Ndiyo wakuu! Heshima kwenu! Natambua uwepo wenu hapa JF. Ninaomba kukishauri chama changu cha CDM kumtimua Zitto haraka. Sababu zifuatazo:-
Mosi siku zote amekuwa mtu wa kuanzisha chokochoko na asiyeeleweka. Katika nafasi yake aliyonayo katika chama alipaswa awe mtu wa kukijenga chama siyo kubomoa. Kwa MFANO:- Wakati chama kinapambana ili kulinyakua jimbo la Arumeru mashariki kwa Joshua Nasari Zitto akaona ili kukivuruga chama aufanye huo ni muda wa kukivuruga chama kwa kutangaza kugombea Urais.
Pili huwa hashiriki katika kazi za chama kikamilifu. Siku zote amekuwa akionyesha kushiriki shughuli za chama kwa manati.
Tatu, amekuwa akipingana na maamuzi ya chama Tena waziwazi. Akiwa kama kiongozi alipaswa awe mstari wa mbele kupigania na kuyatetea maamuzi ya pamoja ya chama. Kwa mfano siku ile bungeni wezake wanatoka kwa kuonyesha kutorizika na matokeo yaliyompa ushindi kiwete yeye hakufika kabisa bungeni kuonyesha kutokubaliana ma maamuzi ya chama.
Nne, ana makundi ya sirisiri ndani ya chama yanayolenga kuwabomoa wapinzani wake kitu amabacho kinaweza kuvuruga chama pia
Tano, Mshirikina. Siku zote uchawi ndiyo limekuwa tumaini lake. Si mara ya kwanza kwa huyu ndugu kusema ameaga kwao................ Hizo zote ni tambo za kishirikina. Katika karne hii hayo mambo ya kishirikina yamepitwa na wakati.
NB:- Wamekuja wakina Pro. Safari ndani ya muda mfupi wamekisaidia sana chama lakini zitto ana lengo la kukivuruga chama. Naomba zitto atimuliwa.
Naunga hoja mkuu, Zitto lazima atimuliwe Na asipo timuliwa natoa angalizo lifuatalo
kuna possibilty ya zitto kukihma chama ifikapo karibu na uchaguzi 2015
Hali hiyo itajitokeza ,na itasababisha kuwagawa wapiga kura, Bora afukuzwe mapema ili wananchi wamjue mapema ,na wajue sababu za kumtimua ni zipi. tukija waambia babaye wananchi hawata tuamini. Bora tumfukuze mapema ili tujipange sawasawa.
Zitto yupo kimalengo ya kuisambaratisha Chadema, na kuifanya ishindwe kufikia Malengo yake.
zitto alishaanza kutuhujumu akishirikiana na wana CCm, sasa tumesha mstukia ,anaweza kuomba msamaha au akajisafisha ki jinsi anavyojua yeye ,ili mradi anasubiri Uchaguzi ufike ili agombee either kama mgombea Binafsi au agombee kupitia chama kingine cha siasa kitu ambacho kitazigawa Kura za Chadema
Solution to the problem
Afukuzwe avuliwe nadhifa zake zote ndani ya chama, then baadaye wamfukuze..
afukuzwe,afukuzwe,afukuzwe,afukuzwe,afukuzwe,afukuzwe,afukuzwe,afukuzwe,afukuzweafukuzwe,
Asije kuja kuzigawa kura za chadema ,na kuipa ushindi CCM.
AFUKUZWE KABISA