Shocking! Kupunguza foleni, Amina Amour (mbunge) ashauri serikali iongeze ushuru!

Ndugu Uswe alichosema huyo mama hajakosea kabisa , ni moja tu ya namna ya kupunguza foleni. Alichokosea ni kuwa bado public transport ni mbaya hivyo hata ukipandisha kodi huyu mtu anakuwa hana alternative zaidi ua kuendelea kuumia kutumia gari lake. Nchi zingine kwa mfano Brazil walifanya sana hiyo style lakini wakijua RBT zinasaidia na kuwa substitute. Tanzania huwezi ukaingia kwenye daladala na laptop yako ukajiona salama!

Kati watanzania 1000 ni watanzania 4 wenye magari yakutembelea,kuna haja ya kushusha CIF ili watz wamiliki magari.Dar kuna watu zaidi ya 4.5 milion lakin magari hayafiki 100,000.Bado mikoani hamna hata magari.
 
Tatizo la huyo Mbunge Hajui Mahrsabu

Hajui mpk sasa wananchi wanakatwa shs ngapi au % ngapi ya Kodi unapoingiza gari toka nje ya nchi
 
Kati watanzania 1000 ni watanzania 4 wenye magari yakutembelea,kuna haja ya kushusha CIF ili watz wamiliki magari.Dar kuna watu zaidi ya 4.5 milion lakin magari hayafiki 100,000.Bado mikoani hamna hata magari.

CIF stands for Cost Insurance and Freight, hii iko nje ya uwezo wa serikali, i mean hakuna kitu serikali inaweza kufanya kitakachoshusha CIF, ila serikali inaweza kupunguza idadi na viwango vya ushuru ili kumpunguzia mTZ mzigo
 
Uswe,

Nani anapanga Cost, Insurance and Freight?

Ukienda TPA ukasema nimeleta gari langu nimenunua dola buku moja tu, nimesafirisha bure kwenye contena la mjomba wangu na niliamua nisikate bima maana ni kimeo anyway, na makaratasi yake haya hapa. Watakubali? Assume ni ukweli kabisa. Watakubali?

Nani anapanga cost, insurance and freight?

Ndo maana mshkaji anasema serikali ipunguze cost, insurance and freight.
 
yaani hawa wabunge wengine sijui hata wamefikaje fikaje huko bungeni, na akili zake kabisa badala ya kuja na solution ya kupanua barabara yeye anataka magari yapungue sio? Tanzania ni zaidi ya uijuavyo jamani
 
Uswe,

Nani anapanga Cost, Insurance and Freight?

Ukienda TPA ukasema nimeleta gari langu nimenunua dola buku moja tu, nimesafirisha bure kwenye contena la mjomba wangu na niliamua nisikate bima maana ni kimeo anyway, na makaratasi yake haya hapa. Watakubali? Assume ni ukweli kabisa. Watakubali?

Nani anapanga cost, insurance and freight?

Ndo maana mshkaji anasema serikali ipunguze cost, insurance and freight.

CIF ni kati yako na Supplier, Tatizo watu huwa wanachakachua sana ili kupunguza kodi kwa sababu wanajua TRA huwa wanatumia CIF kukokotoa kodi.

Kama TRA wanahisi kuna tofauti ya bei ya kawaida na ile unayo-declare huwa wanafanya estimation wenyewe mara zote kwa ku-uplift price, lakini ukitoa uthibitisho kwa mfano ukatoa transmission copies say za swift kutoka bank huwa wanakubali, shida ni pale unaposhindwa kuthibitisha hiyo bei yako.

Insurance si lazima kulipa na kama hujalipa huwa hawalazimishi, kama hujalipa insurance basi kodi watakokotoa kwenye C&F.

Pia wana-assumption kwamba hiyo gari ina gharama flani, hata kama wewe umepewa zawadi na gharama ya kusafirishia umelipiwa (kwa hiyo kwako ni bure) yule aliekutpa bure na kukulipia gharama ya usafirishaji si kalipa kiasi flani?
 
Amefikiri hadi kichwa kikamuuma,akagundua Foleni ya Dar inasababishwa na kiwango kidogo cha Kodi kwenye Magari,Anahitaji pongezi na si lawama.Bila kauli kma hiyo kutolewa bungeni ingekuwa vigumu sana kwenu kutambua uwezo wa waheshimiwa kufikiri na kutafuta namna ya kutatua matatizo ya taifa

Wakuu hapo kwenye red, Nadhani ingebidi aambiwe ni % ngapi inayolipwa halafu aseme kama ni vijisenti ama?
 
Inasikitisha Bungeni kuna wawakilishi wenye ubongo wa namna hiyo! MAGARI SIYO MENGI ila Barabara hazijaongezwa ni hizo hizo alizoacha Mkoloni,miaka hamsini(50) iliyopita na serikali yake imeshindwa kuongeza barabara,kama ilivyoshindwa kuongeza mashule, vyuo, hospitali, nyumba, viwanda nk nk FAILURE OF THE GOVERNMENT TO BUILD INFRASTRUCTURES siyo wingi wa magari. Wingi wa Magari haujui huyo kilaza! Kila mtanzania mtu mzima ana haki ya kumiliki gari, na hapo bado ni maskini wa kutupwa je nchi ikiwa tajiri na kila mtu akawa na gari atasemaje! naona anadhani magari ni haki ya Viongozi na Wanasiasa.
 
Barabara hujengwa na kodi sasa lipeni kodi ili mjengewe... Au Magogoni kuna mpesa pesa?
 
I strong agree with you ndugu yangu, hawa wanajijali wao zaidi kuliko maslahi ya wale waliliowapo hivyo vibarua vya kuingia bungeni

Kwani shangingi lake limelipiwa kodi? Tangu lini aliyeshiba akamjua mwenye njaa wakubwa? Ni kama story ya Malkia wa Ufaransa wakati watu wana andamana kwa kukosa mkate akashauri kama mkate haupo si wale keki! Ndo wawakilishi wetu hao,
 
eeh!! I'm never too old to be surprised.

Najiuliza hivi mbunge kama huyu aliteuliwa kwa vigezo gani kuingia bungeni? Naamini hata house girl wangu ana upeo mkubwa kuliko huyu mbunge!!

Tanzania tuna safari ndefu kuelekea kwenye maendeleo, jiulize huyu mbunge anaweza kusoma ripoti ya CAG akaielewa na kutekeleza jukumu lake? Anaweza kusoma mswada wowote na kuelewa impact yake in a bigger picture?

Ndo maana bunge limegeuka kuwa ukumbi wa mipasho kama club continental "kanga moja...laki si pesa"
 
Back
Top Bottom