Shule za Kata zifutwe, na Ujenzi zaidi usiendelee kwa shule mpya

Kenya Mtaala wao mpya wa elimu umefuta mitihani ya Taifa hata ile NECTA yao inaenda kufutwa. Hii mitala ya Div 1 ni mitala ya mwanzo kabisa ambayo sisi still tunaibadu sana.

Inahitajika mifumo mipya ambayo mtoto anapo soma atoke na vitu vingine vya ziada pale, sio tena aje kuomba pesa ya kwenda kozi hapana.

Tunahitaji kama ni shule za Kilimo ziwe na kila kitu kiasi kwamba mtoto akimaliza pale anyokee shambani.

Hizi za kufundisha watoto wafaulu NECT isha pitwa na wakati kwa sasa. Hili la kuwa na shule zenye miundo mbinu halitawezekana kwa urahisi kwa utitili wa shule za kata
 
Ni mawazo mazuri sana haya, na mkuu ujue zama za kujikita kwenye matokeo zisha isha. Angalia vijana tu wametoka Chuo kikuuu wako mtaa hakuna kazi na hata hukuna ujuzi yaani hawana kazi na hawana ujuzi, kijana kamaliza Chuo kikuu inabidi apige hata kozi ya ufugaji ili aweze kujiajiri kufuga.

Makosa haya yamefanyika kuanzia chini kule.

Ndo maana zinahitajika shule za zenye uwezo wa kuwandaa watoto kujitegemea na au kuendelea na kidato cha Tano.
 
True wafanye maboresho kuna mambo mengi yanakwamisha elimu...
 
Sasa unachokitaka ndicho Rais wa nchi anakitaka, ndicho TET wanakifanyia kazi na last year nilishiriki kwenye interview yao juu uboreshaji.

Kinachotakiwa ni kubadili mfumo wa Elimu ambao umeanza taratibu kwa Sera ya Elimu 2014 ndiyo maana Msingi kunambadiliko tayari lkn mentality ya shule na walimu haijabadilika.

Mwanzo uliisema kata kama shule nao unasema kata kama mfumo wa elimu hivyo mabadiliko yanakuja na tutakuwa na mjadala wa kitaifa Dar na Dom shiriki au peleka maoni yako huko TET but mengi yako incorporated


Malengo ya shule za kata yametimia


Suala LA ujuzi si kata ni Taifa kwa ujumla

Waliopo fedha na kiluvya hawana tofauti kwani wanakutana UD na hana maajabu zaidi ya kingereza na kompyuta
Hajui kulima, kufuga, crafts n.k
 
Uko na hoja ya msingi sana, Kikwete na Lowassa walichangia kushusha hadhi ya elimu kwa kuweka hizi shule, kwa kuziita tu "Shule za Kata" ni sababu tosha ya kushusha na kuweka hadhi yake chini kabisa.

Hawakutakiwa kuanza na "shule za kata" kama walivyojinasibu kisiasa, walitakiwa kwenda k8mkakati kwanza, kuwe na shule mbili au tatu nzuri kila wilaya(angalau), hizi shule ziboreshwe kwa viwango vinavyotakiwa, viwango vya kisasa kabisa kwa sababu ukweli ni kuwa population inaongezeka kila siku, shule zilizokuwepo zisingetosha, ila kuweka shule kila kata ni kuikosea elimu yetu, ona sasa imeshuka viwango vya ajabu kabisa.

Likewise vyuo vikuu, vyuo kama DIT au IFM kwa mfano, havikutakiwa kuwa vyuo vya kutoa madigrii wala, vile vingeendelea kuwa vyuo vya kutoa dip, tech institutes kwa ajili ya watu wa field, degree holders wote tunajua elimu zetu zilivyo, vocational training institutions na Institutions za technology kwa ajili ya watendaji wenye skills huko sites na field...well, kupanga ni kuchagua.
 
heeh unawazimu.
 
shida una elimu ya Tanzania thats why huoni kama ina shida, alichosema na kushauri mtoa mada kikifanyika hili taifa litaanza hata kufanya tafiti za kisayansi, sio kama sasa walimu wenyewe wa kata tia maji tia maji
 
Unamzungumzia Mwl Samuel Mbise?
 
Hizo shule za government zinauliwa na wenye private kwa lengo la kukuza biashara za shule zao,
Kuanzia mitihani na vyote ,,
ili kuaminisha watu ubora wa shule zao,,

Zamani elimu haikuwa biashara, ilikuwa kusoma shule za government ni fahari kubwa sna,,
lakini Leo kusoma government ni fedheha kubwa.

Sababu ya biashara ya elimu.,
Shule za private zifutwe kama ilivyokuwa miaka ya 80 ili kurudisha ubora wa elimu ktk shule za government


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio nancho sisitiza
 
Acha uongo wako wee.
 
Ni kweli hizi shule za kata sisi kinacho tudanganya ni ule ufaulu, ila nyakati za sasa hizi shule hazifai kabisa, angalia mitaani watoto walio maliza kidato cha nne sana sana inabidi waanze kuzunguka mitaani wasajilie watu laini.
khaaaah
 
Ombi langu shule kongwe za serikali zirudishwe kuwepo na O level.
 
Ile Shule inayo Jengwa Zanzibar ambayo Mwinhi kamfuku Mkandarasi, ni ujenzi wa shule inayo chukua wanafunzi 3690, hiki ndio ninacho manisha na sio kuwa na utitir wa shule za jata kila shule ina wanafunzi 800,

Tunaweza tukawa na shule ya wanafunzi 4000, au 3500 au hata 5000 na inawa na miundo mbinu yote
 
Wewe mwenyewe ni mjinga mojawapo maana hata kuandika hujui?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…