Shughuli za maendeleo zitakazofanyika Septemba 1 ni zipi?

Massenberg

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
1,173
1,370
Karibu nchi nzima inasubiri Operation UKUTA ambayo imepangwa kufanyika tarehe 1 mwezi ujao, yaani Septemba. Vitisho karibu vyote ambavyo vimetolewa na mabwana wakubwa kwa nyadhifa zao mbalimbali vimejijenga katika hoja kwamba siku hiyo wananchi wasishiriki harakati hizo na badala yake wajikite katika kufanya shughuli za maendeleo.
Swali kubwa ni kwamba ikiwa leo hii ambayo siyo Septemba 1 sehemu nyingi nchini ajira zimepotea na biashara zinafilisika na kufungwa kutokana na mfumo mpya wa uchumi wa awamu ya tano, kazi zipi hizo zitakuwa zikifanyika siku hiyo tofauti na hali ya leo?
Watu kwa maelfu wanakumbana na hali ngumu bila kuwa na vipato lakini hapo hapo wanaambiwa walizoea vya bure kitu ambacho hakina ukweli thabiti.
Nafahamu watakuja watu humu na kusema wengi walizoea kupata hela kwa ubadhirifu na ufisadi, ni kweli lakini yote hayo ni matokeo ya mfumo wa uchumi uliokuzwa na kuendeshwa kibadhirifu na kifisadi chini ya serikali zilizokuwa na mizizi hiyo.
Huu mwaka ungetumika kuurasimisha uchumi wetu kwanza, kuweka mfumo rasmi ya kodi na shughuli zote za kiuchumi halafu kubana mambo ndiyo kufuate kuanzia mwakani hapo naamini wengi wasingeumia kiasi hiki.
Kwa hiyo basi kama ambavyo leo watu hawana kazi za kufanya za maendeleo, ifikapo Septemba 1 bado watakuwa hawana kazi pia ndiyo maana wapo watakaoshiriki harakati za siku hiyo.
 
Ni swala la muda tu haya yanayoonekana kuwasumbua wananchi kwa sasa yatakua sawa hata awamu iliyopita kulikua na uhaba wa ajira pia,kama Serikali imeamua kudhibiti mapato yake tofauti na hapo nyuma ili yatumike kama ilivyokusudiwa na kusababisha hali iliyopo sasa unayoilalamikia ina maana kua kuna mabadilko na bila kubadilika hatuwezi kutoka hapa tulipo na kuelekea kwenye hali bora zaidi.Maumivu yapo lkn yanasababishwa na mchakato wa kuyaondoa ili yasiwepo tena siku za usoni.
 
Back
Top Bottom