Show za Magari Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Show za Magari Dar

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Buswelu, May 23, 2011.

 1. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #1
  May 23, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Hello Wakuu JF

  Mie sitaki kuhangaika na kuagiza gari toka Japan nataka kununua hapo hapo dar.Niko na Choice tatu tofauti za gari nazotaka...Kuna Toyota Volts,Toyota Harrier,Toyota Kluger.

  But first ni Kluger nikosa ndio ntachukua zingine.Swali langu ni kwamba dar kuna show room kibao kama utitiri na kila mwenye nayo anatoa japan.Kama kuna mwenyeji anaye jua ni show room gani wanaleta gari zilizoko kwenye hali nzuri.....zinatoka sana so siwezi pata gari zilizo kaa muda mrefu...na kama kuna ushauri mwingine regarding kununua gari Dar Es Salaam utanisaidia sana.

  Regards
  Buswelu
   
 2. S

  Speedo Member

  #2
  May 23, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 13
  Kutaja uende wapi ni kutangaza biashara ya mtu bila malipo. Kila mmoja anaweza kutaja nzuri ni ipi kutokana na yeye alivyohudumiwa na hali ya gari aliyoipata. Naamini unaulizia magari ya mtumba ambayo hata wauzaji wengi wanayauza bila kuyafahamu vizuri na hata pale wanapofahamu udhaifu wa gari husika huwa hawasemi ukinunua ukagundue wewe.
  Kila muuzaji akikupa sifa za gari analouza utaona kila mmoja anauza gari zuri. Yote ni biashara na lengo ni faida.
  Nikikupa reference mimi ya gari nililonunua showroom A mwaka 2005 haitakusaidia leo.

  Wengi tunatafuta nani anauza bei nafuu sio nani anauza gari zuri. Wapo wauzaji wengi wasio na showrooms, huwa wanaagiza gari wanasajili kisha wanauza. Mara nyingi huwa bei zao ni nafuu kuliko wenye showrooms kwa kuwa hawana kodi ya pango wala walinzi wakuwalipa.
   
 3. Jaramba

  Jaramba Member

  #3
  May 24, 2011
  Joined: Oct 27, 2008
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Nakushauri usijisumbue kununua gari kwenye Show Room za Bongo (DSM).

  Nilishauriwa kama ninavyokushauri ila sikusikia,kilichonipata sitokuja kusahau.

  Miaka kadhaa iliyopita nilinunua gari kwenye show room ya "MAZRUI" pale nyuma ya Break Point - Kijitonyama,nilifanya malipo yote kama tulivyokubaliana na wakaniahidi watamaliza ishu za TRA (Usajili+Kubadilisha umiliki etc) ndani ya wiki moja but ilichukua miezi mitatu mpaka nilipokuja kupata kadi ya gari,plate number etc, tena baada ya kuwapelekea samansi ya kuwaita Mahakamani.

  Kwa muda huo wa miezi 3 unakuwa umeshaagiza gari from Dubai/Japan or elsewhere na inakuwa ishafika Bongo na utakuwa unaitumia.
  Kipindi chote hicho nilipokuwa nasubiri niliwaomba documents za ile gari hasa za ukaguzi kule Japan (JAAI) but sikupewa kila siku walikuwa wananizungusha,nilikuja kupata hizo docoments pamoja na gari,kuzichunguza nikabaki nimeduwaa,gari ilikaguliwa Japan mwezi April 2007 ikiwa na 132,000 Kms!But wakati nafanya manunuzi kigezo kimoja wapo kilikuwa ni idadi ya Kms ilizotembea na Odometer ilikuwa inasoma 80,000 Kms !So walicheza na Odometer.

  Tulifikishana kwenye vyombo vya sheria ili wanirudishie pesa yangu na wachukue gari yao but kama ujuavyo mfumo wetu wa sheria Mwanasheria anataka pesa,Hakimu anataka pesa,Karani wa Mahakama anataka pesa,Polisi anataka pesa etc etc na nikizingatia nimeshasubiri hiyo gari for 3 month nikaamua kusamehe,ki ukweli ilinigharimu sana mpaka kuweza kuiweka katika hali nzuri maana ni aibu.

  So mkuu kama unataka kununua body nzuri,na muonekano just go ahead ila kama unataka kupata gari zuri na la uhakika bila longolongo nakushauri agiza.

  Najua kuna wafanyabiashara wachache ni waaminifu ila wengi wao ni wasanii na wanafanya biashara za ujanja ujanja.

  Nawasilisha.
   
 4. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,652
  Trophy Points: 280
  Kaka achana na Kluger bora uchuku hito voltz au RAV4
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,495
  Trophy Points: 280
  pole sana kaka
   
 6. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Hapo ndo huwa wananiacha hoi hawa wanaojiita wafanya biashara! Pole mkuu!
   
 7. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #7
  May 24, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kwanini Mkuu!!!Maelezo zaidi...Jaramba naona kapitia makuu sana...kwenye swala hili la magari....kuna vitu kavisema hapo inabidi kufanya consideration....sana..hasa documents za ukaguzi Japan...one.then na show room kama zile za break point duu naifahamu hiyo..imekaa kimatata sana.a..
   
 8. s

  sawabho JF-Expert Member

  #8
  May 24, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Jitahidi uagize gari, itakuchukua muda na unatakiwa kuwa makini na unakoagiza, lakini utapata gari ingawa limetumika lakini ni zuri. Wafanya biashara wa Japani hawana tamaa na wanafahamu kuwa akikuuzia gari zuri anajitangaza, kabla ya gari kusafirishwa linafanyiwa ukarabati. Wanakupatia maintenance history. Mimi nilishauriwa hivyo, wakanitumia kimtumba kizuri tu, sina tatizo nacho.
   
 9. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  wauzaji wa magari dar wengi wao sio wakweli, nikama wanakukabidhi bomu, likakulipukie mbele kwa mbele.. but sio wote unaweza bahatika. nimenunua gari tatu hapahapa bongo my 1st and 2nd cars was cool the third one ilikuwa ni mshikemshike! the car was good lakini doccuments zilikuwa hovyo sana imenigharimu 1.5M etra kuweka sawa, so be careful but you can try your lucky
   
 10. Vinci

  Vinci JF-Expert Member

  #10
  May 24, 2011
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 2,642
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Mkuu wewe kama kweli unahitaji gari nzuri ambayo hutokuwa na wasi wasi nayo bora uwe mvumilivu iagize mwenyewe japan. kwanza kule uatachagua gari uipendaye yenye vigezo unavyopenda gari yako iwe nayo. kama rangi, odometer, na vingine vingi. usanii wa hapa bongo ni mwingi bora umvue mtu alieagiza kutoka japan kuliko uende show room. walio wengi wanachakachua magari ili yauzike kwa bei ya juu na haraka. kutoka na aina ya magari unayozungumzia inaonekana umejipanga na una budget nzuri. ukiagiza nje utasave hela nzuri tuu.
   
 11. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #11
  May 24, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mkuu sasa kama Kluger kuagiza mpaka inafika hapa ni 23m....Na show room wanakuuzia 23 hiyo hiyo..bado pale bandarini haujachakachuliwa na wale TRA...Wenye njaa ndio hapo sasa mie sipataki jamani...any agent anaye leta na kuuza ?unaye mfahamu!!
   
Loading...