Should Tanzanians living abroad be allowed to vote?

Should Tanzanians living abroad be allowed to vote?

Utapiga vipi kura wakati hulipi kodi TZ? Nyie mnaojiita WTZ mnaoishi nje ya nchi mnataka kupiga kura bila ya kuchangia kodi. Mnafanya kazi nje ya nchi, hamlipi kodi TZ; lakini mnataka mpewe haki kama WTZ wengine. Kama mnataka kupiga kura lipeni kodi ya kipato mnachoingiza.

Kwa mfano, raia wa USA analipa kodi ya nchi hata kama akifanya kazi nje ya nchi. Sasa kwanini nyinyi hamlipi kodi? Sisi tunaumia huku Bongo na tunalipa kodi; kwa sababu tunataka maendeleo ya Taifa letu. Naliomba Bunge lichukue hatua kali dhidi ya watu wanaoishi nje ya nchi wanaotaka kupiga kura bila ya kulipa kodi. Inaumiza sana kuona WTZ wanaoishi nje ya nchi hawalipi kodi; lakini wanapewa haki kama raia wengine ambao wanalipa kodi. Tunaomba Bunge lipitishe Muswaada kuhusu haki za wanaolipa kodi na wasiolipa kodi.

Kama hulipi kodi pia FISADI. Kwa hiyo hawa wanaojiita WTZ wanaoishi nje ya nchi ni MAFISADI pia.
Hujasema kuwa ni kodi ipi inayotakiwa kulipwa Tanzania ili iwe kigezo cha kumuwezesha mtu kupiga kura. Mimi naishi nje ya Tanzania, lakini nalipa kodi nchini Tanzania kila mwaka.

Ninalipa kodi za viwanja na majengo yangu mbalimbali, pamoja na magari yangu ambayo yapo barabarani. Sasa utaniambia nini, kuwa silipi kodi? Ee bwana we, wacha mchezo!!
 
Dhana ya kodi ya mapato inatokana na kwamba serikali inakuhudumia. na ndo maana unaona watu wanatishia kutolipa kodi serikali ikishindwa kutoa huduma. Bahati mbaya serikali ya tanzania haiwahudumii watu wake nje ya nchi. watu wanajihudumia wenyewe tu. kwaiyo hawapaswi kulipa kodi. lakini kikatiba hawazuiwi kupiga kura. Tanzania siyo zanzibar wanaotaka kitu kinachoitwa kitambulisho cha mkazi
 
Aksanteni wote kwa majibu mazuri Zakumi,August,Ngambo Ngali,Pundamilia07,Arsene wenger and wadela wa Madilu...Nina shukuru sana maana nilikuwa nauliza ili kupata kujua maana wenzetu utaona wakati wa kupiga kura hata kama wako nje ya nchi kula yao inahesabika ndiyo nikauliza kama na nchi yetu inatoa kigezo hiko....

thanks!!!!!
 
Utapiga vipi kura wakati hulipi kodi TZ? Nyie mnaojiita WTZ mnaoishi nje ya nchi mnataka kupiga kura bila ya kuchangia kodi. Mnafanya kazi nje ya nchi, hamlipi kodi TZ; lakini mnataka mpewe haki kama WTZ wengine. Kama mnataka kupiga kura lipeni kodi ya kipato mnachoingiza. Kwa mfano, raia wa USA analipa kodi ya nchi hata kama akifanya kazi nje ya nchi. Sasa kwanini nyinyi hamlipi kodi? Sisi tunaumia huku Bongo na tunalipa kodi; kwa sababu tunataka maendeleo ya Taifa letu. Naliomba Bunge lichukue hatua kali dhidi ya watu wanaoishi nje ya nchi wanaotaka kupiga kura bila ya kulipa kodi. Inaumiza sana kuona WTZ wanaoishi nje ya nchi hawalipi kodi wanapewa haki kama raia wengine ambao wanalipa kodi. Tunaomba Bunge ipitishe Muswaada kuhusu haki za wanaolipa kodi na wasiolipa kodi.
kuna njia nyingi za kuchangia maendeleo na mojawapo ni Remittances
 
Japokuwa sina takwimu, lakini inaonesha watanzania wenye makazi ya kudumu nje ya nchi ni wengi ukilinganisaha na wale walioko masomoni au wanafanya kazi kwa muda maalum then watarejea nyumbani. Kwa mantiki hiyo basi nadhani suala la kupiga kura liachwe kwa wale waliopo ndani ya Tanzania wachague viongozi wanaotaka wawaongoze. Akina sie ambao tunakaa na kuishi ughaibuni tusiwachagulie waliondani waongozwe na nani.
Punda,
Una address wale watanzania walio nje au wapinzani walio nje?
Mtanzania aliye nje kwa sababu yoyote ile hana haki za kitanzania.

"suala la kupiga kura liachwe kwa wale waliopo ndani ya Tanzania wachague viongozi wanaotaka wawaongoze." na "tusiwachagulie waliondani waongozwe na nani."

ina maana gani? Hawa unao waondoa kwenye kundi la watanzania wakiwa huko nje rais wao ni nani?

Naona sijaona hoja kwenye hoja yako hiyo!
 
Sheria ya kupiga kura haitumii kodi ya mapato kama sifa ya kupiga kura; kuna watu wenye kipato cha chini kisichotozwa kodi ya mapato ambao wanapiga kura. Sifa pekee ya kupiga kura ni kuwa na umri usipongua miaka kumi na nane, kuwa na akili timamu, kutokuwa mfungwa, na kuwa umejiandikisha katika daftari la wapiga kura. Nina imani kuwa kitendo cha serikali kushindwa kuweka utaratibu wa kuandikisha watanzania walioko nje ili wapige kura zao ni kuwakoshesha watanzania hao haki yao ya kikatiba.

Mkuu Kichuguu kama ulivyoandika hapo awali,Sifa za kupiga kura ni Umri wa miaka 18 & +,Uraia wa Tanzania na Akili Timamu....Kwa Watanzania wengi walio nje ya Nchi inakuwa vigumu kwao kupiga kura,kwa sababu hawapo kwenye Daftari la Wapiga kura.......Lakini siku za karibuni Balozi nyingi za Nje za Tanzania ikiwa pamoja na USA & UK ( kwenye Watanzania wengi), wameanzisha Utaratibu wa Watanzania kujiandikisha katika Balozi zao,Ikiwa Mpango huu utafanikiwa si siku nyingi Watanzania tutaanza kupiga kura hata kama tunaishi Nje ya mipaka ya Tanzania.
 
Tanzania kuna kodi nyingi sana, inawezekana kweli watanzania walioko nchi za nje hawalipi kodi ya mapato na kodi ya VAT, lakini kuna watu wengi sana wallioko nje ya nchi wanalipa kodi za viwanja vya nyumba zao zilizoko Tanzania, kodi za magari yao yaliyoko Tanzania na kodi nyinginezo. Nadhani umetumia dhana potofu ya odi kudhani kuwa kodi ni ya mapato tu, na vile vile kudhani kuwa watanzania wanaoishi nchi za nje hawana mali zinazotozwa kodi Tanzania.

Kodi yenye kuumiza na yenye machungu sana ni Income tax; ambayo WTZ wengi waliopo nje hawalipi. Najua kwamba hakuna sheria inayowakataza WTZ waliopo nje kupiga kura, ndiyo maana nimeliomba Bunge liangalie upya sheria na haki za MTZ aliyopo TZ na asiyepo TZ. Kwa mfano, Kikwete alishawahi kusema kwamba nyinyi mliopo nje "mnataka kula kotekote". Sasa hivi kodi ya Wafanyakazi ni kubwa; kwa sababu wapo wafanyakazi wachache wanaolipa kodi. Kama nyinyi mliopo nje ya TZ, mngekuwa mnalipa Income tax, mzigo ungepungua kwa Wafanyakazi waliopo TZ. Tunaliomba Bunge la Jamhuri wa Muungano lipitishe muswaada utakaofanya nyinyi mnaotaka "kula kotekote" muanze kulipa kodi, ili mapte haki ya kuwa WTZ kamili. Kumbuka, kulipa kodi si adhabu; bali ni kusaidia kujenga uchumi wetu.Tujitolee kujenga hili Taifa letu zuri. God bless you all, and God bless Tanzania.
 
Ok mnavyosema kuwa watanzania nje ya nchi hawatambuliko katika daftari la wapiga kura....so what is the point ya kuanzisha matawi ya chama nje ya nchi? au kuwa na balozi nje ya nchi si balozi zinawakilisha tanzania nje ya nchi na watanzania wake? unless i am wrong.

Kama London wameanzisha TAWI LA CCM na hivi karibuni pia marekani wameshafungua tawi la CCM na katibu wake i think ni Zainabu janguo.Kuanzisha tawi la ccm si maana yake kuwa na watanzania nje ya nchi wanatambulika? correct me if i am wrong.
 
Dadangu Kelly01:

Huko sahihi kabisa. Ubalozi wa Tanzania uliopo Marekani au nchi nyingine ni sehemu ya Tanzania. Hivyo kwa hoja zako ofisi hizi zilitakiwa kuwa na madaftari ya kujiandikisha wapiga kura kwa sababu ni sehemu ya nchi kama vile Chakechake au Mpindimbi.

Anyway sitajiingiza sana kwenye mambo ya nchi nyingine kwa sababu uraia wangu niliukana. Lakini ukweli wa mambo ni kuwa uraia wangu wa Marekani unanipa haki nyingi za kiraia kuliko nilipokuwa raia wa Tanzania kwa sababu katiba ya Marekani inatangulia na Bill of Rights.

Kwa upande wa Tanzania, katiba ya nchi ni framework tu ya jinsi serikali inavyoundwa na kuchaguliwa na hiko nyuma sana kuelezea rights za watanzania.
 
Kodi yenye kuumiza na yenye machungu sana ni Income tax; ambayo WTZ wengi waliopo nje hawalipi. Najua kwamba hakuna sheria inayowakataza WTZ waliopo nje kupiga kura, ndiyo maana nimeliomba Bunge liangalie upya sheria na haki za MTZ aliyopo TZ na asiyepo TZ. Kwa mfano, Kikwete alishawahi kusema kwamba nyinyi mliopo nje "mnataka kula kotekote". Sasa hivi kodi ya Wafanyakazi ni kubwa; kwa sababu wapo wafanyakazi wachache wanaolipa kodi. Kama nyinyi mliopo nje ya TZ, mngekuwa mnalipa Income tax, mzigo ungepungua kwa Wafanyakazi waliopo TZ. Tunaliomba Bunge la Jamhuri wa Muungano lipitishe muswaada utakaofanya nyinyi mnaotaka "kula kotekote" muanze kulipa kodi, ili mapte haki ya kuwa WTZ kamili. Kumbuka, kulipa kodi si adhabu; bali ni kusaidia kujenga uchumi wetu.Tujitolee kujenga hili Taifa letu zuri. God bless you all, and God bless Tanzania.

Kodi hipo kwenye sheria za mapato na sio haki ya raia. Na vilevile umeshaeleza mwenyewe kuwa kodi yenye machungu ni income tax. Income tax inalipwa pale unapopata mapato. Na kutafuta mapato ni chaguo la mtu. Umehamua kufanya kazi yenye kukuletea mapato mengi na ambayo yanaambatana na wewe kulipa kodi. Hilo ni chaguo lako lakini sio haki yako ya kiraia. Unaweza kuacha hiyo kazi na kukaa nyumbani hili usilipe kodi.

Hivyo mwenye mapato mengi analipa kodi nyingi kuliko yule mwenye mapato kidogo. Na ukiingiza sheria za mapato kwenye haki za kiraia basi itafikia kipindi wenye kulipa kodi kubwa watataka kuwa na kura yenye sauti kubwa kuliko masikini. Na mwekezaji kutoka nje anayelipa kodi atadai haki ya kupiga kura.

Na usipokuwa makini itafikia kipindi mgonjwa asiyeweza kufanyakazi na wastaafu watanyimwa haki zao za kupiga kura kwa sababu hawalipi kodi.
 
Anyway sitajiingiza sana kwenye mambo ya nchi nyingine kwa sababu uraia wangu niliukana. Lakini ukweli wa mambo ni kuwa uraia wangu wa Marekani unanipa haki nyingi za kiraia kuliko nilipokuwa raia wa Tanzania kwa sababu katiba ya Marekani inatangulia na Bill of Rights.

Kwa upande wa Tanzania, katiba ya nchi ni framework tu ya jinsi serikali inavyoundwa na kuchaguliwa na hiko nyuma sana kuelezea rights za watanzania.

Zakumi lini utaacha kuudanganya umma? Wajamaa tuliweka 'Bill of Rights' kwenye Katiba yetu mwanzoni mwa miaka ya 80 baada ya mchakato wa kidemokrasia na ikiwa ni miaka michache baada ya kuunda Katiba ya Jamhuri yaTanzania ya mwaka 1977. Toleo lenye Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2005 ambalo lipo hapa mbele yangu linaonesha kuwa iko mbele sana kuelezea haki za Watanzania. Tatizo ni hao walioapa kuitetea Katiba!

P.S. Alafu kuendelea kwako kuungopea umma bila soni/aibu/haya kumenikumbusha posti yako ambayo nimeitafuta sana niijibu ila sijaiona. Nazungumzia ile posti unayosema kina Fanon na Guevarra walisema mambo yaliyokuwa yanaendana na mazingira ya wakati ule na sio sasa. Je, unaweza kusema hilo hilo kuhusu John Maynard Keynes ambaye nadharia zake uchumi ambazo zilionekana kupitwa na wakati ndio sasa zinatumiwa na kina Obama na watu wenye mrengo kama wako kujaribu kutatua zahama la mgogoro wa kiuchumi duniani? Hebu angalia uchambuzi huu kuhusu hilo: http://groups.yahoo.com/group/wanazuoni/message/4432

"Hakuna jambo jipya chini ya jua" - Mfalme Suleimani Mwenye Hekima

Alamsiki!
 
Commandante:

Jaji Nyalali asingetoa mapendekezo ya kubadilisha vipengele vya katiba kama wajamaa mngejua haki. Kwa mfano ni haki ya kiraia ya mtu asiye mwanachama wa chama chochote kugombea nafasi ya uongozi. Lakini ili ugombee nafasi ya uongozi Tanzania ni lazima uwe mwanachama wa kisiasa.

Mimi sidanganyi umma lakini wewe uchoki kuboronga. Nilichosema kuhusu Fanon, Nyerere na Che Guevara ni kuwa solution za matatizo walizokuwa nazo zilikuwa incomplete kwa sababu ya assumptions walizochukua.

Mapinduzi siku zote yanafanywa na watu wenye common enemy na sio common interests. Na ukosefu wa common interests ndio kikwazo kikubwa cha mapinduzi.
 
Zakumi hizo 'dhahania' zao sisi tumeshazikamilisha, sasa zinatekelezeka!

Mkuu kwa kuzingatia mgawanyo wa madaraka kati ya Bunge, Mahakama na Serikali, Mahahakama imeshatoa hukumu kuwa kuwe na Mgombea binafsi. Kama nilivyosema, tatizo ni watu walioapa kuilinda Katiba. Hiyo Katiba pamoja na kuwa na matatizo, inatoa haki.Na kama alivyoulize Mdau mmojawapo humu, kama Katiba yao wenyewe hawailindi je tukiibadili ndio watailinda? Hebu cheki dondoo hizi kutoka kwenye 'Muswada wa Haki' wetu na zingatia maswali ya 'yanayojijibu yenyewe' niliyoyaongezea hapo:

------
Ibara ya 14: Kila mtu anayo Haki ya Kuishi na kupata kutoka katika jamii hifadhi ya maisha yake, kwa mujibu wa sheria.

Je, maalbino wa Tanzania wana haki hiyo? Vibaka wanaochomwa moto je? Na wale waliouliwa kwa mujibu wa kesi ya Zombe na Wenzake kulikoni?

Ibara ya 13 (1): Watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki bila ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria.

Je, Mzee wa Vijisenti ni sawa mbele ya sheria na wale wafugaji waliofunguliwa mashtaka kwa kuchunga kwenye eneo lao wenyewe?

Ibara ya 18(d): Kila mtu anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu masuala muhimu kwa jamii.

Je, Mwanakijiji anapata haki ya kupewa taarifa kuhusu Meremeta na Kiwira?
--------

Kwa sasa tuna adui mmoja, ufisadi, hivyo wakati wa mapinduzi ni huu!
 
By a Correspondent in Nairobi, 4th September 2009

Tanzanias living abroad may start voting in next year’s general elections, it has been learnt. The Prime Minister, Mr Mizengo Pinda, said here on Wednesday that the government was working on modalities to facilitate the move following sustained pleas from overseas-based Tanzanians.

“Relevant authorities are currently working on the matter to see how best it could be undertaken,” said the premier during talks with Tanzanians living in Kenya, held at Laico Regency Hotel in Nairobi.

They asked the government to facilitate their participation in the 2010 General Election, having made a similar call in 2005. Mr Pinda assured them that the government was taking their request seriously, noting that he had received similar appeals from Tanzanians living in the UK earlier this year.

He said he had forwarded the requests to relevant authorities within the ruling party, CCM for action. Some Tanzanians also appealed to the government to build more boarding schools that would accommodate students from all over the country, instead of concentrating on ward secondary schools.

"Ward secondary schools are good, but do not expand horizons of students who are mostly enrolled from villages within a particular area. These students may grow up without the spirit of nationalism," one Tanzanian argued.

Reading the message on behalf of Tanzanians, Ms Slyvia Bankobeza said the construction of the schools was denying the students the opportunity to leave their regions and mix with others to learn new things. "They are left to grow up and live in the same environment throughout their lives," she noted.

"To address this situation, we urge the government to construct more boarding schools so that students from different regions can get the opportunity to study there," she said. Issues of land, identity cards, passports in the East Africa community (EAC), were also raised during the meeting attended by over 200 Tanzanians.

On the issue of land and identity cards, Premier Pinda assured them that the ministries responsible were working out various solutions to problems raised. The PM yesterday visited the Nairobi Stock Exchange and later met President Mwai Kibaki. He also visited co-operative farmers and livestock keepers' society of Limuru and the Karen flower area.

Source: Daily News
 
By a Correspondent in Nairobi, 4th September 2009

Tanzanias living abroad may start voting in next year's general elections, it has been learnt. The Prime Minister, Mr Mizengo Pinda, said here on Wednesday that the government was working on modalities to facilitate the move following sustained pleas from overseas-based Tanzanians.

Sisi tumeomba siku nyingi kuwa na wagombea binafsi katika ubunge, uraisi na udiwani lakini serikali inatuona hayawani, kumbuka sisi ndio tuliowaweka madarakani( kwa kura zetu za ndio na hapana) na sisi ni wengi hivyo priority ingekuwa sisi tunaoomba wagombea binafsi.

Juzi waziri mmoja ameenda gerezani na kusema kuwa sheria ya uchaguzi itabadilishwa ili wafungwa wawe na haki ya kupiga kura, sio kitu kibaya lakini naona cha msingi zaidi ni mgombea binafsi kuliko vitu vyote that should be the priority after which we should proceed with an indepedent and impartial electoral commission.

Ukimpa mtu haki ya kupiga kura ina maana haki ya kugombea lazima apewe in which case wafungwa itabidi waamue kugombea nafasi wakiwa gerezani huku wakiwa chini ya vyama vyao. No wonder tunakuwa na matawi ya vyama london, india , states etc kwa matayarisho hayo hapo juu. Tupeni wagombea binafsi kwanza kwani mnaogopa nini ????
 
Utapiga vipi kura wakati hulipi kodi TZ? Nyie mnaojiita WTZ mnaoishi nje ya nchi mnataka kupiga kura bila ya kuchangia kodi. Mnafanya kazi nje ya nchi, hamlipi kodi TZ; lakini mnataka mpewe haki kama WTZ wengine. Kama mnataka kupiga kura lipeni kodi ya kipato mnachoingiza. Kwa mfano, raia wa USA analipa kodi ya nchi hata kama akifanya kazi nje ya nchi. Sasa kwanini nyinyi hamlipi kodi? Sisi tunaumia huku Bongo na tunalipa kodi; kwa sababu tunataka maendeleo ya Taifa letu. Naliomba Bunge lichukue hatua kali dhidi ya watu wanaoishi nje ya nchi wanaotaka kupiga kura bila ya kulipa kodi. Inaumiza sana kuona WTZ wanaoishi nje ya nchi hawalipi kodi wanapewa haki kama raia wengine ambao wanalipa kodi. Tunaomba Bunge ipitishe Muswaada kuhusu haki za wanaolipa kodi na wasiolipa kodi.

1. Nani kakwambia haki ya uraia inatokana na kodi? Unataka kumnyima mtu haki ya uraia kwa sababu halipi kodi? Na watu wasio na kazi walio Tanzania ambao hawalipi kodi nao utawanyima haki ya kupiga kura? Wewe unaonekana unataka kugeuza "No taxation without representation" kuwa "No representation without taxation" sad indeed.

2. Watu wengi walio nje ya nchi wananchangia uchumi wa Tanzania mara nyingi zaidi ya Watanzania wa average walio nchini, mimi hapa nikituma nyumbani $ 500 mara moja tu - and I do more than that- ninakuwa nishapeleka hela kwenye uchumi wa Tanzania ambazo zinatosha kunilipia kodi ya Mtanzania wa kawaida several times over.

Acha narrowmindedness, chuki na ubaguzi kwa Watanzania wenzako.
 
Last edited:
Jamani hamuoni CCM inafungua avenue nyingine ya kuiba kura. We are not ready to have this privilege. Na ni kwa sababu kwa sasa, serikali na chama = kitu kimoja. Tumeshindwa kabisa ku-separate hivi viwili. Na pili Serikali na Tume ya Uchaguzi = kitu kimoja. Which means, Tume ya Uchaguzi = Chama.
Na hatuwezi kuamishia hii Tume ya Uchaguzi kuwa chini ya Bunge kwa sababu, Bunge = Chama. Na hivyo, Bunge = Serikali. Ndo kiini macho hicho. Deal with it!!

Mmenielewa?
 
Court backs S Africa exile vote​

BBC News Online

Britain has a large South African diaspora community
South Africans living abroad should be allowed to vote, according to a ruling by Pretoria High Court.

The decision could mean a delay to elections, due in April or May, to allow time for the law to be changed.

The court found current laws breached the rights of South Africans living abroad and referred the judgment to the Constitutional Court for confirmation.

The government says it will not comment until it has studied the ruling. Some two million South Africans live abroad.

John Battersby, of the Global South Africans Network in the UK, said that of these, 5-600,000 were in the UK.

"It might be a difficult decision to implement in a short space of time," he told the BBC's Focus on Africa programme.

The court ordered the electoral commission to change its procedures to let South Africans living abroad to vote.

Tight contest

The opposition Afrikaner nationalist Freedom Front Plus party had brought the legal application on behalf of a South African school teacher living in the UK.

Speaking outside the court, party spokesman Willie Spies told Sapa news agency it was still possible the Constitutional Court, the country's highest court, could overrule the judgment.

The party said it was filing an application for the proclamation of election day to be postponed to allow the Constitutional Court ample time to consider the matter.

The date for the elections was expected this week.

Currently certain groups, including government employees and people on holiday and business trips, are entitled to vote while out of the country.

The poll is shaping up to be the most interesting since the end of apartheid in 1994.

African National Congress (ANC) leader Jacob Zuma is the front-runner to become president but his bid has been overshadowed by the corruption charges he is facing.

Bitter divisions in the ruling party recently led to the launch of the breakaway Congress of the People (Cope) party, which could win enough votes to deny the ANC a two-thirds majority to parliament, needed to change the constitution.

The tensions have spilled over into clashes between groups of rival supporters.

Kama kura za wananchi waliopo nchini wanapiga kura halafu zinapotea au hazihesabiwa, itakuwaje kwa kura zinazopigwa nje ya nchi? I am telling you it is one who builds castles in the air - unrealistic!
 
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inaandaa utaratibu ili Watanzania wanaoishi nje ya nchi wapige kura katika uchaguzi Mkuu.

Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji mstaafu Lewis Makame amesema,kila Mtanzania ana haki ya kupiga kura na kumchagua kiongozi anayemtaka.

Jaji Makame amesema, Watanzania wanaoishi nje ya nchi pia wana haki ya kupiga kura kama walivyo Watanzania wengine.

Ameyasema hayo mwishoni mwa wiki mjini Dodoma na akabainisha kwamba, uaandaliwa utaratibu ili wafungwa magerezani wapige kura.

"Sheria inasema kuwa wafungwa wanaoruhusiwa kupiga kura ni wale ambao wamefungwa kifungo cha chini ya miezi sita lakini utaratibu wa kuwaandikisha wakiwa gerezani ndiyo tatizo", amesema Jaji Makame

Amesema kuwa bado maandalizi ya kuandikisha watu walioko magerezani hususan wale waliofungwa kifungo cha chini ya miezi sita hayajakamilika kutokana na unyeti wa suala hilo.

Jaji makame amesema, NEC bado inaangalia suala hilo kwa kuwa uandikishaji wa wafungwa unajumuisha na mahabusu

Source: http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=3668
 
Back
Top Bottom