Shule za Kata zifutwe, na Ujenzi zaidi usiendelee kwa shule mpya

Kenya Mtaala wao mpya wa elimu umefuta mitihani ya Taifa hata ile NECTA yao inaenda kufutwa. Hii mitala ya Div 1 ni mitala ya mwanzo kabisa ambayo sisi still tunaibadu sana.

Inahitajika mifumo mipya ambayo mtoto anapo soma atoke na vitu vingine vya ziada pale, sio tena aje kuomba pesa ya kwenda kozi hapana.

Tunahitaji kama ni shule za Kilimo ziwe na kila kitu kiasi kwamba mtoto akimaliza pale anyokee shambani.

Hizi za kufundisha watoto wafaulu NECT isha pitwa na wakati kwa sasa. Hili la kuwa na shule zenye miundo mbinu halitawezekana kwa urahisi kwa utitili wa shule za kata
Screenshot_20220718_084630_com.android.chrome.jpg
 
Tuelewe hoja yake mengine ni nyama za kujazia


Majengo ya shule hizi kwanza ni ya kizazi 1 kamwe hayawez vuka miaka 30 yakiwa yana uwezo wa kuendelea kutumika.

Ubora wa majengo na miundombinu wezeshi haikuwa lengo LA shule za kata.

Elimu wezeshi iliachwa tangu kwa Sera ya elimu ya 1995 hivyo shida iliyokuwepo tangu nyerere ni wanafunzi kukosa nafasi za kwenda sekondari ( nafasi)

Nafasi si ujuzi
Nafasi si ujuzi
Nafasi si ujuzi


Tulitaka watoto wetu waende sekondari
Tulitaka wafanyakazi wenye elimu ya sekondari na chuo
Utakumbuka mwaka 1997 serikali ilifuta utumishi wa drs LA saba kuajiriwa kwa masharti ya kudumu na ndipo watumishi walipokwebda kusoma sekondari wapate Cheti wakaenda na chuo wapate ujuzi stahiki wa kisekondari mfano walimu, madereva, manesi n.k

Mkapa alipopanua ushiriki wa elimu msingi na sekondari kwa kutoa mafedha kujenga mashule ya msingi na mojamoja kila wilaya ( shule za msingi ziliongezeka maradufu kwenye mpango wa MMEM ambapo ilizaa kiluvya A na kiluvyaA zote zinajitegemea na akawapa ruzuku. MMES huko sekondari akaanza kuboresha wazo likaja mwishoni wa utawala wake kuwa hatuwezi kujenga sekondari kwa mahitaji toshelevu ya wanafunz waliopo msingi hivyo tuwaombe wananchi wajijengee shule zao..
.ndipo rasmi 2005 tukaanza kujenga shule zetu na kikwete akaushikilia tukajenga shule za kata.

Malengo ya shule hizi yamefanikiwa sanasana kututanabaisha kuwa Tz tumeiboresha elimu yetu
Hatukujua hizi shule zinahitaji hiyo miundombinu wakati huo tulitaka
Watumishi
Kiwango cha wasomi paper oriented
Huduma ya elimu ya wote
Maendeleo pia

Vyote juu tumepata
Watumishi wengi ni zao LA kata wanao hoji ni wa kata, waliomstari wa mbele kudai ujuzi ni hao

Kikwete aligundua kumbe seko zinataka maabara akaagiza tukajenga japo hazijakamilika vizur

Kikwete aligundua kama umma unaweza jenga shule pia unaweza jenga Zahanati na tukajenga

Kote huko wanaofanya kazi ni kata products

Ni kweli hizi shule kwa kuwa zimejengwa kipindi kinachokaribiana mwaka 2030 serikali ijiandae kuyajenga tena hivyo maendeleo ya hizo shule tusahau unless irudi tena kwa umma.

Wazo lako ni zuri lkn kuzifuta ni uongo

Kuziunganisha ni uongo

Kuzoboresha kwa kadri ya mahitaji inawezekana tukishirikishwa



Nimeona watu wa makongo juu wanataka kujijengea shule yao yenye ubora unaozingatia ujuzi, hongera kwao labda nasi tuwaige.
Ni mawazo mazuri sana haya, na mkuu ujue zama za kujikita kwenye matokeo zisha isha. Angalia vijana tu wametoka Chuo kikuuu wako mtaa hakuna kazi na hata hukuna ujuzi yaani hawana kazi na hawana ujuzi, kijana kamaliza Chuo kikuu inabidi apige hata kozi ya ufugaji ili aweze kujiajiri kufuga.

Makosa haya yamefanyika kuanzia chini kule.

Ndo maana zinahitajika shule za zenye uwezo wa kuwandaa watoto kujitegemea na au kuendelea na kidato cha Tano.
 
Napinga hii hija kwa nguvu zangu zote.
Kwanza ujue shule ni wanafunzi na walimu, madarasa hata kama yakiwa ya nyasi sawa tu. .
Kikubwa wadau waendelee kuboresha elimu na kuandaa walimu wanaokidhi mahitaji. Madarasa sio madrasa tutajenga kwa misaada ya wadau wa elimu. .
True wafanye maboresho kuna mambo mengi yanakwamisha elimu...
 
Ni mawazo mazuri sana haya, na mkuu ujue zama za kujikita kwenye matokeo zisha isha. Angalia vijana tu wametoka Chuo kikuuu wako mtaa hakuna kazi na hata hukuna ujuzi yaani hawana kazi na hawana ujuzi, kijana kamaliza Chuo kikuu inabidi apige hata kozi ya ufugaji ili aweze kujiajiri kufuga.

Makosa haya yamefanyika kuanzia chini kule.

Ndo maana zinahitajika shule za zenye uwezo wa kuwandaa watoto kujitegemea na au kuendelea na kidato cha Tano.
Sasa unachokitaka ndicho Rais wa nchi anakitaka, ndicho TET wanakifanyia kazi na last year nilishiriki kwenye interview yao juu uboreshaji.

Kinachotakiwa ni kubadili mfumo wa Elimu ambao umeanza taratibu kwa Sera ya Elimu 2014 ndiyo maana Msingi kunambadiliko tayari lkn mentality ya shule na walimu haijabadilika.

Mwanzo uliisema kata kama shule nao unasema kata kama mfumo wa elimu hivyo mabadiliko yanakuja na tutakuwa na mjadala wa kitaifa Dar na Dom shiriki au peleka maoni yako huko TET but mengi yako incorporated


Malengo ya shule za kata yametimia


Suala LA ujuzi si kata ni Taifa kwa ujumla

Waliopo fedha na kiluvya hawana tofauti kwani wanakutana UD na hana maajabu zaidi ya kingereza na kompyuta
Hajui kulima, kufuga, crafts n.k
 
Uko na hoja ya msingi sana, Kikwete na Lowassa walichangia kushusha hadhi ya elimu kwa kuweka hizi shule, kwa kuziita tu "Shule za Kata" ni sababu tosha ya kushusha na kuweka hadhi yake chini kabisa.

Hawakutakiwa kuanza na "shule za kata" kama walivyojinasibu kisiasa, walitakiwa kwenda k8mkakati kwanza, kuwe na shule mbili au tatu nzuri kila wilaya(angalau), hizi shule ziboreshwe kwa viwango vinavyotakiwa, viwango vya kisasa kabisa kwa sababu ukweli ni kuwa population inaongezeka kila siku, shule zilizokuwepo zisingetosha, ila kuweka shule kila kata ni kuikosea elimu yetu, ona sasa imeshuka viwango vya ajabu kabisa.

Likewise vyuo vikuu, vyuo kama DIT au IFM kwa mfano, havikutakiwa kuwa vyuo vya kutoa madigrii wala, vile vingeendelea kuwa vyuo vya kutoa dip, tech institutes kwa ajili ya watu wa field, degree holders wote tunajua elimu zetu zilivyo, vocational training institutions na Institutions za technology kwa ajili ya watendaji wenye skills huko sites na field...well, kupanga ni kuchagua.
 
Napinga hii hija kwa nguvu zangu zote.
Kwanza ujue shule ni wanafunzi na walimu, madarasa hata kama yakiwa ya nyasi sawa tu. .
Kikubwa wadau waendelee kuboresha elimu na kuandaa walimu wanaokidhi mahitaji. Madarasa sio madrasa tutajenga kwa misaada ya wadau wa elimu. .
heeh unawazimu.
 
Aisee we jamaa huna akili ivi hujui kwmba population ya watu inaongezeka na shule lazima ziwe nyingi.....mm product ya shule za kata advance Pugu nimekutana na watoto wa iliboru na kibaha advance na chuo hawana maajabu yoyote so sio kweli unachokisema.....
shida una elimu ya Tanzania thats why huoni kama ina shida, alichosema na kushauri mtoa mada kikifanyika hili taifa litaanza hata kufanya tafiti za kisayansi, sio kama sasa walimu wenyewe wa kata tia maji tia maji
 
Wazo la kufuta shule za kata siyo zuri.

Nilisoma Karatu Sec School miaka ile shule inaanza, ilikuwa shule ya kilimo. Namkumbuka Mwalimu Mbise (ambaye alikuja kupata ajali, ni kama alilazwa KCMC kwa miaka mingi sana till he died, Rest well Mwalimu Mbise)

Huyu bwana alikuwa mwalimu wa kilimo, eneo lile lilikuwa kubwa, tulilima ngano sana kulikuwa na kila aina ya trekta ya kulimia, kupanda, kupalilia, hadi kuvuna, Mbise alimudu hii kazi.

Sikujua ni nini kilichokuja kuharibu huu mfumo ila kwa ushauri tu ni vizuri urudishwe.

Shule za kata, ni shule nzuri sema mtoto awe smart na ajue alichofuata shuleni.

Nina mfano mzuri wa binti yangu, alisoma mshikamano primary, then kiluvya secondary alipokutana na mwalimu aliyemtanfika fimbo zaidi ya 20 baada ya kuwakuta wamechelewa shule wakajificha mtaroni.

Kiluvya alipata division three, akapangiwa Mungai mafinga huko high school, hizi zote ni za kata.

JJ Mungai alipata division one ya point saba,

Then to jkt mlale,

Sijui ubaya wa shule za kata, cha kusema ni serikali iweke waalimu wazuri pia mazingira yaboreshwe.

All in all, this is challenge and I should vote to you.

Hongera mwaya.
Unamzungumzia Mwl Samuel Mbise?
 
Swala sio shule za Privatw swala ni kwamba kuna shift ya Dunia kwa sasa na kwa mtindo wa mifumo ya elimu tutalia sana. Usha fika International School hata kutembelea tu? Zile shule kwanza vuwanja vyao vya Mpira huo Pitch ni balaa tupu, njoo kwenye walimu wa Michezo ni wale walio qualify na kazi yao ni hio tu, wana kila aina ya vifaa vya kujifunzia, Sasa Serikali kwa wungi wa shule haitaweza kamwe ni lazima ziunganiswe.

Lazima tuwe na shule ambazo zina muandaa mtoto kwa mambo mengi na sio swala la kufaulu tu.

Kenya unazani ni wajinga kufuta mitihani ya Taifa?
Hizo shule za government zinauliwa na wenye private kwa lengo la kukuza biashara za shule zao,
Kuanzia mitihani na vyote ,,
ili kuaminisha watu ubora wa shule zao,,

Zamani elimu haikuwa biashara, ilikuwa kusoma shule za government ni fahari kubwa sna,,
lakini Leo kusoma government ni fedheha kubwa.

Sababu ya biashara ya elimu.,
Shule za private zifutwe kama ilivyokuwa miaka ya 80 ili kurudisha ubora wa elimu ktk shule za government


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo shule za government zinauliwa na wenye private kwa lengo la kukuza biashara za shule zao,
Kuanzia mitihani na vyote ,,
ili kuaminisha watu ubora wa shule zao,,

Zamani elimu haikuwa biashara, ilikuwa kusoma shule za government ni fahari kubwa sna,,
lakini Leo kusoma government ni fedheha kubwa.

Sababu ya biashara ya elimu.,
Shule za private zifutwe kama ilivyokuwa miaka ya 80 ili kurudisha ubora wa elimu ktk shule za government


Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio nancho sisitiza
Screenshot_20220718_132209_com.android.chrome.jpg
 
Aisee we jamaa huna akili ivi hujui kwmba population ya watu inaongezeka na shule lazima ziwe nyingi.....mm product ya shule za kata advance Pugu nimekutana na watoto wa iliboru na kibaha advance na chuo hawana maajabu yoyote so sio kweli unachokisema.....
Acha uongo wako wee.
 
Ni kweli hizi shule za kata sisi kinacho tudanganya ni ule ufaulu, ila nyakati za sasa hizi shule hazifai kabisa, angalia mitaani watoto walio maliza kidato cha nne sana sana inabidi waanze kuzunguka mitaani wasajilie watu laini.
khaaaah
 
Ile Shule inayo Jengwa Zanzibar ambayo Mwinhi kamfuku Mkandarasi, ni ujenzi wa shule inayo chukua wanafunzi 3690, hiki ndio ninacho manisha na sio kuwa na utitir wa shule za jata kila shule ina wanafunzi 800,

Tunaweza tukawa na shule ya wanafunzi 4000, au 3500 au hata 5000 na inawa na miundo mbinu yote
Screenshot_20220718_214058.jpg
 
Katika moja ya makosa yaliofanyika ni uanzishwaji wa Shule za Kata, hizi Shule zimekuja kabisa kuua elimu nchini na mchango wa hizi shule kwenye kuzalisha wajinga ni mkubwa sana.

Kabla ya Shule za Kata tulikuwa na shule kubwa za Serikali, Shule kama Mkwawa, Tabora Boys and Girls, Karatu , Iliboru na kadhalika na kadhalika.

Hizi shule zilikuwa ni kubwa sana na hata majengo yake yalikuwa ni majengo yenye hadhi ya kuitwa shule kweli na kweli zilikuwa zinazalisha watalamu sana. Shule zilikuwa na Madarasa mengi sana, Labalatories Viwanja vya michezo na hata Magari ya Shule.

Shule kama Karatu Sec ilikuwa mchepuo wa Kilimo, Ile Shule ilijengwa kwa standard ya Chuo kabisa, ina kila kitu cha kuitwa Chuo, Nyumba za Walimu ni za Standard sana, pia na shule nyingine kwingineko huko.

Miaka ya 2000 na kuendelea huko ndio ikaja wazo la shule za kata na Walimu wa Clashing Program zikazalishwa shule balaa kila kata na shule yake. Na kwa sababu ya Siasa wanachozingatia pale na Mdarasa basi hata kama hayana sakafu chini ilimuladi ni Madarasa na walimu waingie wafundishe. Unakuta shule ya kata inawanafunzi 600 na kata ya jirani 500 na nyingine 700 na unaweza kuta Wilaya nzima ina wanafunzi 11, 000 kutoka kwenye shule zaidi ya 15 za kata.

Kwa utitili wa shule za kata kuja kuboreshwa kuendana na mazingira ya sasa ni kazi ngumu saba inahitajika fund ya kubwa sana, kwamba shule ziwekewe mifumo, ziwe na viwanja vya mazoezi, ziwe na Maabara za kisasa kabisa za kujifunzia, ziwe na miundombinu ya kila namna sio leo wala kesho.

Shule za zamani za Serikali mfano chukulia Ilboru au hata hiyo Karatu au Ihungo Sec. Shule kama Karatu Sec ingeboreshwa ingeweza ku accomodate wanafunzi 3000+.

Sasa wilaya kama Karatu zikawa na Shule ya ina ile 4 zinatosha kabisa ku accomodate wanafunzi, hizi shule zinakuwa na kila kitu kinachohitajika cha wanafunzi kujifunzia. Shule zikaaa na Computer Lab, Walimu wa Michezo wa aina zote za miche, Vifaa vya mazoezi kwa vitendo na kadhalika.

Au angalieni Majengo ya shule kama Ihungo, yale ndio mazingira ya shule inavyopaswa kuwa, Shule ikiongezewa nguvu inaweza accomodate wanafunzi 4000 ile.

Serikali badala ya kuendelea kuongeza shule za kata ni bora zikaunganishwa, kata 5 shule 1 au 2 na zikawa ni shule kweli za wakati tuliopo, hii ya kuwa na utitili wa shule sio kukuza elimu ni kuzalisha taifa la wajinga na mbumbumbu.

Dunia ya sasa na tunakoelekea tunahitaji shule ziwe na miundombinu na sio vyumba vya madarasa na Vyoo.

Kwa baadae Serikali ianze kuangalia namna ya kuziunganisha hizu shule za kata na kuja na shule moja au mbili standard kabisa. Shule zingine hizo zifungwe na majengo yabadilishwe kuwa Clinic za wakina mama.

Waasisi wa hili wazo la shule za kata waliangalia benefit za kisiasa zaidi kuliko za Maendeleo ya nchi. Ilipaswa nguvu ziwekwe kwenye ujenzi wa shule standard kwa wilaya na zenye kila kitu, hizi pesa zilizotawanywa kwenye shule za kata zingetosha kujenga shule za viwango kwa kila wilaya.

Tunakoelekea kwa sababu ya siasa zitakuja shule za Sekondari kila kijiji.

Tuishauri Serikali kama kweli inataka kukuboresha elimu lazima iangalie miundombinu na kwa shule za kata zilivyo nyingi Serikali haitaweza.

Mfano mzuri ni shule za Msingi za Serikali sawa zinasaidia sana ila wakati sio rafiki.

Picha : Shule ya Sekondari Ihungo baada ya ukarabati: Picha mtandaoni


View attachment 2293125View attachment 2293126
Wewe mwenyewe ni mjinga mojawapo maana hata kuandika hujui?
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom