Shule Dar yatoza ada ya shilingi 60 milioni!

Shule Dar yatoza ada ya shilingi 60 milioni!

Naona watu mnashabikia tu....hiyo Ada nanyi mnachangia kuwalipia kwa hao mabosi zenu bila kujijua.....leo hii kibarua analipwa 2500/- kwa siku,watu wanafanya ufisadi ili watoto zao waendelee kuwepo ktk hizo shule......!
 
IST pale Upanga unalipa michango ya ziada + ela za form kama milioni 18+ na bado mtoto wako haruhusiwi kuingia darasani (kama hujalipa ada yenyewe ya mafunzo)
Sasa kama unalipa milioni 18+ halafu huna ada ya mafunzo utakuwa mjinga.
 
Nimeona hapo na wao wanatoa Michango ya Majengo ina maana na wao kila siku Hizo Shule zinakarabatiwa?....
 
nitampeleka mwanangu nikishazaa na mahabuba @lara1
 
Mil 60 si unajenga nyumba kabisa. Watu wanachezea hela aisee

Mkuu hawachezei bali wanatumia fedha kuwekeza kwenye elimu ya watoto wao.Wewe unafikiria nyumba wenzako nyumba kwao siyo issue hivyo wanaona elimu ndiyo issue.Mimi nakubali tu kuwa tangu Dunia hii imeumbwa haijawahi kuwa sawa kwa wote!
 
Mleta uzi au mwandishi wa makala hii kwenye gazeti anapiga porojo tu. Kwanza, Watanzania wote hatulingani kwa kipato. Ndio maana tunatofautiana kwenye umiliki wa magari, nyumba, matumizi ya chakula na vinywaji, nk.

Kwa kumbukumbu ndogo, tangu miaka ya 60 hadi kufikia 80 kama siyo 90, shule binafsi zilikuwepo lakini shule bora zilikuwa za serikali. Ndiyo sababu wakati huo hata watoto wa vigogo wa Kiafrika walikuwa wanasoma shule hizo. Wengi wa waliokuwa na uwezo mdogo ndio walikuwa wanaomba nafasi shule za binafsi hasa ngazi ya sekondari. Wahindi wamekuwa na shule zao kwa sababu ya matabaka yaliyotengenezwa na mkoloni mwingereza kwa sababu zao. Wasilaumiwe. Tunachotakiwa kufanya sasa kama taifa ni kurejsha ubora wa shule za serikali badala ya kupoteza muda na nguvu nyingi kufukuzana na shule binafsi. Ubora wa elimu ya vijana wetu ndilo suala la msingi.
 
Atakama ada ingekuwa mil 100 kama ni private sio tatizo; hoja ya msingi kwenye elimu ya Tanzania kwanini kuwe na gap baina ya shule za serikari zingine zitoe ufaulu mzuri na zingine zifanye vibaya, kwanini asilimia kubwa sana ya wanafunzi kuanzia la kwanza mpaka form four wengi wao awafikii criteria za uelewa zinazotakiwa.

Kwa minajili hiyo issue ni quality ya kiwango cha elimu wanayopata wanafunzi wa shule za serikari, investment ya elimu ya sasa, uamasishaji wa wazazi na mambo mengine ya msingi ambayo serikari ina role; hizi habari za GPA/Division marking au what private is doing sio hoja hasa za msingi la tatizo la elimu hapa ni kama serikari inatakufanya mazingaombwe tu ili kujitoa katika hoja za msingi kwa wale ambao hizo ada za private wakipata ni kama kushinda bahati nasibu ya maisha.

Swala la jamii mwanafunzi kila anapopita anatakiwa awe na level gani ya uelewa na asilimia ngapi wanafanikiwa sio kukimbia majukumu ya serikari na elimu halafu kuanza kuleta mambo ambayo hayana tija kwa wengi; iweje wawekezaji wageni wanapendezewa wafanyakazi wa kutoka nje ya nchi kuliko wazawa mbona waziri akutani nao hao ili kujua sababu zao kusudi serikari waje na mikakati ya ku-intervene kwenye elimu kufikia viwango wanavyotaka. Hawa jamaa wanapenda zuga sana sijui kwanini amuwaoni for what they are Phd my foot.
 
Mleta uzi au mwandishi wa makala hii kwenye gazeti anapiga porojo tu. Kwanza, Watanzania wote hatulingani kwa kipato. Ndio maana tunatofautiana kwenye umiliki wa magari, nyumba, matumizi ya chakula na vinywaji, nk.

Kwa kumbukumbu ndogo, tangu miaka ya 60 hadi kufikia 80 kama siyo 90, shule binafsi zilikuwepo lakini shule bora zilikuwa za serikali. Ndiyo sababu wakati huo hata watoto wa vigogo wa Kiafrika walikuwa wanasoma shule hizo. Wengi wa waliokuwa na uwezo mdogo ndio walikuwa wanaomba nafasi shule za binafsi hasa ngazi ya sekondari. Wahindi wamekuwa na shule zao kwa sababu ya matabaka yaliyotengenezwa na mkoloni mwingereza kwa sababu zao. Wasilaumiwe. Tunachotakiwa kufanya sasa kama taifa ni kurejsha ubora wa shule za serikali badala ya kupoteza muda na nguvu nyingi kufukuzana na shule binafsi. Ubora wa elimu ya vijana wetu ndilo suala la msingi.
Kabisa hii ndio hoja serikari inayoikimbia siku zote kwenye kuporomoka kwa elimu na kila mara wakiibuka kwenye issue za elimu ni kuja na visingizio tu kila uchao vya kutafuta wachawi na mambo yasiyo wahusu wazazi wanaotumia public schools.
 
peleka mtoto wako kwenye shule utakayomudu kuilipia.

wakimaliza hapo watasema kuna hoteli chumba dollar 200, na sahani ya wali dollar 20 , na watashauri serekari iingilie kati kuuza wali sh. 1500 kwa sahani kama kwa mama ntilie... upuuzi mtupi shule za bure zipo peleka huko mwanao acha husda
 
Back
Top Bottom