Shukuru kama umepata mwenzi mwaminifu katika ndoa

manuu

JF-Expert Member
Apr 23, 2009
4,064
10,731
Walikutana wakiwa chuoni wakaanzisha uhusiano na baada ya mwanaume kumaliza chuo mpenzi wake akiwa mwaka wa mwisho wakoana kwa harusi.

Maisha yakaenda wakapata mtoto na mume akapata kazi mkoa tofauti na walipo kuwa wakisoma.Ikambidi aende kule kwa makubaliano mke wake akimaliza chuo watahamia wote sehemu mume alipo pata kazi.

Mke alipoachwa huku nyuma akiwa anamalizia chuo akianzisha uhusiano na kijana mmoja wa mtaani.Mapenzi yao yakapamba moto sana.Mume wake alikuwa akija kila weekend na hakuwahi kujua mke wake yupo na mahusiano nje ya ndoa yao.

Mke kamaliza degree yake akahamia kule mume wake alipo pata kazi.Akakaa kidogo akamwambia mume wake anataka kusoma masters ila anataka akasomee chuo kile kile alichosomea degree.

Mume akamkubalia kwa makubaliano awe anaenda home kila baada ya wiki 2 kumcheki mtoto.Mke ameanza masomo yake ya Masters na lengo kubwa si masomo lakini alitafuta chansi ya kuwa karibu na mchepuko wake.

Sasa hivi yule mke amaehamia kwa jamaa anaamkia hapo anaenda chuo na kurudia hapo yaani mume anajua mke yupo chuo kumbe mke kila usiku anakumbatiwa na mwanaume mwingine.

Si nzuri sana maana mke ni binti mdogo tu kama 25 yrs hafanani na tabia anayoifanya kabisa lakini ndiyo maisha ameyaamua hayo.

Tuombe Mungu sana atupe wenza waaminifu.Maana imagine yule bwana akija kugundua hili atakuwa kwenye hali gani.
 
Mmmh! Si ndo mana wengine wanatembea na miguu ya kuku! Ndo dawa yake huyo! Mumewe hamtoshi?? Mweeh! Distance nayo majanga! Afu huyo mume naye apimwe!
 
Mwambie km rafki yako maana anahangaika na mtu ambaye hana future nae.ajue tu mapema maana isijekuwa una plan na mtu kumbe na yeye ana plan na mtu mwngne unakuta unapoteza mda bure ambao huo muda hautajirudia tena.usikute jamaa nae anasoma hii article jf sshv ila hajui km inamhusu daahhhhh
 
Walikutana wakiwa chuoni wakaanzisha uhusiano na baada ya mwanaume kumaliza chuo mpenzi wake akiwa mwaka wa mwisho wakoana kwa harusi.

Maisha yakaenda wakapata mtoto na mume akapata kazi mkoa tofauti na walipo kuwa wakisoma.Ikambidi aende kule kwa makubaliano mke wake akimaliza chuo watahamia wote sehemu mume alipo pata kazi.

Mke alipoachwa huku nyuma akiwa anamalizia chuo akianzisha uhusiano na kijana mmoja wa mtaani.Mapenzi yao yakapamba moto sana.Mume wake alikuwa akija kila weekend na hakuwahi kujua mke wake yupo na mahusiano nje ya ndoa yao.

Mke kamaliza degree yake akahamia kule mume wake alipo pata kazi.Akakaa kidogo akamwambia mume wake anataka kusoma masters ila anataka akasomee chuo kile kile alichosomea degree.

Mume akamkubalia kwa makubaliano awe anaenda home kila baada ya wiki 2 kumcheki mtoto.Mke ameanza masomo yake ya Masters na lengo kubwa si masomo lakini alitafuta chansi ya kuwa karibu na mchepuko wake.

Sasa hivi yule mke amaehamia kwa jamaa anaamkia hapo anaenda chuo na kurudia hapo yaani mume anajua mke yupo chuo kumbe mke kila usiku anakumbatiwa na mwanaume mwingine.

Si nzuri sana maana mke ni binti mdogo tu kama 25 yrs hafanani na tabia anayoifanya kabisa lakini ndiyo maisha ameyaamua hayo.

Tuombe Mungu sana atupe wenza waaminifu.Maana imagine yule bwana akija kugundua hili atakuwa kwenye hali gani.
Hakuna marefu yasiyokuwa na mwisho, huyo dada anafikiri anakula maisha kumbe anajikulawenyewe, mwishowe atajimaliza mwenyewe
 
Hakuna MUME wala MKE mwaminifu ni just muda tu then UTAGONGEWA au MUME atatoka nje. So stay Calm and continue to CHEAT......Because if you don't the HE/SHE will.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom