Shule kunufaika na mpango wa satelaiti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shule kunufaika na mpango wa satelaiti

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 14, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na Kampuni ya Multichoice Africa imezindua mpango maalumu wa kusambaza vifaa vya kisasa katika Shule mbalimbali nchini kwa ajili kutoa vipindi vya elimu.
  Mpango huo ambao unajulikana kama 'Multichoice Resource Centre programme' umezinduliwa jana na Meneja mkuu wa Multichoice Tanzania Limited, Peter Fauel, ambapo shule hizo zitanufaika kwa kuwekewa teknolojia ya Setelaiti na kufundishwa masomo kwa kutumia kituo cha elimu cha Dstv Education Boutuet.
  Meneja huyo alisema mpango huo huwezesha shule kupata huduma ya kisasa zaidi katika nyanja za teknolojia ya satalaiti ili kuweza kupata vipindi vya masomo ya sayansi ya wanyama, Jiografia, Historia pamoja na kupata taarifa mbalimbali za habari kupitia BBC.
  Aidha, Fauel alisema kutokana na Tanzania kuwa nyuma katika kutumia teknolojia hiyo mpango huo utawezesha kupatikana kwa elimu bora hata katika sehemu za ndani zaidi ya nchi na itawanufaisha walimu na wanafunzi bila kuzingatia mipaka ya eneo.
  Shule 20 nchini Tanzania, tayari zinafanya majaribio juu ya mpango huo zikiwemo shule za mkoa wa Dar es salaam. Hata hivyo mpango kama huo umeanzishwa katika nchi 22 za Afrika.
  Mwakilishi wa Wizara ya Elimu na mafunzo ya Unfundi Selestine Gesimba, alisisitiza juu ya umuhimu wa teknolojia katika kutoa ujuzi wa kisasa zaidi. Alisema kupitia mpango huu, kutawezesha upatikanaji wa ujuzi kwa upana zaidi huku ikichangia kuongezeka kwa utafiti.  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hivi tunakagua relevance ya hivi vitu au basi tu kila kitu twaenda tu kichwakichwa?
   
 3. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  kwa nini wamechagua dar es salaaam. sio lindi kigoma au rukwa. Aliyenacho anaongegezewa
   
Loading...