ameline
JF-Expert Member
- Jan 8, 2013
- 2,292
- 1,152
Nawashukuru wale woote wanaoniunga mkono katika kusaidia vijana ambao hawana ajira ili waweze kujitambua kwa kutafuta mbinu mbadala mbalimbali ambazo zitawasaidia kujikwamua katika hali ngumu ya maisha achilia mbali degree zao au elimu zao ambazo wanazo. Baada ya kupost ile thread iliyosomeka " ushauri kwa vijana ambao wanatafuta ajira" nimepokea email nying sana kwa vijana ambao walionesha nia ya dhat katika kujikomboa kifikra mpaka sasa nimefanikiwa kuwasaidia vijana wawili 1mdada, na mwingine mkaka. ilikua hivi;baada ya kuchat nao kwa muda sana niliona ni kweli wana maanisha mmoja ametokea mwanga kilimanjaro na mwingine ametokea hapahapa arusha. mdada anafanya kazi katika sheli ya panone hapa arusha shahara 95,800/= anapewa chakula na mkaka anasimamia store yaan storekeeper katika kampuni inayoitwa arusha sundries mshahara ni 150,000/= anapewa nauli chakula ni yeye hapa arusha.mdada nimemdhamini anaishi kwangu kwa miez 3, mkaka yupo kwa uncle wake. wote wana degree, nimewaomba waje huku jf wawashuhudie members wengine ili wayaamini haya. otherwise, natoa shukrani zangu za dhati kwa kuniamini na kuniunga mkono katika harakati za kupigana na maisha hasa hili suala la kuweka degree chini na kufanya kile unachoona ni sahihi kwako bila kuchagua ili mradi kiwe halali..naomba tuendelee kushirikiana kwa hili, nawaombea hawa waliojitoa kwa moyo kufanya kazi hizi, nawaombea kila la kheri Mungu awajaalie uhai na maisha marefu ili waje kuwa ushuhuda kama mimi.kile mnachoona kinawasaidia kichukueni ila kile kisichofaa kinachopotosha achaneni nacho hasa mawazo ya watu wanaokatisha tamaa.Mungu awabariki woote, pamoja sana. amelinechao@gmail.com