Kipala
JF-Expert Member
- Jan 10, 2009
- 3,763
- 700
Wakuu nimetafakari neno hili "shubiri". Tunaikuta katika sentensi kama "Ametia tone la shubiri katika sukari", au "mapenzi ni asali lakini ni pia shubiri".
Hapo "shubiri" linataja ladha chungu (ing. bitter). Asili ni ladha ya mmea mshubiri au aloevera. Ila tu inaonekana wengine hutumia pia "shubiri" badala ya "mshubiri".
Lakini tofauti na maana hii kuna pia matumizi ya "shubiri" kwa ajili ya kipimo cha urefu yaani umbali kati ya kidole gumba na kidole cha mwisho kama hapa chini kwenye picha. Napenda kuuliza kama kipimo hiki bado kinajulikana kwa watu wengi au kama kimeshasahauliwa?