Shule Vs Mafanikio

Ukuu na Mafanikio havipatikani kwa kwenda shule au kwa kuwa na degree. Kama ingekuwa ni shule basi Maprofesa ndo mabilionea wa dunia. Kwenda shule ni kitu kimoja na kufanikiwa kupitia shule yako ni jambo jingine. Kuna watu wana elimu kubwa ya darasani lakini ni masikini na kuna watu wameenda shule na wamefanikiwa sana, lakini pia kuna watu hawajaenda shule ila wamefanikiwa sana.

Kila mtu ana chance ya kufanikiwa haijalishi ni professor mwenye degree za kutosha au ni darasa la saba B au hujaenda shule kabisa. Ulimwengu ume-prove hili kupitia watu ambao wamefanya mambo makubwa duniani na hawakwenda shule. Watu hao ni kama Bill Gates, Bilionea Richard Branson, Michael Dell Mmiliki wa Computer za Dell, Abraham Lincoln Rais wa 16 wa Marekani na wengine wengi.

Nimelazimika kuandika andiko hili baada ya mmoja wa watu wanaofatilia maandiko yangu kwa ukaribu ambaye aliishia darasa la saba kuwa na hofu kwa kudhani kuwa Mafanikio ni kwaajili ya watu walioenda shule tu au Wasomi”.

Narudia tena Ulimwengu wenyewe umetudhihirishia hili kuwa watu wote tuna chance sawa ya kufanikiwa uwe umeenda shule au hujawahi kwenda kabisa. Ukiangalia hapa kwetu Tanzania watu wenye mafanikio makubwa ya kifedha wengi wao hawajaenda shule kabisa. Mimi naishi Mbeya, Hapa kwetu Mbeya Top 10 ya Matajiri wa Mbeya walioenda shule ni wawili tu hawa wengine wote ni darasa la saba.

Sasa ili kujiweka kwenye kundi la watu watakaofanikiwa haijalishi wewe ni Professor au umeishia darasa la saba au hujawahi kwenda shule kabisa ni lazima ufanye mambo yafuatayo;

1. Tambua Uwezo wako wa Kipekee.

Ili ujiweke kwenye nafasi ya kufanikiwa ni lazima kwanza ujue wewe ni bora kwenye eneo gani. Lazima ujue strengths zako. Je wewe ni mzuri zaidi kwenye biashara au wewe ni mzuri kwenye kilimo au unaweza zaidi kufuga au una kipaji cha aina fulani? Ukishajua eneo la ubora wako inakupa mwerekeo sahihi wa mapambano yako kuliko kukaa kupambana kwa kukisia mara leo upo kwenye kilimo kesho umehamia kwenye biashara mwezi ujao unaonekana unaigiz movie utakuwa unajichelewesha. Hakikisha unatulia na kujichunguza eneo la uwezo wako wa kipekee.

John Rockerfeller alijiona kuwa yeye ni bora kwenye biashara hivyo akawekeza nguvu zake zote huko. Diamond hajaenda shule ila alijijua kuwa yeye ni mzuri kwenye muziki hivyo akawekeza nguvu zake huko. Na wewe tafuta eneo lako kisha wekeza nguvu zako huko utafanikiwa.

2. Tafuta Maarifa (Knowledge).

Kukosa chance ya kwenda shule hakukunyimi chance ya kuwa na Maarifa. Sifa moja kuu ya watu wanaofanikiwa either wameenda shule au hawakwenda shule ni watu wanaotafuta maarifa. Abraham Lincoln hakwenda shule lakini alikuwa na Maarifa ndiyo maana aliaminiwa kuwa Rais wa Marekani. Michael Dell hakwenda shule lakini alijitafutia maarifa ambayo ndiyo yalimfanya afikie level ya kuwa na kampuni kubwa ya computer dunia nzima. Henry Ford hakusoma shule lakini alikuwa na maarifa na ndiyo maana aliweza kuongoza kampuni kubwa duniani ya uzalishaji wa magari, kama asingekuwa na maarifa Ford isingekuwepo mpaka leo hii. Maarifa yapo tu kwa mtu anayehitaji, unaweza kusoma vitabu, kusoma kozi za bure kwenye mitandao, kusoma Makala positive kama hii, kujifunza youtube.

“Unaweza kuwa na sababu za msingi za kukosa elimu ya darasani na kila mtu akakubaliana na sababu zako lakini huwezi kuwa na sababu za msingi za kukosa maarifa”. Maarifa ni kitu unajitafutia mwenyewe. Elon Musk amejifundisha mwenyewe kuandika code na akfikia kiwango cha kuwa miongoni wa Programmers wakubwa duniani. Uzuri ni kuwa kwa dunia ilipofikia sasa elimu ya darasani haina impact kubwa ukilinganisha na maarifa ya kujitafutia na ndiyo maana watu wanaojitafutia maarifa wanafanikiwa zaidi kuliko wale ambao wameenda shuleni kwani mengi ya wanayoyasoma shuleni huwa hawayatumii kwenye maisha yao na huwa wanasoma bila hata kujua umuhimu wake. Lakini mtu anayeamua kujitafutia mwenyewe huwa anatafuta maarifa ambayo yana msaada directly kwenye maisha yake. “Kama unataka kujiweka kwenye kundi la watu watakaofanikiwa basi hakikisha unayatafuta maarifa kwa hali na mali”.

3. Weka Malengo.

Hakikisha unakuwa unajua pale unapotaka kufika. Usitembee tu bila kuwa na picha ya kule unakoelekea, lazima uweke malengo ambayo yanakufanya upambane ukiwa unajua exactly kitu unachokitaka. Kuwa na Malengo ni jambo muhimu na la lazima kwa kila mwenye nia ya dhati ya kufanikiwa. Sijawahi kukutana na mtu aliyefanikiwa ambaye anasema amefika hapo alipofika bila kuwa na Malengo. Hakikisha unajiwekea malengo kuhusu level unazotaka kuzifikia kimafanikio.

4. Pambana kwa bidii ili ufikie Malengo yako.

Kuwa na uwezo wa kipekee ni jambo moja na ni muhimu sana, kuwa na Maarifa ni muhimu pia na kuweka malengo ni kitu cha lazima lakini hivi vyote havina maana kama utakuwa navyo halafu ukaa tu. Ukishakuwa na hivyo vyote sasa ni lazima uingie kwenye mapambano kuhakikisha unafikia malengo yako ili kuwa na kiwango cha mafanikio unayoyataka. Kumbuka kuwa kuwa na uwezo mkubwa au kipaji kikubwa bila kupambana hutafika popote, Lakini pia kuwa na Maarifa mengi bila kuyaweka kwenye matendo ni kazi bure, na malengo bila mapambano hayawezi kutimia. Ingia kwenye Mapambano. Hapa kwenye mapambano ndiyo mahali penye ugumu mkubwa. Hapa lazima ujiweke sawasawa kivita, lazima ukubali kuvuja jasho, kutoa damu, kutoa machozi, kukosa usingizi na kuwa tayari kulipa kila aina ya gharama ili kufikia malengo yako.

Live Your Dream!!
Konga Fadhili
Mungu akubariki uendelee kufundisha mambo ya msingi kama haya
 
So wote ni wazungu mkuu, mazingira yao na yetu ni tofauti kabisa. Tupe mifano ya wabongo ambao hawakwenda shule lakini ni mabilionea.
 
Naona mafanikio umeyaelezea kwa muktadha wa kuwa na utajiri tu/pesa/bilionea/milionea zaidi

Je hayo ndo mafanikio pekee maishani?

Vipi kuhusu afya na familia bora,elimu dunia ya mambo mbali mbali nk

Pesa ni muhimu ila si kila kitu
 
Na kiasi gani ndio utajiri?
Hadi uwe bakhresaa?ama Mo
Au ukiwazidi mtaani kifedha ?

Ama ukiweza pata mahitaji ya msingi and extra luxuries?..

Kila mtu ana kipimo cha pesa anayohitai
 
Kwenda shule ni some times ni kupoteza muda!!!

Kuna watu watasema nasema hivo sabab cjaenda shule..mm nmesoma sn ndo maana masema hiv
Uko sahihi mkuu hata Mimi nimegundua hilo.
Kwa Tanzania kadri unavyozidi kusoma sana ndio kadri unavyozidi kupunguza asilimia za kufanikiwa na kuwa kituko ktk jamii.
E.g Lpumba,Palamgamba,Shika.
 
Nilichojifunza hapa ni kuwa KOMAA NA MAARIFA YA KITU AMBACHO UNATAKA KUWA MASTER NACHO.
Yes ulaya ndio wanaishi hivyo.
Kuna watu kule German Wana certificates za Engineering tu na wanaspecialize tangu akiwa primary anasoma mashine moja tu.
Sasa ukienda naye site mwenye masters au phd ya tz akasome.
 
Mkuu hongera sana umeongea vizuri sana na umefafanua hoja zako vizuri sana...
Ila kusema Bill Gates hajasoma unakosea mkuu yule ni university dropout mwenyewe amewahi kusema yeye ni valedictorian of his own class na ni tajiri wa kwanza duniani pia Aliko Dangote ni tajiri wa kwanza kwa Africa kasoma chuo kikuu Misri ukija hapa Tanzania tuna mabilionea wawili ambao wote wana elimu ya chuo kikuu tena nje ya nchi..
Nenda Angola etc
Naunga mkono hoja yako ila elimu ya darasani ni muhimu kama ulielimika sio ulimaliza masomo tu yako..
Hata Kama hao uliowataja wamesoma lkn hawakusoma Kama sisi kukariri masomo 20 kwa mwaka bali walikuwa wanasoma huku wakijiandaa na talent yake itakayompatia pesa badae.
Na huu ndio usomaji wa wazungu na wahindi,hawasomi Kama sisi ile unakomaa hadi masters halaf hujui utafanya kazi gani
 
Exactly umetisha sana ishu kumbe sio kwamba elimu haina msaada ila elimu ya aina gani tunayopata ndio itaamua tuishie wapi kujikwamua kiuchumi.
 
tatizo linalofanya shule isionekane nichanzo cha mafanikio huku ikiwa mafanikio yana itaji maarifa na shule inatoa maarifa ni kwa sababu...binadam hufanikiwa kwa kufanya kitu anachopenda ndipo unakutana natatizo la shule zetu kutufundisha ilimrad bila ata kumuelewa mwanafunzi anapenda nini zaidi...ndiomana mwisho wa siku waliofanikiwa niwatu walio jiongeza ..watoto wa mjini wanasema

...by mjukuu wa king solomon
 
Shule na mafanikio vinaenda pamoja. Shule inaondoa ujinga ili uweze kupambana kwa weledi wa hali ya juu. Mafanikio bila shule ni kubahatisha ndio maana kazi nyingi za waliofanikiwa bila shule hufanywa na walioenda shule. Shule + mafanikio ni raha zaidi kuliko mafanikio bila shule.
 
Mmmmmmmmh kwani kusema mtu amesoma ni mpaka afikie kiwango gani?maana hata kuishia darasa LA saba napo ni kusoma au umeclaim mpaka awe degree holder?maana in real sense hakuna tajiri duniani ambaye ajasoma na kama unamjua naomba unitajie,ko bandiko lako linakosa mantiki maana kukuta MTU hajasoma na ni tajiri never,may be huseme KIWANGO CHA ELIMU VS MAFANIKIO OK.
Ukuu na Mafanikio havipatikani kwa kwenda shule au kwa kuwa na degree. Kama ingekuwa ni shule basi Maprofesa ndo mabilionea wa dunia. Kwenda shule ni kitu kimoja na kufanikiwa kupitia shule yako ni jambo jingine. Kuna watu wana elimu kubwa ya darasani lakini ni masikini na kuna watu wameenda shule na wamefanikiwa sana, lakini pia kuna watu hawajaenda shule ila wamefanikiwa sana.

Kila mtu ana chance ya kufanikiwa haijalishi ni professor mwenye degree za kutosha au ni darasa la saba B au hujaenda shule kabisa. Ulimwengu ume-prove hili kupitia watu ambao wamefanya mambo makubwa duniani na hawakwenda shule. Watu hao ni kama Bill Gates, Bilionea Richard Branson, Michael Dell Mmiliki wa Computer za Dell, Abraham Lincoln Rais wa 16 wa Marekani na wengine wengi.

Nimelazimika kuandika andiko hili baada ya mmoja wa watu wanaofatilia maandiko yangu kwa ukaribu ambaye aliishia darasa la saba kuwa na hofu kwa kudhani kuwa Mafanikio ni kwaajili ya watu walioenda shule tu au Wasomi”.

Narudia tena Ulimwengu wenyewe umetudhihirishia hili kuwa watu wote tuna chance sawa ya kufanikiwa uwe umeenda shule au hujawahi kwenda kabisa. Ukiangalia hapa kwetu Tanzania watu wenye mafanikio makubwa ya kifedha wengi wao hawajaenda shule kabisa. Mimi naishi Mbeya, Hapa kwetu Mbeya Top 10 ya Matajiri wa Mbeya walioenda shule ni wawili tu hawa wengine wote ni darasa la saba.

Sasa ili kujiweka kwenye kundi la watu watakaofanikiwa haijalishi wewe ni Professor au umeishia darasa la saba au hujawahi kwenda shule kabisa ni lazima ufanye mambo yafuatayo;

1. Tambua Uwezo wako wa Kipekee.

Ili ujiweke kwenye nafasi ya kufanikiwa ni lazima kwanza ujue wewe ni bora kwenye eneo gani. Lazima ujue strengths zako. Je wewe ni mzuri zaidi kwenye biashara au wewe ni mzuri kwenye kilimo au unaweza zaidi kufuga au una kipaji cha aina fulani? Ukishajua eneo la ubora wako inakupa mwerekeo sahihi wa mapambano yako kuliko kukaa kupambana kwa kukisia mara leo upo kwenye kilimo kesho umehamia kwenye biashara mwezi ujao unaonekana unaigiz movie utakuwa unajichelewesha. Hakikisha unatulia na kujichunguza eneo la uwezo wako wa kipekee.

John Rockerfeller alijiona kuwa yeye ni bora kwenye biashara hivyo akawekeza nguvu zake zote huko. Diamond hajaenda shule ila alijijua kuwa yeye ni mzuri kwenye muziki hivyo akawekeza nguvu zake huko. Na wewe tafuta eneo lako kisha wekeza nguvu zako huko utafanikiwa.

2. Tafuta Maarifa (Knowledge).

Kukosa chance ya kwenda shule hakukunyimi chance ya kuwa na Maarifa. Sifa moja kuu ya watu wanaofanikiwa either wameenda shule au hawakwenda shule ni watu wanaotafuta maarifa. Abraham Lincoln hakwenda shule lakini alikuwa na Maarifa ndiyo maana aliaminiwa kuwa Rais wa Marekani. Michael Dell hakwenda shule lakini alijitafutia maarifa ambayo ndiyo yalimfanya afikie level ya kuwa na kampuni kubwa ya computer dunia nzima. Henry Ford hakusoma shule lakini alikuwa na maarifa na ndiyo maana aliweza kuongoza kampuni kubwa duniani ya uzalishaji wa magari, kama asingekuwa na maarifa Ford isingekuwepo mpaka leo hii. Maarifa yapo tu kwa mtu anayehitaji, unaweza kusoma vitabu, kusoma kozi za bure kwenye mitandao, kusoma Makala positive kama hii, kujifunza youtube.

“Unaweza kuwa na sababu za msingi za kukosa elimu ya darasani na kila mtu akakubaliana na sababu zako lakini huwezi kuwa na sababu za msingi za kukosa maarifa”. Maarifa ni kitu unajitafutia mwenyewe. Elon Musk amejifundisha mwenyewe kuandika code na akfikia kiwango cha kuwa miongoni wa Programmers wakubwa duniani. Uzuri ni kuwa kwa dunia ilipofikia sasa elimu ya darasani haina impact kubwa ukilinganisha na maarifa ya kujitafutia na ndiyo maana watu wanaojitafutia maarifa wanafanikiwa zaidi kuliko wale ambao wameenda shuleni kwani mengi ya wanayoyasoma shuleni huwa hawayatumii kwenye maisha yao na huwa wanasoma bila hata kujua umuhimu wake. Lakini mtu anayeamua kujitafutia mwenyewe huwa anatafuta maarifa ambayo yana msaada directly kwenye maisha yake. “Kama unataka kujiweka kwenye kundi la watu watakaofanikiwa basi hakikisha unayatafuta maarifa kwa hali na mali”.

3. Weka Malengo.

Hakikisha unakuwa unajua pale unapotaka kufika. Usitembee tu bila kuwa na picha ya kule unakoelekea, lazima uweke malengo ambayo yanakufanya upambane ukiwa unajua exactly kitu unachokitaka. Kuwa na Malengo ni jambo muhimu na la lazima kwa kila mwenye nia ya dhati ya kufanikiwa. Sijawahi kukutana na mtu aliyefanikiwa ambaye anasema amefika hapo alipofika bila kuwa na Malengo. Hakikisha unajiwekea malengo kuhusu level unazotaka kuzifikia kimafanikio.

4. Pambana kwa bidii ili ufikie Malengo yako.

Kuwa na uwezo wa kipekee ni jambo moja na ni muhimu sana, kuwa na Maarifa ni muhimu pia na kuweka malengo ni kitu cha lazima lakini hivi vyote havina maana kama utakuwa navyo halafu ukaa tu. Ukishakuwa na hivyo vyote sasa ni lazima uingie kwenye mapambano kuhakikisha unafikia malengo yako ili kuwa na kiwango cha mafanikio unayoyataka. Kumbuka kuwa kuwa na uwezo mkubwa au kipaji kikubwa bila kupambana hutafika popote, Lakini pia kuwa na Maarifa mengi bila kuyaweka kwenye matendo ni kazi bure, na malengo bila mapambano hayawezi kutimia. Ingia kwenye Mapambano. Hapa kwenye mapambano ndiyo mahali penye ugumu mkubwa. Hapa lazima ujiweke sawasawa kivita, lazima ukubali kuvuja jasho, kutoa damu, kutoa machozi, kukosa usingizi na kuwa tayari kulipa kila aina ya gharama ili kufikia malengo yako.

Live Your Dream!!
Konga Fadhili
 
Safi sana...

Ili ufanikiwe fanya kile unachokiweza zaidi kwa ufanisi na moyo wote... kitakuletea mafanikio unayoyatazamia...

Cc: mahondaw
 
Hahaha kwani mafanikio ni nini pesa au vitu?!
Kusoma ni kujiandaa au unaandaliwa ukatumike.
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom