ram
Platinum Member
- Oct 5, 2007
- 9,385
- 8,648
Ni huruma za Bwana kwamba hatuangamii, kwa kuwa rehema zake hazikomi
Ni mpya kila siku asubuhi, uaminifu wako ni mkuu
Bwana ndiye fungu langu, husema nafsi yangu, kwahiyo nitamtumaini yeye.
Maombolezo 3:22-24
Wapendwa wana JF, Mungu wetu ni mwema sana, yeye hutoa kwa majira na nyakati, naye hutwaa kwa majira na nyakati atakapo yeye, hatuna budi kumshukuru Mungu kwa yote anayotufanyia katika maisha yetu. Nimekuja hapa kuwashukuru ninyi nyote mlioneshwa kuguswa na misiba iliyonipata within two weeks, katika hali ya kibinadamu ni ngumu lakini kwa kuwa Mungu wetu ni mwena yatupasa tushukuru kwa yote.
Ninawashukuru sana kwa faraja miliyonipa ktk kipindi chote cha msiba, faraja zenu zilinitia moyo na kunipa nguvu hata nikajiona siko peke yangu katika matatizo haya, narudia kusema tena kwangu JF ni zaidi ya mtandao wa kijamii. Mungu awabariki wote mlionisaidia kwa hali na mali wakati wa matatizo haya.
Kipekee nikushukuru sana charminglady, Mungu akubariki mamii, umekuwa nami kwa kipindi chote cha matatizo haya, ahsante kwa kuleta taarifa hizi hapa Mungu akubariki sana sana, sina cha kukulipa ila Mungu atafanya kitu kwako
Ahsante wote wote na Mungu awabariki sana sana
Pamoja sanaa....!!!!

Last edited by a moderator: