Shule kumi ghali Tanzania

Milioni 70 ada tu kwa mwaka kwa miaka Sita hadi form Six na matumizi mengine ni wastani wa kalibu Tsh. milioni Mia Tano.
Ukichukua na ghalama za Shule ya Chekechea miaka 2 na Msingi miaka 7 inakaribia Tsh Billioni moja

Ndo sababu nimesema iyo ni bln sasa kweli mimi nataka iyo hela asome tu basi? Hiyo hamnaga aisee
 
SHULE KUMI GHALI ZAIDI TANZANIA.

1- International School of Tanganyika (IST)
— Hii ndio shule ghali zaidi nchini. Iko jijini Dar Es Salaam na hufuata Mtaala wa IB. IST hutoza ada kuanzia shilingi za Kitanzania milioni 34 kwa chekechea hadi shilingi milioni 71 kwa sekondari, kwa mwaka.

2. Braeburn International School
—Hii ni shule ya kimataifa ambayo iko Dar Es Salaam na Arusha. Hufuata mfumo wa IB na ada yake kwa mwaka ni kuanzia shilingi za Kitanzania milioni 20 kwa shule ya msingi hadi shilingi milioni 43 kwa sekondari.

3. Dar Es Salaam International Academy (DIA)
—Hii ni shule ya tatu kwa kuwa na ada ghali zaidi nchini. Iko Dar Es Salaam na hufuata Mtaala wa IB. Ada yake kwa mwaka ni kuanzia Shilingi za Kitanzania milioni 23 kwa shule ya msingi hadi shilingi milioni 40 kwa sekondari.

4. Iringa International School (ISS)
— Iko mkoani Iringa na hufuata mitaala miwili ya IB na ule wa Cambridge. Hutoza ada kati ya Shilingi za Kitanzania milioni 17 kwa Chekechea hadi milioni 27 kwa sekondari.

5. Saint Constantine International School
—Inapatikana mkoani Arusha na hufuata Mtaala wa Cambridge. Ada yake ni kati ya Shilingi za Kitanzania milioni 8 kwa Chekechea hadi shilingi za Kitanzania milioni 23 kwa sekondari.

6. Kennedys House Schools
—Shule za Kennedys ziko maeneo mengi duniani. Nchini Tanzania iko katika mkoa wa Arusha wakiendesha Chekechea na Shule ya Msingi. Ada zao huanzia Shilingi za Kitanzania milioni milioni 8 kwa Chekechea hadi milioni 22 kwa Shule ya Msingi. Shule hii hufuata Mtaala wa Cambridge.

7. Haven of Peace Academy (HOPAC)
—HOPAC ipo katika Jiji la Dar Es Salaam. Hufuata Mtaala wa Cambridge na hutoza ada kati ya shilingi za Kitanzania milioni 16 hadi 22 kwa mwaka.

8. Aga Khan Primary & Secondary School
—Shule hii iko katika Jiji la Dar Es Salaam, na hufuata Mtaala wa IB kama ilivyo ISM. Hutoza ada kuanzia Shilingi za Kitanzania milioni 7 hadi milioni 20.

9. Internation School Moshi (ISM)/ UWC East Africa
— Hii ndio shule ghali zaidi katika mkoa wa Kilimanjaro. Hutoza ada kuanzia shilingi za Kitanzania milioni 16 kwa chekechea hadi shilingi za Kitanzania milioni 41 kwa wale wa kidato cha tano na sita. Shule hii hufuata Mtaala wa International Baccalaureate (IB).

10.Morogoro International School (MIS)
—Hii inapatikana mkoani Morogoro na hufuata mtaala wa Cambridge. MIS hutoza kuanzia Shilingi za Kitanzania milioni 6.4 kwa chekechea hadi shilingi za Kitanzania milioni 18 kwa sekondari. Hii ni ada peke yake, mbali na fedha ya usajili na boarding kwa wale wanaolala shuleni.

Huna hela wewe wenzako wanazo .....
Kuna haja ya kuzifanyia uchunguzi, nina mashaka kuna Watanzania wenzetu wanakamuliwa bure hapo! Hata ukitazama matokeo ya kidato cha IV 2020/2021 yaliyotangazwa mwaka jana (2021), utakuta ndani ya shule 10 bora hakuna hata moja kati ya hizo!
 
Hizo shule ndiyo wanaosoma watoto wa vigogo na wafanya biashara wakubwa nchini,, ambao wakimaliza mpaka mavyuoni, tayari wana nafasi zao serikalini huko,,
Wapi shule za kata????
Yani umlipie ada mamilioni yote hayo halafu aje aajiriwe na sisi huku serikalini duh!
 
Hizo shule ndiyo wanaosoma watoto wa vigogo na wafanya biashara wakubwa nchini,, ambao wakimaliza mpaka mavyuoni, tayari wana nafasi zao serikalini huko,,
Wapi shule za kata????
Mkuu ukisoma kwa ada hiyo.....sidhani kama kuna proffesion yoyote nchini inaweza kukulipa mshahara unaoendana na ada yako kwenye hii serikali yetu so sad......
Inabidi uwe mfanyabiashara
 
Kuna haja ya kuzifanyia uchunguzi, nina mashaka kuna Watanzania wenzetu wanakamuliwa bure hapo! Hata ukitazama matokeo ya kidato cha IV 2020/2021 yaliyotangazwa mwaka jana (2021), utakuta ndani ya shule 10 bora hakuna hata moja kati ya hizo!
Sasa umeambiwa hizo ni international school zinafata curriculum za IB na Cambridge bila shaka haziusiani na NECTA hizo mkuu.

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Kuna haja ya kuzifanyia uchunguzi, nina mashaka kuna Watanzania wenzetu wanakamuliwa bure hapo! Hata ukitazama matokeo ya kidato cha IV 2020/2021 yaliyotangazwa mwaka jana (2021), utakuta ndani ya shule 10 bora hakuna hata moja kati ya hizo!
Hizo shule hazipo chin ya mitaala ya NECTA ndio maana uwezi kuziona kwenye hio orodha. Wao wanatumia mitaala ya nje
 
Elimu ya sasa ni biashara, na ukiteleza na kuingia kwenye huo mtego, utajikuta unatumia gharama kubwa kwa kitu cha kawaida. Jiulize hawa maprofesa tulionao, walisoma huko? Ni sawa na duka A ununue mirinda kwa 500 huku duka B mirinda hiyo hiyo inauzwa 10,000. Kule watakachotofautiana zaidi ni lugha tu, lakini haina maana akisoma kule kuna uhakika wa kuja kuwa Director wa IMF/ world bank.
Hapo japo ni brand kuwa kasoma wapi wapi lakini pia hizo zinaubora zaidi ukilinganisha na hizo zingine.
 
Back
Top Bottom