kwa sababu kadha ya kadha.

Turudi kwenye Mada.
Ni kweli elimu yetu imejikita kuzalisha white color Job wengi wakat nafasi na kazi hizo hazitoshi watahiniwa wote.

Huu Mtaala mpya utaleta matokeo miaka 10 ijayo.
Sio Mbaya. Better later than Never.
Msukuma na Kishimba wakianzisha chuo na kufundisha wenyewe italipa sana.
 
Mkuu, hivi unajua hata unacho kiongea?..
Utahakikisha vipi qualifications za mtu alie homeschooling kwamba yupo qualified kwenye career?
Elimu Saizi ni open source... Na mtu sio lazima I aende shuleni..., angalia wengine wana wa homeschool watoto wao..
Utakubali kutibiwa na daktari aliyeji homeschool?
Engineers wapo, na wataendelea kuwepo na mitaala imagine unazidi kugeuka siku hadi siku...
Utakubali engineer au architecture aliye ji homeschool ajenge miradi yako?

Utahakiki vipi qualifications zake kama hakupita shule na chuoni?
What about Elon musk, what a about Steve Jobs wamekuwa wabobezi wa fields zao kwa ku drop vyuoni
Walienda shule na chuo walifika then ndio waka drop.

Hata Mark Zuckerberg chuo ali attend akapata maarifa fulani then ndio aka drop.

Elimu ina umuhimu wake.
 
Umemaliza kila kitu in this comment. BIG UP
Halafu siku zote failures ndio wanapenda kujifariji kwamba elimu sio kitu.

Wanatumia pesa kama silaha ya kuiponda elimu.

Kwamba fulani hajasoma ila ana pesa nyingi.

Basi na wao wanapata faraja kwa kufeli kwao kielimu.

Mtu aliyepata elimu hawezi kusema kwamba elimu sio kitu. Atasema kwamba kuna mapungufu fulani kwenye elimu yanahitaji kurekebishwa.

Vilaza na failures pekee ndio watabaki kusema elimu sio kitu. Kwa sababu walifeli. Sasa wamebaki kujifariji na kufeli kwao.
 
Ndio useme sasa mfano mimi nimeshuhudia kijana awesomemeshwa na serikali chuo kikuu Telecommunications degree kapewa na mkopo 100%, baada ya kumaliza chuo yupo mtaani hana kazi hana ajira.

Mwingine ni the same kasoma hadi Masters masuala ya Diplomasia yupo mtaani hana ajira hana kazi, wewe unafikiri ufumbuzi wa hili ni nini?

Sio unabwabwaja tu na wewe uonekane ulibwabwaja wakati huna ufumbuzi wowote.

Dhumuni la mleta mada ni kuwaamsha akili nyinyi mliolala na mnaojihisi mna ufumbuzi, onyesheni ufumbuzi wenu mlionao unasema marubani kuendesha ndege wapo marubani mtaani kwa mfano yupo dogo mmoja alisomea urubani akasota mtaani mpaka akahama Nchi akaenda Uganda ndio anafanya kazi huko ameajiriwa, sasa ufumbuzi wa haya matatizo ni nini?

Sio kusema tu watu wasiposoma unesi nani atawachoma sindano? Hayo sio majibu ya maswali yanayohitaji ufumbuzi.
Sasa hapo tatizo sio elimu.

Tatizo ni ukosefu wa kazi.

Hao unaosema kwamba walisoma na sasa hawana kazi, wangefanikiwa kupata kazi bado ungesema elimu sio kitu?

Wewe kama hukwenda shule tulia na kama huna elimu tulia.

Aliyesoma kasoma na hawezi kujuta kwa nini alisoma. Hata kama hana kazi kwa sasa, lakini muda wowote ule kazi ikitokea anapata. Kwa sababu qualifications anazo.

Nyie mabumunda ambao shule hamjaenda, hata ikitokea fursa ya kazi. Qualifications hamna wala vyeti vya kielimu hamna.

Mtabaki kuranda randa na kutumia pesa kama silaha ya kuiponda elimu. Kumbe deep down, qualifications hamna. Na mnajuta kwa nini hamkusoma.
 
Siku hizi degree holders wanaranda randa mitaani tu..

Yaani watoto wanamakiza shule na vichwani mwao hata kujenga hoja na kuitetea hawawezi.

Na jinsi teknolojia inavyo kuja kwa kasi sioni kabisa umuhimu wa shule...

Paychek za ajira hazikidhi mahitaji na kuleta financial freedom..

Wenye stadi kazi za maisha na experience ya mtaa ndo wanakula mema ya nchi.

Wengi wenye vyeti wako mitaani kama mazuzu kwasababu hawana ujuzi wa maisha, akili zao zimedumazwa na kukaririshwa mavitu yasiyo kuja kuwa saidia mbeleni.

Imagine walio soma logarithms, Chand ya physics,.. Yoote hayo alafu anakuja mtaani a natakiwa a handle mahusiano, ajue namna ya kujenga familia, anapaswa kuwa na chanzo kingine cha pesa na hawezi kufanya kazi nyingine tofauti na taaluma yake?

Binafsi naona watoto waishie sekondari tu, alaf kama kuna uwezekano asomee ufundi ama field husika baada ya hapo aachane na mavitabu.

Siku hizi elimu si kitu tena... Angalieni mtu kama baba levo, mwijaku, niffer, hanscana, na wengine ambao jitihada zao tu za kuyajua maisha zimewatoa kimaisha....

Hapa siongelei Paychek tena, naongelea mtu kuyafikia mafanikio na financial freedom.

Shule (vyuo) vinadumaza. Kwanza unaingia kwenye debt ya mkopo and all that.. Alaf unasahaulishwa kabisa maisha ya mtaa sio hayo ambayo shule zinawafundisha.
Watanzania wenye elimu ya hadi chuo kikuu ni asilimia ndogo sana. Wengi wameishia darasa la saba, form four na wengine hawakumaliza elimu ya msingi au hawakwenda shule kabisa. Swali ni je kwa watanzania wengi ni maskini? Nchi ni maskini?
 
Mkuu, hivi unajua hata unacho kiongea?..

Elimu Saizi ni open source... Na mtu sio lazima I aende shuleni..., angalia wengine wana wa homeschool watoto wao..

Engineers wapo, na wataendelea kuwepo na mitaala imagine unazidi kugeuka siku hadi siku...

What about Elon musk, what a about Steve Jobs wamekuwa wabobezi wa fields zao kwa ku drop vyuoni
Elon Musk na Steve Jobs wameenda shule. Ku drop university haina maana hajasoma. Kuna Bilgate ni walikuwa na akili nyingi kiasi kwamba elimu/ujuzi ambayo alitegemea aipate chuoni kwa miaka minne yeye ndani ya miaka miwili anakuwa nayo.
 
Elon Musk na Steve Jobs wameenda shule. Ku drop university haina maana hajasoma. Kuna Bilgate ni walikuwa na akili nyingi kiasi kwamba elimu/ujuzi ambayo alitegemea aipate chuoni kwa miaka minne yeye ndani ya miaka miwili anakuwa nayo.
Sasa kwani mimi nimesema shule completely... Nimesema elimu ya chuo
 
Ukizaa mtoto wako hutompeleka shule?

Au kama una watoto hujawapeleka shule?

Halafu kiingereza ndio international language. So lazima watu wajifunze.

Huwezi kwenda USA, UK, Australia. Halafu ukifika kule ukazungumze kiswahili.
😅😅😅Kwani wewe baba na mama yako wamefika huko Uk ,Australi 😅.

Shule anakwenda kwua zoba ,atakuwa ni mti wa maneno mengi kama majinga haya ya siasa ..
 
Halafu siku zote failures ndio wanapenda kujifariji kwamba elimu sio kitu.

Wanatumia pesa kama silaha ya kuiponda elimu.

Kwamba fulani hajasoma ila ana pesa nyingi.

Basi na wao wanapata faraja kwa kufeli kwao kielimu.

Mtu aliyepata elimu hawezi kusema kwamba elimu sio kitu. Atasema kwamba kuna mapungufu fulani kwenye elimu yanahitaji kurekebishwa.

Vilaza na failures pekee ndio watabaki kusema elimu sio kitu. Kwa sababu walifeli. Sasa wamebaki kujifariji na kufeli kwao.
Ndio akina Dotto Magari hao 🤣🤣🤣
 
Kusoma ni kitu kingine na kufanikiwa kimaisha ni kitu kingine,kusoma ni muhimu kila mtu na bahati yake usiingie kwenye mkumbo,upate elimu mkononi hata mtu akikuuliza nikusaidiaje unaanza na utetezi wa elimu yako ndipo fursa zingine zinakuja, sasa hujasoma unasaidiwaje kwenye dunia ya kila mtu ana elimu?

Elimu ni daraja ya kufikia ndoto zako usibeze,Hiyo hiyo Elimu unayoiona umeipatia ya nini wapo watu serikalini wana diploma na angetamani awe na bachelor au Masterz ili mshahara upande,kila mtu ana bahati yake msijikanyage bali mjitambue umuhimu wenu kwenye jamii
 
Wapo wenye bachelor au Masterz anakosa ajira sio kwasababu hana akili no bali amekosa kuyaangalia mazingira yanayomzunguka,sasa unashinda na wavuta bangi kitaa hizo fursa zitakuja saa ngapi, au una smartphone fursa zipo kwenye simu halafu wewe unatumia njia moja tu kuzungusha bahasha njia sahihi huleta majibu sahihi,elimu zitusaidie na sio zituletee ujinga vichwani

Natambua fursa zipo scarcity ila kila mmoja wetu anafanikiwa na namna ametega mitego ya fursa mazingira uliopo marafiki uliona yote hayo ni fursa za kukutoa ulipo, sasa pata elimu ujiachie ukifikiri umasikini utakuepuka kama hujachukua hatua sahihi
 
Back
Top Bottom