Shule ya Sekondari Swila inaminya uhuru wa kuabudu

domokaya

JF-Expert Member
Apr 22, 2010
3,546
1,725
Swila Sekondari iliyopo Mbalizi jijini Mbeya haijasajiliwa kama shule ya kidini kwa maana ya religious school, imesajiliwa kama secular school lakini wanafunzi wote wanaosoma shule hiyo wanalazimishwa kuabudu katika madhehebu ya Moravian.

Mwanafunzi yeyote asiyeshiriki katika ibada za Moravian awe Msabato, M -Roman Catholic, M-lutheri, Muislamu anafukuzwa shule.

Hebu wadau nisaidieni hili linafanyikaje katika Tanzania yetu ambapo kila mtu ana haki ya kuabudu.

Katika shule inayofundishwa na walimu waliosomeshwa na walipa kodi wote wa nchi hii tena katika shule ya mtu binafsi?
 
Swila Sekondari iliyopo Mbalizi jijini Mbeya haijasajiliwa kama shule ya kidini kwa maana ya religious school, imesajiliwa kama secular school lakini wanafunzi wooote wanaosoma shule hiyo wanalazimishwa kuabudu katika madhehebu ya Moravian. Mwanafunzi yeyote asiyeshiriki katika ibada za Moravian awe msabato, M -Roman Catholic, M-lutheri, Muislamu anafukuzwa shule. Hebu wadau nisaidieni hili linafanyikaje katika Tanzania yetu ambapo kila mtu ana haki ya kuabudu. Kaika shule inayofundishwa na walimu waliosomeshwa na walipa kodi wote wa nchi hii tena katika shule ya mtu binafsi?
ziko nyingi. watu wamekaa kimya tu. mm watoto wangu wamesoma shule(jiankapuni) walikuwa wanasali na kufanya taratibu zote za dini nyingine mpaka wakamaliza, waliporudi wakaendelea kama zamani..
 
Ndugu hizi shule za binafsi zina taratibu na miiko yako, huo ni utaratibu tu. Hata hivyo sidhani kama ni lazima mtu kumsomesha mwanao ktk shule hizo. Zipo shule nyingi za binafsi zinazotoa nafasi kwa mwanafunzi wa dhehebu lolote kushiriki masuala ya dini yake anapokuwa shuleni, mpeleke huko.

Lakni pia, Mungu anayeabudiwa ni mmoja, kama anapata elimu bora mwache kijana asome, anapokuwa nyumbani umlee katika maadili ya dini yako/yake. Kwani huko moravian wanamwabudu nani? katika kupata elimu bora nchini mwetu kwasasa, bado tunahitaji kuwatumia watu waliojitolea kutoa elimu hiyo stahiki, na siku zote "MTAKA CHA UVUNGUNI SHARTI AINAME".
 
Habari gani kama ungesikia wanalazimishwa kuvuta bangi ungefurahi? Anayeelekeza mtoto kumwabudu Mungu ni mtu mwenye mapenzi mema na mwanao
 
Hapo dawa ni kuvumilia tu na kama huwezi ni kuhamia tu shule yenye mlengo wa dini unayoipenda (na zipo nyingi) Hakuna namna. Zaidi ya hapo utakua unatafuta chokochoko tu.

Tuchukulie mfano una binti yako mkristo/mpagani, unampeleka shule inayofuata imani ya dini ya kiislam anaambiwa avae hijjab, wewe unaanza kulalamika!! Afuate tu taratibu za hiyo shule.
 
Sioni sababu yakulalamika maana ile nishule binafsi yenye taratibu zake, kama huridhiki si umuhamishe mtoto maana hakuna aliyelazimishwa kupeleka mtoto pale
Nchi haiendeshwi na sheria binafsi.Kuna sheria iliyopo inayofanya shule hiyo kuwepo na kusajiliwa, kuna masharti ya usajili ndio maana mtu huwezi kujiamulia mambo tu hata yanayohusumwili wako kama yanaenda kinyume cha sheria, ndiomaana hata wale wanaume wanaopenda kuolewa wanashindwa kufanya hivyo katika nchi ambazo sheria haziruhusu japo miili ni yao
 
Hama walikulizimisha mtoto mpeleke pale si KIHELEHELE chako
Katiba inanipa freedom of association na pia inakataza ubaguzi wa aina yeyote kama hili suala lipo juu ya uwezo wako wa ufikiri na kuona mbali na kujua kwa namna hii taifa linapelekwa wapi pole sana, ufinyu wa upeo nao ni ugonjwa pia
 
Hapo dawa ni kuvumilia tu na kama huwezi ni kuhamia tu shule yenye mlengo wa dini unayoipenda (na zipo nyingi) Hakuna namna. Zaidi ya hapo utakua unatafuta chokochoko tu.

Tuchukulie mfano una binti yako mkristo/mpagani, unampeleka shule inayofuata imani ya dini ya kiislam anaambiwa avae hijjab, wewe unaanza kulalamika!! Afuate tu taratibu za hiyo shule.
Uzuri shule zilizosajiliwa kama shule za kidini zinafahamika, tatizo linakuja shule imesajiliwa kama secular school mwenye shule mwenyewe ndio anaamua pasi kufuata sheria, wasiwasi wangu tukitoka kwenye shule utakuja kwenye maduka, kwenye hoteli na kwingineko, mtu wa dini fulani hupati huduma lazima useme salamu ya dini fulani au kufanya ishara ya dini fulani, mwanzo wa moto ni cheche
 
Habari gani kama ungesikia wanalazimishwa kuvuta bangi ungefurahi? Anayeelekeza mtoto kumwabudu Mungu ni mtu mwenye mapenzi mema na mwanao

Mkuu kuna Miungu wengine wanataka waumini wa jinsia tofauti wasali uchi tena gizani ndugu yangu nao wanasema wanamuabudu Mungu
 
Daaa umenikumbusha mbali mkuu,nimesoma kidato cha 1-3 hapo mwak a 2000,kimsingi sioni tatizo,maana kwa wakat huo utoaj wao elimu ulikuwa wa kiwango kizuri ukizngatia unapata mafundisho ya kumjua Mungu,na hili lilifanyika ktk kiwango cha juu sawasawa na elimu wanayotoa!!mi ni mkatolik lakin sikuona tatizo as long Mungu tunayemwabudu ni mmoja!our school motto was "LIFE-JESUS=0"
 
Sasa umeleta mada kama taarifa au unataka ushauli? maana kila aliyekushauli umemvamia, kama unajua cha kufanya si uchukue uamuzi kimya kimya?
 
Swila Sekondari iliyopo Mbalizi jijini Mbeya haijasajiliwa kama shule ya kidini kwa maana ya religious school, imesajiliwa kama secular school lakini wanafunzi wote wanaosoma shule hiyo wanalazimishwa kuabudu katika madhehebu ya Moravian.

Mwanafunzi yeyote asiyeshiriki katika ibada za Moravian awe Msabato, M -Roman Catholic, M-lutheri, Muislamu anafukuzwa shule.

Hebu wadau nisaidieni hili linafanyikaje katika Tanzania yetu ambapo kila mtu ana haki ya kuabudu.

Katika shule inayofundishwa na walimu waliosomeshwa na walipa kodi wote wa nchi hii tena katika shule ya mtu binafsi?
Mkuu yaani wataka shule yenye taratibu zake ibadirike kwa sababu yako wewe na si wewe ubadirike kutokana na mazingira? Mbona nasikia hadi fomu zao wameandika kwamba shule inafuata malezi ya kikristo?
 
Swila Sekondari iliyopo Mbalizi jijini Mbeya haijasajiliwa kama shule ya kidini kwa maana ya religious school, imesajiliwa kama secular school lakini wanafunzi wote wanaosoma shule hiyo wanalazimishwa kuabudu katika madhehebu ya Moravian.

Mwanafunzi yeyote asiyeshiriki katika ibada za Moravian awe Msabato, M -Roman Catholic, M-lutheri, Muislamu anafukuzwa shule.

Hebu wadau nisaidieni hili linafanyikaje katika Tanzania yetu ambapo kila mtu ana haki ya kuabudu.

Katika shule inayofundishwa na walimu waliosomeshwa na walipa kodi wote wa nchi hii tena katika shule ya mtu binafsi?
Sasa si umeshasema shule ya kidini!! Saa what's the point !!? Maana yake inafuata mlengo wa kidini fullstop sasa ww kaa unataka kila MTU aabudu anavotaka Itakua sio ya kidini tena Bali ya serikal au binafsi isiyonamlengo wa kidini
 
Swila Sekondari iliyopo Mbalizi jijini Mbeya haijasajiliwa kama shule ya kidini kwa maana ya religious school, imesajiliwa kama secular school lakini wanafunzi wote wanaosoma shule hiyo wanalazimishwa kuabudu katika madhehebu ya Moravian.

Mwanafunzi yeyote asiyeshiriki katika ibada za Moravian awe Msabato, M -Roman Catholic, M-lutheri, Muislamu anafukuzwa shule.

Hebu wadau nisaidieni hili linafanyikaje katika Tanzania yetu ambapo kila mtu ana haki ya kuabudu.

Katika shule inayofundishwa na walimu waliosomeshwa na walipa kodi wote wa nchi hii tena katika shule ya mtu binafsi?
Waamisheni watoto wenu tu
Haina haja ya kulalamika
 
Mkuu Domokaya

Hiyo shule tajwa hapo juu ni shule binafsi na siyo shule ya serikali hata kidogo au kusema ni shule ya wazazi kwamba masharti na vigezo anapanga mtu mwingine. Tujue kabisa shule zinaposajiliwa pia hupewa na mwongozo wa namna elimu inatolewa bila kuvunja sheria za nchi. Na kwa maelezo yako hapo juu nadhani umeshindwa tambua kuwa au hukuwahi kusoma hiyo "motto" ya shule au hata kusoma hizo joining instructions au matangazo ya kuomba nafasi ya mwanafunzi pale.

Nijuavyo mimi ile shule ni ya kikistro ila haibagui wanafunzi kwa minajili ya wewe ni dini gani. Kuna bango lao hapo mbalizi japo sikumbuki maneno halisi ila linasomeka kuwa Swilla schools ziko under Christian ministry. Huo ndio uelewa wangu wa haraka.

Lakini pia hayo madai ya kufukuzwa shule kisa dhehebu/dini ni ya kweli?. Ulifukuzwa wewe au una mwanao alifukuzwa?, je kama mzazi ulienda shuleni na kujua uhalisia wa kosa lililomfukuza shule?.

Bottom line. Nadhani ni vyema kutambua hizi shule za binafsi ni biashara na kila mmoja anajitahidi kuweka mazingira bora ya kuzalisha wasomi lakini mwisho wa siku wenye maadili. Hamna mtu angependa kuona mtoto anatoka shule ndio kwanza amekuwa mvuta bangi au kibaka.

Katika dunia ya sasa ya utandawazi na muanguko wa kimaadili tunahitaji shule zitakazotupa elimu bora kwa wanetu lakini pia watoke wakiwa ni watu wenye maadili. Kama wengine walivyosema mwisho wa siku hawabadilishi dini ya mtu pale, mtoto akirudi likizo au kumaliza basi anaendelea na mambo yake. Na nadhani kwa matokeo ya mwaka huu ni miongoni mwa shule zimefanya vizuri kimkoa.
 
Back
Top Bottom