Shugga Mama anataka Gari yake irudi haraka

:D :D we jamaa umemshauri vibaya mwenzio
huko ni kumsagia kunguni indirect
rudisheni ilo gari mkae kwa amani hapo mtaani
 
Wakuu mambo vipi?

Na rafiki yangu tunapiga kazi sehem moja sasa alibahatika kupata mpenzi ni mama wa miaka42 hivi, huyu mama ni anapesa sana ana biashara zake kibao znamwingizia pesa bado anafanyia kazi campun kubwa sana hapa DSM.

Walianza mapenzi toka august mapenz yakawa moto, mama amedata kwa jamaaa, hapo mama alisema hana mme ila anawatoto 3. Jamaa angu nae alikuwa amekolea tayr kwa penzi la mama hakutaka kumchunguza san huyu mama, japo nilimsisitiza sana awe makini na pia sikutaka kuingilia mambo ya watu.

October mama akamnunulia jamaa ndinga NISSAN DUALIS kali kabisa, jamaa akawa anaenda kwa mama analala na mama sometime anaenda lala kwa jamaa, siku jamaa aloshtuka alikua kwa mama kama kawaida usiku akasikia gate linafunguliwa akaingia mzee mzma wa makamo akasalimia akaunga chumbani, jamaa anasema alipigwa na butwaa alihisi yule ni mme wake tu. Alimwuliza mama akakubali ni mme wake eti walichana amekuja salimia watoto.

Jamaa baada ya kujua yule ni mke wa mtu akaamua kujitenga taratibu, hapo mama mapenzi ndo yamekolea haelewi kitu. Jamaa akafanikiwa kuwa nae mbali kimtindo akipiga cm hapokei nk. Yule mama akamind akatuma txt kwamba jamaa arudishe gari yake haraka.

Jamaa akanichek akanichana situation yote aktaka nimpe ideas kuhusu hii ishu, nikamwuliza gari umesajili kwa tin ya nan? Ya yule mama au yako? Akasema tin yake nikamwambia imeisha hio gari ni mali yako cha msingi hama hapo ulipokua unakaa then na gari tafuta sehem ifungie kwa muda. Manake hii ndinga tunavimbia nayo sana mtaani hadi batani

Wakuu mnasemaje kuhusu ushauri nilompa??
Kwani gari bei gani? Mbona Vijana mnapenda ubwete
 
Muebrainia Halisi Rudisha Dualis ya watu

Hapa ndio JF inapokua Konyo
 
Back
Top Bottom