shukurani yake kwa tovuti ya Facebook | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

shukurani yake kwa tovuti ya Facebook

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Feb 25, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Feb 25, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Baba mmoja nchini Misri amempa mtoto wake mchanga jina la Facebook kama shukurani yake kwa tovuti ya Facebook kwa kusaidia kuwaunganisha Wamisri katika kumung'oa dikteta rais Hosni Mubarak aliyeitawala Misri kwa miaka 30.
  Katika kusherehekea mapinduzi ya kumng'oa rais Hosni Mubarak, baba mmoja nchini Misri ameamua kumpa jina Facebook mtoto wake mchanga.

  Jamal Ibrahim alikuwa miongoni mwa vijana nchini Misri walioshiriki kikamilifu katika kumshinikiza Mubarak aachie ngazi katika mapinduzi makubwa yaliyoanzia januari 25.

  Kwa mujibu wa gazeti la Al-Ahram la nchini Misri, Jamal katika kuishukuru tovuti ya Facebook kwa kuwa chanzo cha kuwaunganisha waandamanaji, aliamua kumwita binti yake Facebook.

  Jina kamili la mtoto wake litakuwa Facebook Jamal Ibrahim na tayari ndugu na jamaa wameanza kukusanyika nyumbani kwa Ibrahim ili kumuona mtoto Facebook.

  Nchini Misri kuna watumiaji wa Facebook milioni tano, idadi ambayo ni kubwa kuliko nchi zote za mashariki ya kati.

  Jumla ya makundi 32,000 yalianzishwa na Wamisri kwenye Facebook wakati wa kipindi cha mapinduzi ya kuuondoa utawala wa rais Mubarak.
   
 2. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Duhh!! hii kali ya mwaka!!
   
 3. k

  kisukari JF-Expert Member

  #3
  Feb 25, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,754
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  mmh,face book.imagine,face book,facebook uko wapi face book.njoo ule face book.beatrice "nipo mwalim",mary "nipo mwalim"face book,mmh.maybe hilo jina litampa umaarufu
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Feb 25, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Me nikijaaliwa, wangu ataitwa "Jamiiforums Katavi"
   
 5. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #5
  Feb 25, 2011
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  ama kweli duniani kuna mambo..
   
 6. Jaluo_Nyeupe

  Jaluo_Nyeupe JF-Expert Member

  #6
  Feb 25, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 2,269
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  hee! Ila ni jina zuri, wangu nikijaaliwa ataitwa MMU
   
 7. Outlier

  Outlier JF-Expert Member

  #7
  Feb 25, 2011
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  teh teh teh,
  kiarabu itakuwa fersibuki labda kwa hiyo ni bomba tu,
   
 8. P

  PSYCHOLOGY Senior Member

  #8
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 177
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamii members hatari tupu!
  Ha ha ha ha ha !!!
   
 9. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #9
  Feb 26, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,719
  Likes Received: 1,628
  Trophy Points: 280
  na hapa atakayelianzisha tutamuita "sura kitabu" ndilo litakuwa la mtanzania wa kwanza kuwaunganisha wapigania uhuru
   
Loading...