Mkuu hebu jibu swali jepesi tu. Tanzania ni muungano wa nchi huru mbili amambazo ni Tanganyika na Zanzbar. Zanzbar bado ipo kama nchi na kama serikali. I wapi Tanganyika kama nchi na serikali? Na kama Tanganyika haipo iliyeyukia wapi?Kwa hiyo unakubali wenzako kubaguliwa?
Kwakuwa Nilisha sema na kuandika Mawazo yangu juu ya Muundo Wa Muungano wetu Mara kadha na hasa kuhusu dhana ya utanganyika.
ninaomba kuweka Hapa Sehemu Kati ya yale aliyo ya sema Prof. Idea Shivji wakati wa kongamano la vijana hivi majuzi. Msisitizo Zaidi Hasa kwenye Suala la UTANGANYIKA!!
Nanukuu,
"Juu ya hilo la Utanganyika, ningependa kuongeza maneno machache hasa kwa faida ya vijana wetu. Nimeshangaa kidogo kwamba hata mzee na mwanazuoni mwenzangu Prof. Mpangala ametumia msamiati wa Utaifa wa Tanganyika bila kudadisi kihistoria Utaifa wa Tanganyika.
Kwa muhtasari tu, kabla ya vita vya kwanza, hatukuwa na Tanganyika. Tulikuwa na German East Africa ambayo eneo lake lilijumuisha Burundi, Rwanda na eneo hilo la Tanganyika chini ya himaya ya ubeberu wa Wajerumani. Baada ya Ujerumani kushindwa katika vita, Rwanda na Burundi ziligawiwa kwa Ubelgiji na Tanganyika kwa Uingereza. Waingereza ndipo wakaunda neno hili Tanganyika na iliitwa Tanganyika Territory, yaani, bustani ya wakoloni, siyo taifa.Mababu zetu waliopigania uhuru walijikita kwenye dhana ya Utaifa wa Kiafrika, kama alivyoeleza vizuri tu Profesa Mpangala. Vyama vya wananchi, kutoka TAA (Tanganyika African Association) mpaka TANU (Tanganyika African National Union), viliweka msisitizo kwenye African, Uafrika wao. Iliwabidi kuweka neno Tanganyika kwa sababu tu ndilo lililokuwa eneo la utawala wa wakoloni.Tulipopata uhuru mnamo Desemba 1961, hatukuwa taifa kwa sababu mkuu wa nchi bado alikuwa Malkia. Mwezi wa Novemba 1962 ndipo tukawa Jamhuri ya Tanganyika wakati Mwalimu alipochaguliwa kuwa Rais. Na Mwalimu tangu mwanzo alisistiza kwamba sisi hatukuwa taifa bali mkusanyiko wa makabila na lilikuwa jukumu la serikali huru kujenga utaifa (nation-building).
Lakini Mwalimu hakupata muda wa kutosha kujenga utaifa wa Tanganyika kwa sababu mwezi Aprili 1964, yaani baada ya miezi 14 tu, tukaungana na Zanzibar kuwa Tanzania. Na kwa takriban nusu karne tumekuwa tunajenga Utaifa wa Tanzania.
Sasa hii dhana ya Utaifa wa Tanganyika, au Utanganyika, unatoka wapi? Na mantiki na historia yake ni ipi?Ningependa kujua hapa tulipo ni vijana wangapi kati yenu mlizaliwa kama Watanganyika. Nyoosheni mikono juu. Nyinyi wote mlizaliwa mkiwa Watanzania, utaifa wenu ni Utanzania; utambulisho wenu ni Utanzania; mnajitambua kama Watanzania na mnatambuliwa na wengine kama Watanzania.Ukweli ni kwamba mkingangania Utanganyika wenu, ambao wala hamjui kama mtakuwa mnavunja taifa, mtakuwa mnatumikia maslahi na matakwa ya mabeberu na wanasiasa wachache wenye uchu wa madaraka. Na Utanganyika wenu hautadumu kwa sababu mtaanza kudai sasa Jamhuri ya Makonde na Jamhuri ya Sukuma! Mtakuwa vipande vipande. Hivi siyo vitisho; kuna mifano hai mbele yetu. Somalia imesambaratika, Libya pia, Sudan, Afrika ya Kati, na nchi nyingine nje ya Afrika Afghanistan, Pakistan, Syria, Iraq bila kutaja nchi za Ulaya"
- Prof. Issa Shivji 2014.
Comrades, maneno haya ya mwanazuoni huyu nikama ameyasikia kutoka kwangu ama kuyasoma katika kuta zangu katika mitandao mbali mbali,. Sijilinganishi naye., hapana hata kidogo. Ila ninachosema nikwamba mtu yeyote mwenye nia njema na fikira tulivu anaweza kung'amua nia hasa ya wale wanaotupandikiza hisia za utanganyika na uzanzibari. Walafi wamadaraka!!
Nilisha sema na ninasema tena hapa Tanganyika Siijui, na wala Siihitaji.!!
Comrades ninashukuru sana.
wewe ulishuhudia balali akizikwa?Kwa hiyo Balali kuzikwa Marekani ndio tuseme alikuwa na ngozi ya ki-"Shivji?" Nilishasema huu utanganyika hautaishia kuwabagua tu Wazanzibari, bali tutaanza kubaguana wenyewe kwa wenyewe! Mungu atuepushie mbali na huu msukule wa Utanganyika!
Kwa hiyo unakubali wenzako kubaguliwa?
Mkuu hebu jibu swali jepesi tu. Tanzania ni muungano wa nchi huru mbili amambazo ni Tanganyika na Zanzbar. Zanzbar bado ipo kama nchi na kama serikali. I wapi Tanganyika kama nchi na serikali? Na kama Tanganyika haipo iliyeyukia wapi?
Angalia Post hii hapa chini ndio utaelewa jinsi washabiki wa Utanganyika walivyopinda:nani anabaguliwa?
Male Gigolo
Today 11:53
MemberArray
Join Date : 20th February 2014
Posts : 38
Rep Power : 314
Likes Received9
Likes Given3
[h=2]Re: Shivji: Tanganyika Siijui, Siihitaji[/h] Muhindi wa India huyu anaongea Pumba siku hizi naona anazeeka Vibaya.... Dengu zimezidi pilipili ameamua kupumua.... Tanganyika huku akisema haijui... hana tofauti na Nyani anayekata tawi alilokalia.... Akianguka ndio atajua Janja yake...
I am a Bongo man Male ''Gigolo'' i give Woman Pleasure
Kwa hiyo Balali kuzikwa Marekani ndio tuseme alikuwa na ngozi ya ki-"Shivji?" Nilishasema huu utanganyika hautaishia kuwabagua tu Wazanzibari, bali tutaanza kubaguana wenyewe kwa wenyewe! Mungu atuepushie mbali na huu msukule wa Utanganyika!
naunga mkono hoja kama hakuna haja ya tanganyika na zanzibar nia moja=TAN-ZA-NIA nchi iwe ni tanzania isiyotokana na muungano iwe na serikali moja zanzibar iwe mkoaOk ok if that is the case, tuwe na serikali moja na sio mbili......!!!!!
...Whatever form the new unity takes it ought to observe scrupulously the basic democratic principle of the right of people to self determination. This premise has two sides to it.
A) That between Zanziba and Tanganyika, as a people and nations, we would have to respect the principle of equality on the one hand, and be sensitive to the legitimate culture, history and sentiments of both parts, on the other. This means that THOSE OF US who come from the bigger nation, Tanganyika, and consider OURSELVES progressive and democrats, should be extra responsible and cautious in guiding against big nation Chauvism.
Angalia Post hii hapa chini ndio utaelewa jinsi washabiki wa Utanganyika walivyopinda:
iliyoungana na zanzibar april 26/1964 wendawazimu huita tanzania bara.Tanganyika ipi uitakayo, ya Mwingereza au Mjerumani?
Nimeuliza hapa, ni yupi Kati yetu anaeweza kujifisia akisema yeye ni mtanganyika zaidi kuliko alivyokuwa Mwalimu Nyerere??! Ni nani?
Nimeuliza hapa, ni yupi Kati yetu anaeweza kujifisia akisema yeye ni mtanganyika zaidi kuliko alivyokuwa Mwalimu Nyerere??! Ni nani?
Kaka fikiri nje ya box! Sijasema kuhusu ubaguzi hapo. Kama ungeelewa, nilikuwa ninamaanisha watu wenye uraia pacha hawawezi kuwa na uchungu na nchi zote lazima moja hataitilia maanani. Kama ni suala la rangi mbona Waziri Leader Stirling baada ya kufariki alichomwa na majivu yake yalitupwa hapa hapa Tanzania! Pamoja na hayo, una uhakika gani kama Balali amezikwa US! (tuwekee death certificate hapa)Kwa hiyo Balali kuzikwa Marekani ndio tuseme alikuwa na ngozi ya ki-"Shivji?" Nilishasema huu utanganyika hautaishia kuwabagua tu Wazanzibari, bali tutaanza kubaguana wenyewe kwa wenyewe! Mungu atuepushie mbali na huu msukule wa Utanganyika!