Shule ni ngumu kuliko mtaa

Jokajeusi

JF-Expert Member
Jun 1, 2018
6,305
10,582
Wakuu!

Kwa uzoefu wangu, ninaona shule ni ngumu kuliko kitaa.

Mimi nikikuburuza shuleni ukakaa, basi jua mtaani hutonishinda kwa chochote kile hata kuzaa tuu watoto ambao ni bure kabisa.

Kuna mdau kaanzisha mada kasema Vipanga jeuri mtaa unawanyoosha, kiukweli mimi nilishaapa kuwa nikikuzidi kiakili darasani basi jua kimtaa hutanizidi, na hilo nimelimudu.

Masomo ni magumu kuliko mtaa. Mitihani ya darasani ni migumu kuliko ya kitaa.

Kitaa wajinga wapo wengi ni uwezo wako kuwatumia. Kitaa fursa zipo nyingi ni uwezo wako kuzitumia. Unashindwaje kwa mfano?

Darasani waalimu walikuwa wachache na vitabu vilikuwa vichache lakini bado watu tulinyoosha misonge na kuweka vijiti, NECTA wanatujua, TCU wanatujua, na mtaani wanatujua.

Hakuna kazi rahisi kama kupata pesa kwenye jamii masikini na watu wajinga. Ila hakuna kazi ngumu kama kupata elimu kwenye jamii masikini na watu wajinga.
 
Ndio maana wageni wakija hawataki kuchomoka huku. Fursa zipo sema ukienda na akili za watu wa mtaani unapotea inabidi ujielewe na uchukue advantage ila ukikaa na watu wa kulialia maisha magumu hutoboi. Jiweke tu karibu na watu wenye akili chanya mambo yananyooka.
 
Wasomi wengi wakija mtaa, mitaa inawashinda torati za mitaa hawaziwezi, elimu yao haiakisi mitaa wengi wanasoma ili wakaajiriwe na si wakaajiri.
 
1) Walio na maisha magumu katika jamii ya vipanga ni asilimia ngapi ya vipanga wote?

2) Wenye maisha magumu katika jamii isiyo vipanga ni asilimia ngapi katika jamii ya wasio vipanga?

Hizi data zikipatíkana ndio zitaondoa utata kuliko kuangalia jumla jumla kwa mifano miwili mitatu ya kila upande
 
Wasomi wengi wakija mtaa, mitaa inawashinda torati za mitaa hawaziwezi, elimu yao haiakisi mitaa wengi wanasoma ili wakaajiriwe na si wakaajiri.

Wasomi uchwara, jitu linasoma alafu linajitenga na jamii yake.
 
Ati mtu usome alafu ukose hata hela ya kula, kuendesha maisha yako, wewe si lofa tuu!

Wasomi wengi kinachowaponza ni high expectation than Creativity
Huu ni ukweli kabisa mtu anaona akishakua na cheti basi mambo yatajileta tu yenyewe ndio maana wengi kitaa wanapagawa, wanatoka na expectations kubwa sababu ya ma vyeti yao huku creativity ni 0.....ckitaa fursa bado zipo hatujawa na maisha magumu kushinda hata wa Kenya hapo.
 
Huu ni ukweli kabisa mtu anaona akishakua na cheti basi mambo yatajileta tu yenyewe ndo maana wengi kitaa wanapagawa,, wanatoka na expectations kubwa sababu ya ma vyeti yao huku creativity ni 0 .....kitaa fursa bado zipo hatujawa na maisha magumu kushinda hata wa Kenya hapo

Na dharau, mtu anadharau kazi kwa nini asihenyeke
 
Hahaha madogo wanatoka na mavyeti yenye marks mingi wanajua hizo marks ndo kila kitu mtu anakwambia sifanyi kazi chini ya laki 8 au milioni wakati hata experience hana kabisa mwisho wa siku wanaishia tu kua na stress kitaa

Utadhani amesomea jambo linaloisaidia jamii kuliko wengine
 
Wakuu!

Kwa uzoefu wangu, ninaona shule ni ngumu kuliko kitaa.

Mimi nikikuburuza shuleni ukakaa, basi jua mtaani hutonishinda kwa chochote kile hata kuzaa tuu watoto ambao ni bure kabisa.

Kuna mdau kaanzisha mada kasema Vipanga jeuri mtaa unawanyoosha, kiukweli mimi nilishaapa kuwa nikikuzidi kiakili darasani basi jua kimtaa hutanizidi, na hilo nimelimudu.

Masomo ni magumu kuliko mtaa. Mitihani ya darasani ni migumu kuliko ya kitaa.

Kitaa wajinga wapo wengi ni uwezo wako kuwatumia. Kitaa fursa zipo nyingi ni uwezo wako kuzitumia. Unashindwaje kwa mfano?

Darasani waalimu walikuwa wachache na vitabu vilikuwa vichache lakini bado watu tulinyoosha misonge na kuweka vijiti, NECTA wanatujua, TCU wanatujua, na mtaani wanatujua.

Hakuna kazi rahisi kama kupata pesa kwenye jamii masikini na watu wajinga. Ila hakuna kazi ngumu kama kupata elimu kwenye jamii masikini na watu wajinga.
Huyu mtoto ana akili sana. Ni watu wachache sana wanaolijua hili
 
Back
Top Bottom