Should Tanzanians living abroad be allowed to vote? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Should Tanzanians living abroad be allowed to vote?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Feb 10, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,681
  Likes Received: 82,533
  Trophy Points: 280
  Court backs S Africa exile vote

  BBC News Online

  Britain has a large South African diaspora community
  South Africans living abroad should be allowed to vote, according to a ruling by Pretoria High Court.

  The decision could mean a delay to elections, due in April or May, to allow time for the law to be changed.

  The court found current laws breached the rights of South Africans living abroad and referred the judgment to the Constitutional Court for confirmation.

  The government says it will not comment until it has studied the ruling. Some two million South Africans live abroad.

  John Battersby, of the Global South Africans Network in the UK, said that of these, 5-600,000 were in the UK.

  "It might be a difficult decision to implement in a short space of time," he told the BBC's Focus on Africa programme.

  The court ordered the electoral commission to change its procedures to let South Africans living abroad to vote.

  Tight contest

  The opposition Afrikaner nationalist Freedom Front Plus party had brought the legal application on behalf of a South African school teacher living in the UK.

  Speaking outside the court, party spokesman Willie Spies told Sapa news agency it was still possible the Constitutional Court, the country's highest court, could overrule the judgment.

  The party said it was filing an application for the proclamation of election day to be postponed to allow the Constitutional Court ample time to consider the matter.

  The date for the elections was expected this week.

  Currently certain groups, including government employees and people on holiday and business trips, are entitled to vote while out of the country.

  The poll is shaping up to be the most interesting since the end of apartheid in 1994.

  African National Congress (ANC) leader Jacob Zuma is the front-runner to become president but his bid has been overshadowed by the corruption charges he is facing.

  Bitter divisions in the ruling party recently led to the launch of the breakaway Congress of the People (Cope) party, which could win enough votes to deny the ANC a two-thirds majority to parliament, needed to change the constitution.

  The tensions have spilled over into clashes between groups of rival supporters.
   
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Hivi Watz wanaishi nje ya nchi wapo wangapi?

  Je ni pro-CCM au Upinzani wa CHADEMA au CUF?
   
 3. Giro

  Giro JF-Expert Member

  #3
  Feb 10, 2009
  Joined: Feb 9, 2009
  Messages: 360
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  kwa mtazamo wangu,vizuri wakaruhusiwa kwa sababu ni haki yao kikatiba,but the only problem ambayo mimi naiona ni mchakato mzima wa upigaji kura na kuhesabiwa kwakwe coz hatuna system maana ya system ya kuzi collect,za hapa hapa bongo tu jamaa wanapiga magumashi je hizo si itakuwa balaa tupu,tatizo jingine hakuna system ambayo tutaweza ku confirm je kweli aliye piga kura ni mbongo au la coz hatuna idadi kamili(majina) ya wa wabongo waliopo abroad siunajua mzee some of them wakifika mtoni wana badilisha na majina na uraia pia na sisi hatuna system ya uraia wa inchi zaidi ya moja.But kama tuta advance tukawa na such a system itakuwa vizuri jamaa nao waka piga kura.
   
 4. g

  geek Member

  #4
  May 14, 2009
  Joined: Feb 12, 2009
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna taarifa zinazoenea katika duru za kisiasa na kidiplomasia kwamba watanzania walio nje ya nchi karibu wataruhusiwa kupiga kura baada ya mabadiliko ya sheria yatakayofanyiwa kazi hivi karibuni.

  Kasi ya kufunguliwa kwa mashina na matawi ya Chama cha Mapinduzi [CCM] nje ya imeelezwa kuwa ni "maandalizi" ya kupitisha sheria itakayoruhusu raia wa Tanzania aliye nje kuchagua viongozi walioko Tanzania.

  Inaelezwa kuwa ili chama tawala [CCM] kisiumie kwa hatua hiyo, imebidi matawi yafunguliwe ili kuhamasisha watu kukipigia kura.

  Hizi ni tetesi kama zilivyo tetesi, lakini tetesi ngapi zimegeuka kuwa facts. Haya wanachama wa CCM mlio nje mnajua sababu ya matawi kufunguliwa nje ya Tanzania? Na je kwa wale wasiounga mkono CCM mnatambua kwamba kwa strategy jamaa wako mbele hatua moja?.......
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  May 14, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,681
  Likes Received: 82,533
  Trophy Points: 280
  Watapiga kura kivipi na wakati Watanzania walio wengi wameshachukua uraia wa nchi wanazoishi? na uraia wa nchi mbili, Serikali inaufanyia kauzibe pamoja na kuwa majirani zetu kama Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi wamesharuhusu uraia wa nchi mbili.
   
 6. K

  Kinyikani Member

  #6
  May 15, 2009
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 65
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  mzee umechemsha
   
 7. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #7
  Aug 14, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Naomba kuuliza wajemeni....hivi kama nikiwa nje ya nchi naruhusiwa kupiga kula (vote)?...na kama naruhusiwa je nitapigaje?..sijui kama nimeeleweka.....
   
 8. A

  August JF-Expert Member

  #8
  Aug 15, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  kwa sasa huwezi piga kura, sheria hiyo au haki hiyo haijapitishwa bado, na hii inatokana na historia au dhana kwamba walio nje , ni wapinzani wa serikali iliyo madarakani, hivyo hawawezi mkaribisha adui karibu yao.
   
 9. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #9
  Aug 15, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Japokuwa sina takwimu, lakini inaonesha watanzania wenye makazi ya kudumu nje ya nchi ni wengi ukilinganisaha na wale walioko masomoni au wanafanya kazi kwa muda maalum then watarejea nyumbani. Kwa mantiki hiyo basi nadhani suala la kupiga kura liachwe kwa wale waliopo ndani ya Tanzania wachague viongozi wanaotaka wawaongoze. Akina sie ambao tunakaa na kuishi ughaibuni tusiwachagulie waliondani waongozwe na nani.
   
 10. H

  Haki JF-Expert Member

  #10
  Aug 15, 2009
  Joined: Jan 14, 2009
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Utapiga vipi kura wakati hulipi kodi TZ? Nyie mnaojiita WTZ mnaoishi nje ya nchi mnataka kupiga kura bila ya kuchangia kodi. Mnafanya kazi nje ya nchi, hamlipi kodi TZ; lakini mnataka mpewe haki kama WTZ wengine. Kama mnataka kupiga kura lipeni kodi ya kipato mnachoingiza. Kwa mfano, raia wa USA analipa kodi ya nchi hata kama akifanya kazi nje ya nchi. Sasa kwanini nyinyi hamlipi kodi? Sisi tunaumia huku Bongo na tunalipa kodi; kwa sababu tunataka maendeleo ya Taifa letu. Naliomba Bunge lichukue hatua kali dhidi ya watu wanaoishi nje ya nchi wanaotaka kupiga kura bila ya kulipa kodi. Inaumiza sana kuona WTZ wanaoishi nje ya nchi hawalipi kodi wanapewa haki kama raia wengine ambao wanalipa kodi. Tunaomba Bunge ipitishe Muswaada kuhusu haki za wanaolipa kodi na wasiolipa kodi.
   
 11. H

  Haki JF-Expert Member

  #11
  Aug 15, 2009
  Joined: Jan 14, 2009
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Utapiga vipi kura wakati hulipi kodi TZ? Nyie mnaojiita WTZ mnaoishi nje ya nchi mnataka kupiga kura bila ya kuchangia kodi. Mnafanya kazi nje ya nchi, hamlipi kodi TZ; lakini mnataka mpewe haki kama WTZ wengine. Kama mnataka kupiga kura lipeni kodi ya kipato mnachoingiza.

  Kwa mfano, raia wa USA analipa kodi ya nchi hata kama akifanya kazi nje ya nchi. Sasa kwanini nyinyi hamlipi kodi? Sisi tunaumia huku Bongo na tunalipa kodi; kwa sababu tunataka maendeleo ya Taifa letu. Naliomba Bunge lichukue hatua kali dhidi ya watu wanaoishi nje ya nchi wanaotaka kupiga kura bila ya kulipa kodi. Inaumiza sana kuona WTZ wanaoishi nje ya nchi hawalipi kodi; lakini wanapewa haki kama raia wengine ambao wanalipa kodi. Tunaomba Bunge lipitishe Muswaada kuhusu haki za wanaolipa kodi na wasiolipa kodi.

  Kama hulipi kodi pia FISADI. Kwa hiyo hawa wanaojiita WTZ wanaoishi nje ya nchi ni MAFISADI pia.
   
 12. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #12
  Aug 15, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Pendekezo lako juu ya sheria ya kodi na kupiga kura ni zuri, lakini maswali yako hayana msingi wa kujikita kisheria na kikatiba.

  KWa vile umekwisha toa pendekezo la kutaka Bunge lipitishe sheria juu ya haki za walipa kodi na waso lipa kodi kuhusu kupiga kura, ingekuwa vema ungechukua fursa hiyo kunyamaza na kuacha kusema hayo mengine mpaka ombi lako litekelezwe.

  Vinginevyo kisheria bado tuna haki ya kupiga kura.

  Sasa nikuulize wewe,

  Wale wasolipa kodi wanaishio Tanzania wako kwenye kundi lipi?

  Wale walolipa nusu kodi na nyingine kuikwepa na makazi yao ni Tanzania je?

  Kigezo cha kupiga kura mpaka hivi niandikapo ni uraia, haki ya uraia ya mtu aishiye nje unaindoa vipi?

  Watu walioko nje ya nchi kosa lao ni nini?

  Ni kukimbia nchi ili wasimenyeke kama wewe na kupata raha burebure za huko nje au ni kuishi nje ya nchi ili wakwepe kodi?

  Chombezo

  Walikuliza Viza?
   
 13. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #13
  Aug 15, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  kwa sasa huwezi na hakuna sheria inayopinga bali ni nchi yetu amabayo inaviongozi wenye akili finyu hawajawahi kufikiria swala kama hilo.lakini kama uko nje ya nchi una haki ya kupiga kura kama mtu aliokuwepo tanzania kwani wewe bado ni raia wa tanzania.kwa vile nichi inaongozwa hovyo hovyo hilo swala lijatiliwa maanani.
   
 14. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #14
  Aug 15, 2009
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Cha kwanza watu wa nje hawapigi kura, vilevile hakuna hiyo sheria ya kulipa kodi hivyo huwezi kuwaambia watu walipo kodi wakati hakuna sheria yeyote iliyopitishwa. Huduma kwa Watanzania walio nje hakuna ukifa huku nje unategemea ndugu na jamaa, Wamekani wanalipa kodi lakini wanasaidiwa kwenye matatizo yote wanayoyapata wakiwa nje hata kama ni chakula na malazi. Hatuwezi kulipishwa kodi kama hatuelewi pesa inatumika vipi? Je unajua Watanzania walionje wanatuma kiasi gani cha pesa kila mwaka Tanzania! ni zaidi ya dollar milioni 100 hizo pesa zineenda kusaidia nchi kwa namna moja au nyingine.Bibi zetu nyumbani wanatuomba pesa za solar na visima vitu ambavyo serikali ingeweza kufanya.
   
 15. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #15
  Aug 15, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Tanzania kuna kodi nyingi sana, inawezekana kweli watanzania walioko nchi za nje hawalipi kodi ya mapato na kodi ya VAT, lakini kuna watu wengi sana wallioko nje ya nchi wanalipa kodi za viwanja vya nyumba zao zilizoko Tanzania, kodi za magari yao yaliyoko Tanzania na kodi nyinginezo. Nadhani umetumia dhana potofu ya odi kudhani kuwa kodi ni ya mapato tu, na vile vile kudhani kuwa watanzania wanaoishi nchi za nje hawana mali zinazotozwa kodi Tanzania.
   
 16. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #16
  Aug 15, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Sheria ya kupiga kura haitumii kodi ya mapato kama sifa ya kupiga kura; kuna watu wenye kipato cha chini kisichotozwa kodi ya mapato ambao wanapiga kura. Sifa pekee ya kupiga kura ni kuwa na umri usipongua miaka kumi na nane, kuwa na akili timamu, kutokuwa mfungwa, na kuwa umejiandikisha katika daftari la wapiga kura. Nina imani kuwa kitendo cha serikali kushindwa kuweka utaratibu wa kuandikisha watanzania walioko nje ili wapige kura zao ni kuwakoshesha watanzania hao haki yao ya kikatiba.
   
 17. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #17
  Aug 15, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Kichuguu:

  Nashukuru kwa kuliweka hili sawa. Naona watu wanashindwa kutofautisha haki za raia na sheria za mapato.

  Kulipa kodi ni sheria za mapato. Unalipa kodi pale unapopata mapato kwa sababu kodi hiyo itajenga barabara inayotumika kukupatia mapato, hospitali na huduma zingine za kijamii. Hivyo basi hata mwekezaji wa kutoka nje anatakiwa kulipa kodi lakini hana haki za kiraia.

  Kupiga kura ni haki ya kiraia. Na kama ni haki ya kiraia basi raia yoyote aliyefikisha vigezo vya kupiga kura anaweza kutimiza wajibu wake. Kwa mfano kuna wanafunzi wengi tu ambao hawajawahi kuzalisha au kulipa kodi lakini wakati wa uchaguzi wanapiga kura. Hivyo hakuna sababu zote za watu walio nje wasipige kura.

  Kwa upande wangu nisingependelea watanzania walio nje wapige kura kwa sababu serikali itapata kisingizio cha kufuja pesa.
   
 18. K

  Kinyikani Member

  #18
  Aug 15, 2009
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 65
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  naona bado unausingizi mzito kwanza hiyo kura yako haitakuwa na maana yoyote mbele ya CCM hata watanzania wote wasiipigiye CCM basi bado NEC watawatangaza CCM na la pili CCM hawaruhusu watu kupiga kura waliopo hapa tanzania itakuwa waliopo nje ya nchi???????????????
   
 19. F

  Fungu la kukosa Member

  #19
  Aug 16, 2009
  Joined: Jun 16, 2009
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inashangaza kwa mtu ambaye kama wewe unayeishi majuu kuwa na mawazo potofu kama haya uyatowayo.Kupata makazi ya kudumu ughaibuni hakuondoi utanzania hata kama una passport ya huko. Makazi ya ughaibuni ni sawa na mwanamke aliyewekwa kimada siku na muda wowote hata kama ni usiku wa manane anaweza kutimuliwa.Vivyo hivyo na wewe ukawe tayari kuikabili hali hiyo. Bongo ni kwetu na swala la kupata viongozi bora ni muhimu kwani ipo siku tutake tu si take tutakuwa ni wenye kerejea Bongo japokuwa tu wazee mno au maiti. Mkataa kwao ni Mtumwa, na ukiona vya eleya basi vimeundwa.Ughaibuni kuzuri kweli lakini wazungu walifanya kazi ya kuendeleza nchi zao wewe na mimi je twangoja nini? Tafadhali kuwa na mawazo ya kizalendo na si ya kitumwa.
   
 20. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #20
  Aug 17, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Kelly, katiba unakupa haki ya kupiga kura i.e. kama una miaka zaidi ya 18, lakini sheria ya uchaguzi haikupi fursa hiyo. Sababu kuu ni kuwa, Kwanza zoezi la kuandikisha watu kwenye daftari la kudumu la wapiga kura lilikuwa la wakazi tanzania tu, halikujali kabisa watanzania wenye haki ya kupiga kura lakini wasio wakazi wa tanzania. Sheria ingeweza kukuruhusu kama ungekuwa umejiandikisha na vilevile kama ungeweza kuja na kadi yako ya kujiandikisha na kupiga kura na kurudi ulaya.

  Ingekuwa hivyo kwa vile hatuna System ya kupigia kura ubalozini kama wafanyavyo wenzetu . Utaona kuwa njia iliyobakia ni wewe kuja huku na kupiga kura ( kama umejiandikisha) zoezi ambalo litakugharimu hela nyingi sana kaika kutimiza haki yako ya msingi.

  Ufanye nini? Sheria inakuruhusu kufungua kesi ya kikatiba kupinga kunyimwa haki yako ya kikatiba. Kwa vile sheria ya uchaguzi inapingana na Katiba ya nchi unayo haki ya kudai enforcement ya haki hiyo ya msingi mahakamani.
   
Loading...