Shujaa kijana ws Kirusi (RUSSIA)


KakaKiiza

KakaKiiza

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2010
Messages
10,717
Likes
2,647
Points
280
KakaKiiza

KakaKiiza

JF-Expert Member
Joined Feb 16, 2010
10,717 2,647 280
Mjue SHUJAA KIJANA WA URUSI WA MWAKA 2016 KATIKA MAPIGANO YA SYRIA - ALEXANDER ALEXANDROVICH PROKHORENKO

Alexander Alexandrovich Prokhorenko ni kijana mdogo aliyekuwa Komandoo katika Kikosi cha Kazi Maalum cha Jeshi la Urusi kiitwacho SPETSNAZ akiwa na cheo cha Luteni Mwandamizi (Senior Lieutenant). Alizaliwa tarehe 22 Juni 1990 katika kijiji cha Gorodki, Orenburg Oblast, nchini Urusi au Russia. Alihitimu masomo yake katika Skuli ya Uhandisi ya Ulinzi wa Makombora ya Ndege na katika Chuo cha Ulinzi wa Anga cha Smolensk nchini Urusi. Ndo kwanza alikuwa ameoa na mkewe alikuwa ndo kwanza anatarajiwa kujifungua muda si mrefu.

Alexander Alexandrovich Prokhorenko alikuwa miongoni mwa Makomandoo wa Kikosi cha Spetsnaz waliopelekwa nchini Syria kuisadia serikali ya Rais Bashar Al Assad katika mapigano dhidi ya kundi la ISIS. Alikuwa ni miongozi wa wanajeshi waliopelekwa kuuhami mji wa kihistoria wa Palmyira dhidi ya kundi hilo la ISIS.

Siku ya tarehe 17 Machi, 2016, kijana huyu akiwa katika jukumu lake zito la kukusanya taarifa muhimu za kijeshi zilizolenga kuwabaini wapiganaji wa ISIS mahali walipo na silaha zao na kisha kuzituma taarifa hizo kwa marubani wa ndege za kivita wa Urusi kwa ajili ya kuendesha mashambulizi ya anga yenye kupiga malengo vizuri, alijikuta amezingirwa na wapiganaji katili wa kundi la ISIS baada ya kumng'amua. Kama ilivyo mila na desturi kwa askari aliyefunzwa vyema na akafunzika, hasa komandoo, ni haramu na aibu kubwa kwa askari kuangukia mikononi mwa adui yake akiwa hai kwani anampa adui faida ya kumfanya atakavyo na kumsaidia kupata taarifa za jeshi lake iwapo atazidiwa na mateso atakayopewa na adui yake huyo.

Kwa kulielewa vyema hilo, Alexander Prokhorenko, baada ya kubaini kwamba alikuwa katikati ya wapiganaji wa kundi la ISIS na hakuwa na namna nyingine ya kufanya, aliamuru ashambuliwe kwa kombora na jeshi lake la anga na jeshi lilifanya hivyo mara moja na yeye kupoteza maisha akiwa kazini.

Kwa kushirikiana na vikosi vya Kikurd, jeshi la Urusi liliweza kuupata mwili wake na kuusafirisha kwenda Urusi ambapo uliwasili Moscow tarehe 29 Aprili, 2016. Mazishi yenye heshima zote yalifanyika nyumbani kwao katika kijiji cha Gorodki tarehe 6 Mei 2016.
Tarehe 11 Aprili, 2016, Rais Vladimir Putin alimtangaza Alexander Prokhorenko kuwa Shujaa wa Shirikisho la Urusi, ambayo ni Heshima ya Juu zaidi nchini humo.

Huyu ndiye Alexander Alexandrovich Prokhorenko, ameacha mke mjazito. Pumzika kwa Amani Shujaa Kijana!!
84600bb9141226c26979e0e9de292008.jpg
8197b85e26698cc96ec6c889e913f340.jpg
2815115fcc80f2c58f6a46a621fdc1b7.jpg
7232ae0ee38962d94624847f38957537.jpg
 
Heller

Heller

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2013
Messages
2,369
Likes
5,062
Points
280
Heller

Heller

JF-Expert Member
Joined Dec 17, 2013
2,369 5,062 280
kudadadeki...kombora live.! kweli Komandoo..

Rest In Peace
 
bily

bily

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2012
Messages
8,052
Likes
4,100
Points
280
bily

bily

JF-Expert Member
Joined Apr 5, 2012
8,052 4,100 280
A real patriotic . Rest in peace
 
MNYAMAKAZI

MNYAMAKAZI

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2014
Messages
2,141
Likes
2,081
Points
280
MNYAMAKAZI

MNYAMAKAZI

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2014
2,141 2,081 280
Bw mdogo kabisa. Msiseme uzalendo hatuna, uzalendo unajengwa kwa gharama kubwa. Huku kwetu nani yuko tayari kwenda kufia nchi kati ya watoto wa vigogo waliojazana jeshini? Wanakwenda kama fursa ya ajira ikizingatiwa hatuna choko choko nyingi za kuhatarisha maisha yao.
 
S

Sangomwile

JF-Expert Member
Joined
Aug 17, 2012
Messages
3,084
Likes
158
Points
160
S

Sangomwile

JF-Expert Member
Joined Aug 17, 2012
3,084 158 160
Asante mkuu,lakini jana mkuu figganigga mzee wa mia! aliileta hii habari humu JF.
 
Kete Ngumu

Kete Ngumu

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2014
Messages
5,046
Likes
3,827
Points
280
Age
28
Kete Ngumu

Kete Ngumu

JF-Expert Member
Joined Nov 21, 2014
5,046 3,827 280
Unaweza kutenda ushujaa kama huo kwa Taifa linalojali utawala wa kikatiba kisheria na demokrasia, hata ukifa kitakachofuata kwa heshima kitaifaa familia yako kwa haki, vinginevyo ni ujinga kukubali kifo wengine wabaki wanatumbua dunia.
 
kisu cha ngariba

kisu cha ngariba

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2016
Messages
22,201
Likes
47,981
Points
280
kisu cha ngariba

kisu cha ngariba

JF-Expert Member
Joined Jun 21, 2016
22,201 47,981 280
R.I.P komando
 
Z

zinj

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2013
Messages
863
Likes
400
Points
80
Z

zinj

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2013
863 400 80
Wa Tz. Hivyo ndivyo tulivyokuwa kwenye miaka ya 60;70 na 80. Lakini sijui kwa nini tumebadilika ghafla na kukosa uzalendo.

Hata hao wazee wetu nao wamebadilika kwa kutokuwa na msimamo hadi kupelekea kuhama vyama. Ni vyema wa Tz. tungejitambua.

R.I.P Kijana wa Komsomol.
 

Forum statistics

Threads 1,237,251
Members 475,501
Posts 29,282,699