Shukrani wanAa JF.

MESTOD

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
4,798
2,003
Mwezi March nilitoa thread yangu iliyokuwa na kichwa cha habari, 'Kama ni ndoto mbona haiishi?'. Baada ya kutoa thread ile nilipata faraja sana na ushauri wenu ulinipa nguvu mpaka sasa ninaishi, kwani niliishaanza kukata tamaa ya maisha.

Ndg zangu nimezingatia sana ushauri wenu hasa wale mlionipa kupitia PM, na namuomba Mungu awazidishie hekima na muwashauri wengine pia. Sasa imekuwa kama kawaida kwangu japo ile imebaki kuwa ni ndoto isioisha.

Mwisho kwa yeyote mwenye tatizo, hili ni jungu kuu lisilokosa ukoko. Ukiomba ushauri tegemea yote, chukua lifaalo.

Naomba nisimtaje mmoja mmoja ila wote naomba mpokee shukrani zangu. Nawapenda sana wana JF. AHSANTENI SANA.
 
Mestod cause ni Member pia, i believe utapokea post yangu hata kama sikuhusika moja kwa moja na thread yako. I am just proud kua umetoa fidbak kuhusiana na tatizo lako na wachache wanafanya hivyo... Hongera kwa kupata unafuu na I sincerely wish you all the best.

And Mestod leo ni Mothers day... Please tell some deserving woman kua she is a good mom... hata kama ni mmoja.
 
Dah umenikumbusha machungu ya ile thread Baby take it easy bana yatakwisha usijali
 
Asante kwa kutambua michango ya wana JF,
pia hongera kwa kupungukiwa na tatizo lililokuwa linakusumbua.
 
Mestod cause ni Member pia, i believe utapokea post yangu hata kama sikuhusika moja kwa moja na thread yako. I am just proud kua umetoa fidbak kuhusiana na tatizo lako na wachache wanafanya hivyo... Hongera kwa kupata unafuu na I sincerely wish you all the best.

And Mestod leo ni Mothers day... Please tell some deserving woman kua she is a good mom... hata kama ni mmoja.

Nawashimu sana akina mama, dunia ipo hapa ilipo sababu ya mabega yao. Hakuna cha kulinganisha na ndo maana kila mtu apatapo tatizo huitia jina la mama.
 
Back
Top Bottom