Shule za Kata zifutwe, na Ujenzi zaidi usiendelee kwa shule mpya

Kikubwa ni kwamba siasa ilitumika kwenye shule hizo na Ndio kinachoendelea
Siasa ilitumika sana na ninacho shangaaa si wazazi wala Serikali inashituka, Hivi Wanao maliza shule za Secondary wasipo faulu kwenda kidato cha 5 je kuna ujuzi wanakuwa nao? Au lazima waende tena VETA?
 
Mtoa mada hijui elimu bora ungekaa kimya tu.
Ninacho sema, Je shule za Secondary watoto tofauti na kufaulu je kuna cha zaidi wanacho toka nacho? Kwa hizi nyakati huini hatari si ndio?

Watoto wanarudi mtaani inabidi waombe pesa ya kwenda kozi ya Computer unaona sawa?
Watoto wanarudi mtaani hajui hata kulima tuta 1 la mchicha unaona sawa?

Watoto hawana skilla ya aina yoyote zaidi ya yale matokeo yao kwako unaona hio fresh kabisa?
 
Unachoongea kina maana kwa mbali

Kwa sababu izo shule kama unaweza kuzijataja ni kwamba kuna sehemu zilijengwa na kwingine kujengwa shule za kata ila kufanya elimu za sehemu fulani kuwa duni hii ilikuwa ni agenda tangu enzi za nyerere
Angalia mkuu, Watoto wanamaliza Shule za Secondary, hakuna cha ziada walicho toka nacho pale yaani cha zaida, miaka 4 hakuna inabidi mzazi utoe pesa mtoto mara aende Computer kozi, au akasomee, Ushonaji, wakati shule zilipaswa kuwa na vitengo vya Ushonaji, Upishi, Computer, arts na kazalika mtoto anakuja mtaani ana kitu cha ziada kichwani.

Hili haliwezekani kwa utitri wa shule za kata lazima ziunganishwe tupate shule kubwa zenye hio miundo mbinu.

Watoto wakitoka kule wasiwe tu wanajua Mito na mazisa na Milima wawe wana some skills.
 
Chukulia mfano Karatu Sec yes Je unazani Kuna shule ya Kata inaweza fikia ile levo leo hii hata wakisema warudishe kilimo? Jibu ni hapana kwa sababu kwanza ziko nyingi sana.

Na kumbuka kwa wakati huu wa sasa mambo yamebadilika sana, hadi 2030 zaidi ya kazi Million 800 zitakuwa zimechukuliwa na mashine au roboti, most of kazi za Offisi zinaenda kuisha na tusha anza kuona.

Bila kuwa na shule ambzo zilo equiped unazani tutaweza toboa?

Shule zetu zinaandaa watoto wafaulu mtihani waende Chuo kikuu basi hakuna kitu kingine wanaandaliwa
Naamini wewe siyo m Tanzania, huwezi simama juu ya mnara kusema shule za ki Tanzania hazifai.

Kama Karatu ya zamani haiwezi kuwepo, uwezekano wa kuwa na shule nyingine kama Karatu upo pia.

Unasema shule za kata zinazalisha watu vilaza, ujue tu most of intelligent people wamesoma shule za serikali ambapo
 
Siku Moja zitakuja kuwa magofu.. na pia hakukuwa na haja ya kuharibu walimu wazuri wamekimbia ualimu kwa sababu ya maslahi za kisiasa wamejaza walimu hawana uelewa..wajuzi wamehama kwenye mashirika na taasisi zinazolipa vzr, marehem magufuli ni mfano tosha

Nakumbuka mwl aliyeenda ualimu jamaa wa kwanza mimkoa au kiwilaya alipelekwa teaching.... Zamani hiyo


Majuzi nikasikia kuna mwl wa vida faster Sasa hiv ni afisa taaluma wilaya flan ujinga kabisa. Siasa mbaya sana.

Hata wale wataalamu kabisa wamehamia private school. Namjua mmja kwenye fizikia ni mtamu. Lkn alikinbia miaka ya 90 huko. Kwa Sasa private Moja wanamtumia. Na ndio maana madaktari kwenye upande wa PCB ukicheki utaona wanatokea private school
Ni kweli hizi shule za kata sisi kinacho tudanganya ni ule ufaulu, ila nyakati za sasa hizi shule hazifai kabisa, angalia mitaani watoto walio maliza kidato cha nne sana sana inabidi waanze kuzunguka mitaani wasajilie watu laini.
 
Ninacho sema, Je shule za Secondary watoto tofauti na kufaulu je kuna cha zaidi wanacho toka nacho? Kwa hizi nyakati huini hatari si ndio?

Watoto wanarudi mtaani inabidi waombe pesa ya kwenda kozi ya Computer unaona sawa?
Watoto wanarudi mtaani hajui hata kulima tuta 1 la mchicha unaona sawa?

Watoto hawana skilla ya aina yoyote zaidi ya yale matokeo yao kwako unaona hio fresh kabisa?
What are you trying to say, kwani huko private huwa wanarudi na nini cha ziada?
 
Aisee we jamaa huna akili ivi hujui kwmba population ya watu inaongezeka na shule lazima ziwe nyingi.....mm product ya shule za kata advance Pugu nimekutana na watoto wa iliboru na kibaha advance na chuo hawana maajabu yoyote so sio kweli unachokisema.....
Tuna Population kuliko China, kuliko India? So tuwe na shule ambazo watoto wanaende miaka minne wasome warudi mtaani waombe tena pesa za kwenda kozi mbali mbali hata Computer au Upishi? Au kujifunza ufugaji?

Mkuu nyakati zimebadilisja sana haya masomo sijui History, maji maji war, Geograph hayana nafasi kwa dunia ya sasa.

Shule za Serikali za zamani zilikuwa hadi na Magari unazani kwa sasa Serikali inaweza kwa shule za kata?

Ninachi shangaa Watanzania hatushutuki ni hii hali tunadanganywa na matokeo, matokeo katika mfumo upi?
 
Napinga hii hija kwa nguvu zangu zote.
Kwanza ujue shule ni wanafunzi na walimu, madarasa hata kama yakiwa ya nyasi sawa tu. .
Kikubwa wadau waendelee kuboresha elimu na kuandaa walimu wanaokidhi mahitaji. Madarasa sio madrasa tutajenga kwa misaada ya wadau wa elimu. .
Hii ilikuwa zamani wakati wa Ujima, wewe ndo wale mnao angalia DIV ok sawa DIV je katika mfumo upi na mitala ipi? Sina shida na Div One hata shule nzima wapate One nina shida na mfumo mzima na vitu wanavyo toka navyo secondary.

Sikiliza Broo enzi za Div 1 zinaisha, Kenya hapo wamekaaa wakaona ni ujinga wamefuta mitihani ya Taifa, imebaki mitihani ya school level tu.

Sisi bado tuko enzi za stone age za kuabudu DIV na Paper za Taifa, hizi enzi zimeisha mkuu.
 
Hizo shule zote kubwa kubwa nyingi tulikwiba na nyinginezo zilijengwa kama msaada kwa taifa ili. Sijui kwa nini serikali siku hizi wanapojenga miradi yao mingi wanashindwa kuweka na nyumba za watumishi. Nafikiri shirika la nyumba walitazame ili vizuri.

Hujio wa shule za kata si mbaya ni mzuri. Changamoto ni uwekezaji hafifu unaofanya na serikali kuanzia walimu na nyenzo zinginezo. Inapelekea mapokeo yake kutokutoa majibu.

Sema kiasi fulani zilimkomboa kikwete na ajira za waalimu kwa kila mwaka
Mkuu uko sahihi na shida iko pale pale ni nyungi sana, angalua mazingira ya kujifunzua ya shule za Serikaki za msingi, leo hii wakisema zile shule za Msinhi ziwe Equiped aiseee ni Billion of money.

Pili Sisi tunacho angalia shule za kata ni ufaulu hicho ndio kinatupa nguvu.

Braza Kenya wamefuta mitihani ya Taifa unazani ni wajinga sana wa kiwango cha kutisha kufuta mitihani ya Taifa?

Enzi za DIV zinaisha na sijajua kwa nini still sisi tunaabudu bado hizi na kuziona ndo kiwango cha ubora wa elimu
 
What are you trying to say, kwani huko private huwa wanarudi na nini cha ziada?
Nazungumzia Za Serikali ambazo sisi tunalipa Kodi, Unajua Kenya wamefuta Mituhani ya Taifa na mwaka huu ndo walikuwa watoto wa Miwsho kufanya? Unajua sababu?

Au unazani wamekosea sana kufuta mitihani ya taifa na sasa watoto watapimwa kwenye levo za shule zao?

Wamekuja na kitu kunaitwa CBC
 
Katika moja ya makosa yaliofanyika ni uanzishwaji wa Shule za Kata, hizi Shule zimekuja kabisa kuua elimu nchini na mchango wa hizi shule kwenye kuzalisha wajinga ni mkubwa sana.

Kabla ya Shule za Kata tulikuwa na shule kubwa za Serikali, Shule kama Mkwawa, Tabora Boys and Girls, Karatu , Iliboru na kadhalika na kadhalika.

Hizi shule zilikuwa ni kubwa sana na hata majengo yake yalikuwa ni majengo yenye hadhi ya kuitwa shule kweli na kweli zilikuwa zinazalisha watalamu sana. Shule zilikuwa na Madarasa mengi sana, Labalatories Viwanja vya michezo na hata Magari ya Shule.

Shule kama Karatu Sec ilikuwa mchepuo wa Kilimo, Ile Shule ilijengwa kwa standard ya Chuo kabisa, ina kila kitu cha kuitwa Chuo, Nyumba za Walimu ni za Standard sana, pia na shule nyingine kwingineko huko.

Miaka ya 2000 na kuendelea huko ndio ikaja wazo la shule za kata na Walimu wa Clashing Program zikazalishwa shule balaa kila kata na shule yake. Na kwa sababu ya Siasa wanachozingatia pale na Mdarasa basi hata kama hayana sakafu chini ilimuladi ni Madarasa na walimu waingie wafundishe. Unakuta shule ya kata inawanafunzi 600 na kata ya jirani 500 na nyingine 700 na unaweza kuta Wilaya nzima ina wanafunzi 11, 000 kutoka kwenye shule zaidi ya 15 za kata.

Kwa utitili wa shule za kata kuja kuboreshwa kuendana na mazingira ya sasa ni kazi ngumu saba inahitajika fund ya kubwa sana, kwamba shule ziwekewe mifumo, ziwe na viwanja vya mazoezi, ziwe na Maabara za kisasa kabisa za kujifunzia, ziwe na miundombinu ya kila namna sio leo wala kesho.

Shule za zamani za Serikali mfano chukulia Ilboru au hata hiyo Karatu au Ihungo Sec. Shule kama Karatu Sec ingeboreshwa ingeweza ku accomodate wanafunzi 3000+.

Sasa wilaya kama Karatu zikawa na Shule ya ina ile 4 zinatosha kabisa ku accomodate wanafunzi, hizi shule zinakuwa na kila kitu kinachohitajika cha wanafunzi kujifunzia. Shule zikaaa na Computer Lab, Walimu wa Michezo wa aina zote za miche, Vifaa vya mazoezi kwa vitendo na kadhalika.

Au angalieni Majengo ya shule kama Ihungo, yale ndio mazingira ya shule inavyopaswa kuwa, Shule ikiongezewa nguvu inaweza accomodate wanafunzi 4000 ile.

Serikali badala ya kuendelea kuongeza shule za kata ni bora zikaunganishwa, kata 5 shule 1 au 2 na zikawa ni shule kweli za wakati tuliopo, hii ya kuwa na utitili wa shule sio kukuza elimu ni kuzalisha taifa la wajinga na mbumbumbu.

Dunia ya sasa na tunakoelekea tunahitaji shule ziwe na miundombinu na sio vyumba vya madarasa na Vyoo.

Kwa baadae Serikali ianze kuangalia namna ya kuziunganisha hizu shule za kata na kuja na shule moja au mbili standard kabisa. Shule zingine hizo zifungwe na majengo yabadilishwe kuwa Clinic za wakina mama.

Waasisi wa hili wazo la shule za kata waliangalia benefit za kisiasa zaidi kuliko za Maendeleo ya nchi. Ilipaswa nguvu ziwekwe kwenye ujenzi wa shule standard kwa wilaya na zenye kila kitu, hizi pesa zilizotawanywa kwenye shule za kata zingetosha kujenga shule za viwango kwa kila wilaya.

Tunakoelekea kwa sababu ya siasa zitakuja shule za Sekondari kila kijiji.

Tuishauri Serikali kama kweli inataka kukuboresha elimu lazima iangalie miundombinu na kwa shule za kata zilivyo nyingi Serikali haitaweza.

Mfano mzuri ni shule za Msingi za Serikali sawa zinasaidia sana ila wakati sio rafiki.

Picha : Shule ya Sekondari Ihungo baada ya ukarabati: Picha mtandaoni


View attachment 2293125View attachment 2293126
Unaidea nzuri sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
What are you trying to say, kwani huko private huwa wanarudi na nini cha ziada?
sisi ujue kinacho tudanganya nu ule ufaulu na siku tukijua ufaulu hauna maana tena itakuwa too late.

Nikuulize swali, una mtoto kapata Div 1 ya 7 mwambie sasa mtoto wangu umefaulu sana ingia sasa mtaani uifanyie kazi hii DIV 1 ya 7 je unazani ataweza? kwamba hapa ndo mwisho mtoto wangu sasa ingia mtaani practise hii Div 1 kwa vitendo. Hii ndo sababu Kenya wamefuta mitihani ya Taifa.
 
Enzi za mitihani ya Taifa jamani zimeisha, enzi za One ya Point 7 zimeisha.

Hivi mtoto kapata 1 ya 7 anaweza i practise mtaani? Chukua mtoto wako kapata 1 ya 7 au 8 huko mpele mtaani uone na Duv 1 yake uone.

Kenya wamefuta mitihani ya Taifa kwa sababu hii, baada ya kuona hii mitala isha pitwa na wakati kabisa sisi still tunaona ni fasion.It will be too late
 
Hivi uneandika hayo baada ya kufikiri kwa kutumia akili?

Sawa Watoto wote wanaotoka shule za msingi kwa kusoma bure ungewapeleka wapi? JKT yenyewe haina pa kuwapeleka hao wachache

Au wangekuwa migambo?

Shule za Kata zimesaidia sana kutoa haki ya Elimu kwa Watoto wetu.

Hongera kwa E. Lowassa na Benjamin W. Mkapa kwa idea hii
 
Hii ilikuwa zamani wakati wa Ujima, wewe ndo wale mnao angalia DIV ok sawa DIV je katika mfumo upi na mitala ipi? Sina shida na Div One hata shule nzima wapate One nina shida na mfumo mzima na vitu wanavyo toka navyo secondary.

Sikiliza Broo enzi za Div 1 zinaisha, Kenya hapo wamekaaa wakaona ni ujinga wamefuta mitihani ya Taifa, imebaki mitihani ya school level tu.

Sisi bado tuko enzi za stone age za kuabudu DIV na Paper za Taifa, hizi enzi zimeisha mkuu.
Unaweka maneno mdomoni mwangu. Hakuna sehemu nimezungumzia Div 1 or hata kuliandika. Mitaala inatakiwa iendane na mabadiliko ya kitechnologia na pia mahitaji ya soko husika. .
 
Tuelewe hoja yake mengine ni nyama za kujazia


Majengo ya shule hizi kwanza ni ya kizazi 1 kamwe hayawez vuka miaka 30 yakiwa yana uwezo wa kuendelea kutumika.

Ubora wa majengo na miundombinu wezeshi haikuwa lengo LA shule za kata.

Elimu wezeshi iliachwa tangu kwa Sera ya elimu ya 1995 hivyo shida iliyokuwepo tangu nyerere ni wanafunzi kukosa nafasi za kwenda sekondari ( nafasi)

Nafasi si ujuzi
Nafasi si ujuzi
Nafasi si ujuzi


Tulitaka watoto wetu waende sekondari
Tulitaka wafanyakazi wenye elimu ya sekondari na chuo
Utakumbuka mwaka 1997 serikali ilifuta utumishi wa drs LA saba kuajiriwa kwa masharti ya kudumu na ndipo watumishi walipokwebda kusoma sekondari wapate Cheti wakaenda na chuo wapate ujuzi stahiki wa kisekondari mfano walimu, madereva, manesi n.k

Mkapa alipopanua ushiriki wa elimu msingi na sekondari kwa kutoa mafedha kujenga mashule ya msingi na mojamoja kila wilaya ( shule za msingi ziliongezeka maradufu kwenye mpango wa MMEM ambapo ilizaa kiluvya A na kiluvyaA zote zinajitegemea na akawapa ruzuku. MMES huko sekondari akaanza kuboresha wazo likaja mwishoni wa utawala wake kuwa hatuwezi kujenga sekondari kwa mahitaji toshelevu ya wanafunz waliopo msingi hivyo tuwaombe wananchi wajijengee shule zao..
.ndipo rasmi 2005 tukaanza kujenga shule zetu na kikwete akaushikilia tukajenga shule za kata.

Malengo ya shule hizi yamefanikiwa sanasana kututanabaisha kuwa Tz tumeiboresha elimu yetu
Hatukujua hizi shule zinahitaji hiyo miundombinu wakati huo tulitaka
Watumishi
Kiwango cha wasomi paper oriented
Huduma ya elimu ya wote
Maendeleo pia

Vyote juu tumepata
Watumishi wengi ni zao LA kata wanao hoji ni wa kata, waliomstari wa mbele kudai ujuzi ni hao

Kikwete aligundua kumbe seko zinataka maabara akaagiza tukajenga japo hazijakamilika vizur

Kikwete aligundua kama umma unaweza jenga shule pia unaweza jenga Zahanati na tukajenga

Kote huko wanaofanya kazi ni kata products

Ni kweli hizi shule kwa kuwa zimejengwa kipindi kinachokaribiana mwaka 2030 serikali ijiandae kuyajenga tena hivyo maendeleo ya hizo shule tusahau unless irudi tena kwa umma.

Wazo lako ni zuri lkn kuzifuta ni uongo

Kuziunganisha ni uongo

Kuzoboresha kwa kadri ya mahitaji inawezekana tukishirikishwa



Nimeona watu wa makongo juu wanataka kujijengea shule yao yenye ubora unaozingatia ujuzi, hongera kwao labda nasi tuwaige.
 
Hivi uneandika hayo baada ya kufikiri kwa kutumia akili?

Sawa Watoto wote wanaotoka shule za msingi kwa kusoma bure ungewapeleka wapi? JKT yenyewe haina pa kuwapeleka hao wachache

Au wangekuwa migambo?

Shule za Kata zimesaidia sana kutoa haki ya Elimu kwa Watoto wetu.

Hongera kwa E. Lowassa na Benjamin W. Mkapa kwa idea hii
Mkuu umeeleza andiko langu? Kwani ni kuulize ni lazima shule iwe kwenye kata ndo mtoto asome?

Sijasema watoto wasiende shule nimesema Shule za kata ziunganishwe ili ziwe na hadhi kulingana na wakati, hizi nyakati sio za kufundisha watoto wafaulu NECTA pekee,

Sasa ili kuweka miundo mbinu zile shule ziunganishwe.
 
Kuwa na Shule za kata lilikuwa Zuri isipokuwa walioliendeleza wamekosa maono.
Ni sawa ila wakati huu wa sasa tunahitaji Shule ambazo mtoto akitoka pale sio tu atoke na Dic 1 bali na kitu cha ziada. Sasa kwa wingi wa shule za kata ni ngumu sana ila zikiunganishwa inawezekana.
 
Back
Top Bottom