Shule ya chekechea!

carmel

JF-Expert Member
Aug 24, 2009
2,836
262
Nataka kuanzisha shule ya Chekechea ambayo itakuwa darasa 1 la watoto wasiozidi 40! nahitaji kama shilingi ngapi kuanza hii project? na usajili ni lazima? process yake ikoje?
 
Asante Michelle,kumbe na wewe bahili hivi.
Usijali wadau watakuja,ila ungesema upo Maeneo gani,wa Mkoani au Dar.Halafu usubiri pia vidonge vyako.

Kwa ushauri wangu inabidi angalau uwe na madarasa kuanzia matatu,yaani Baby,Mid and TOP classes.
Maana mtoto wa nursery mara nyingi anakuwa mdogo na inabidi akulie hapo hapo shuleni na wengi hutumia miaka 3 ya chekechea,Sasa ukiwa na darasa moja la Baby(tahadhari,sio baby care,ni umri wa 3.5 na 4 yrs),kisha mwakani unawapeleka wapi ?wakati kuna Intake nyingine inakuja.
Lakini ukiwa na Madarasa matatu ni kwamba watakuwa wanaachana,yaani TOP class ni wale wamiaka 6 na 7 ambao wakitoka kwako wanaingia Primary,na wale wa Baby class wanapanda Mid na wa Mid wanapanda TOP,na wewe unachukua usajili wa Baby class tena.Huu ndio utaratabiu mzuri,la sivyo mzazi hawezi kuleta mtoto mwaka huu kisha mwakani amuhamishe kwenda kwenye Mid class shule nyingine.
Huo,ni mfano hai nimeutoa jinsi walivyosoma wanangu,kule Tabata katika Nursery ya Mtaani tu,kuna mama alikuwa Hodari sana,na sasa hivi wanangu wanakimbiza tu International School na wanafanya vizuri sana kwa mchango waliopata kwa mwalim wao wa chekechea.
Wazo zuri sana.
Lakini pia unaweza kuanza na moja kisha kila mwaka ukaongeza Jingine hadi yafikie Matatu.

Kwani si umuambie Mumeo ikulu akukopeshe pesa? "Joke"
 
Back
Top Bottom