Shivji: Mimi ni muumini serikali mbili

Shivji: Mimi ni muumini serikali mbili

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
26,021
Reaction score
25,423
Mhadhiri mwandamizi mstaafu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) na gwiji wa sheria nchini, Profesa Issa Shivji (pichani), amesema ni muumini wa muundo wa Muungano wa serikali mbili tangu zamani.

Alisema hayo jana kwenye kipindi cha Nipashe, kinachorushwa kila siku asubuhi na Radio One Stereo.

Profesa Shivji alisema amekuwa muumini wa muundo wa serikali mbili tangu mwaka 1983 na kwamba, wanaosema amebadili msimamo wake ni waongo, kwani katika kipindi hicho walikuwa bado hawajazaliwa.

Alisema hakuna siku, ambayo aliwahi kusema wala kushauri uwapo wa muundo Muungano wa serikali tatu.

“Wanaosema kuwa kuna chama kinachonisukuma na ambacho ninaegemea kwenye msimamo wao, kuhusu muundo wa serikali tatu hayo ni maoni yao binafsi,” alisema Profesa Shivji.

Kauli ya Profesa Shivji inakuja, huku kukiwa na shutuma kutoka kwa watu mbalimbali, ambao wamekuwa wakimlaumu kuwa ni kigeugeu, kwani huko nyuma aliwahi kusema kwamba, Zanzibar ina haki ya kuwa na mamlaka kamili.

Profesa Shivji akizungumzia Tume wa Warioba, alisema kuwa hakuwahi kutoa maoni yake kwenye Tume hiyo, isipokuwa aliitwa katika hatua za awali ili kutoa maelezo na mwongozo wa masuala ya kuzingatiwa katika kutengeneza katiba. Machi 30, mwaka huu, Profesa Shivji akizungumza kwenye kongamano la wasomi wa vyuo vikuu, lililoandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, alisema Katiba ya Zanzibar ndiyo sababu kubwa ya mgogoro ndani ya Muungano.

Alisema marekebisho ya 10 mwaka 2010 ya Katiba ya Zanzibar yaliyoitambua Zanzibar kuwani nchi yenye mamlaka na mipaka yake na kumpa mamlaka rais wa Zanzibar kugawa maeneo ya mkoa, wilaya, na kupora madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ndiyo sababu ya matatizo katika Muungano.

Alisema pia kwamba, marekebisho mengine yaliyofanyika mwaka 1993 katika katiba hiyo yaliipa Zanzibar mamlaka ya kuwa na bendera na wimbo wa Taifa na kupendekeza kwamba, njia bora ya kulinda Muungano wenye muundo wa serikali mbili, ni kuondoa marekebisho hayo katika Katiba ya Zanzibar.

Profesa Shivji ambaye alikuwa mzungumzaji mkuu, alifafanua kuwa wanaotaka serikali tatu hawajui historia ya Muungano na ni wanasiasa, ambao ni wavivu kusoma na hawataki kufanya uchambuzi kabla ya kuzungumzia jambo linalowafikia.

Tume ya Jaji Joseph Warioba ilipendekeza muundo wa serikali tatu kwa maelezo kuwa ndiyo utakaokuwa mwarobaini wa kero za Muungano.

Jumatatu wiki hii, wajumbe wawili wa Bunge Maalumu la Katiba, Tundu Lissu na Jussa Isamail Ladhu waliitisha mkutano wa waandishi wa habari mjini Dodoma na kumtuhumu Prof. Shivji kuwa anasaliti msimamo na machapisho yake aliyoyasimamia kwa zaidi ya miaka 30 iliyopita kwa lengo la kuifurahisha serikali na CCM. Lissu na Jussa walisema wanamshangaa Prof. Shivji kwa matamshi yake na kutoamini kama aliyoyasema ilikuwa ni kwa akili yake au alishinikizwa.

Lissu alisema msimamo wa sasa wa Profesa Shivji kwamba Muungano wa serikali mbili unapaswa kudumishwa, umeshtua kwa kuwa unapingana na maandiko yake aliyochapisha kwenye vitabu mbalimbali yakipinga muundo wa serikali mbili.

Lissu alisema mwaka 1990 Prof. Shivji alitoa mhadhara wa kiprofesa uliosababisha apewe u-profesa akizungumzia misingi ya kisheria na uhalali wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kusema kuwa ili makubaliano ya Muungano yaweze kupata uhalali, ni lazima yatungiwe sheria ya kuridhia makubaliano hayo na mabunge ya nchi washirika.

Jussa alisema machapisho ya Profesa Shivji ndiyo yaliyochangia kuamsha vuguvugu la Wazanzibari kudai haki kwenye muundo wa Muungano, hivyo anashangazwa na kitendo cha Profesa Shivji kuyageuka machapisho yake na kutangaza hadharani kuunga mkono muundo ambao alikuwa akiukosoa kwa miaka mingi.

Alisema kitendo hicho kimemkwaza kwa kuwa yeye ni miongoni mwa Wazanzibar waliompatia ushirikiano mkubwa wakati akifanya utafiti wa masuala ya Muungano Visiwani Zanzibar.
CHANZO: NIPASHE

:yield:
 
Shivji next time uwe unasikiliza 93.7 efm kabla hujazungumza
 
Mhadhiri mwandamizi mstaafu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) na gwiji wa sheria nchini, Profesa Issa Shivji (pichani), amesema ni muumini wa muundo wa Muungano wa serikali mbili tangu zamani.

Alisema hayo jana kwenye kipindi cha Nipashe, kinachorushwa kila siku asubuhi na Radio One Stereo.

Profesa Shivji alisema amekuwa muumini wa muundo wa serikali mbili tangu mwaka 1983 na kwamba, wanaosema amebadili msimamo wake ni waongo, kwani katika kipindi hicho walikuwa bado hawajazaliwa.

Alisema hakuna siku, ambayo aliwahi kusema wala kushauri uwapo wa muundo Muungano wa serikali tatu.

"Wanaosema kuwa kuna chama kinachonisukuma na ambacho ninaegemea kwenye msimamo wao, kuhusu muundo wa serikali tatu hayo ni maoni yao binafsi," alisema Profesa Shivji.

Kauli ya Profesa Shivji inakuja, huku kukiwa na shutuma kutoka kwa watu mbalimbali, ambao wamekuwa wakimlaumu kuwa ni kigeugeu, kwani huko nyuma aliwahi kusema kwamba, Zanzibar ina haki ya kuwa na mamlaka kamili.

Profesa Shivji akizungumzia Tume wa Warioba, alisema kuwa hakuwahi kutoa maoni yake kwenye Tume hiyo, isipokuwa aliitwa katika hatua za awali ili kutoa maelezo na mwongozo wa masuala ya kuzingatiwa katika kutengeneza katiba. Machi 30, mwaka huu, Profesa Shivji akizungumza kwenye kongamano la wasomi wa vyuo vikuu, lililoandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, alisema Katiba ya Zanzibar ndiyo sababu kubwa ya mgogoro ndani ya Muungano.

Alisema marekebisho ya 10 mwaka 2010 ya Katiba ya Zanzibar yaliyoitambua Zanzibar kuwani nchi yenye mamlaka na mipaka yake na kumpa mamlaka rais wa Zanzibar kugawa maeneo ya mkoa, wilaya, na kupora madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ndiyo sababu ya matatizo katika Muungano.

Alisema pia kwamba, marekebisho mengine yaliyofanyika mwaka 1993 katika katiba hiyo yaliipa Zanzibar mamlaka ya kuwa na bendera na wimbo wa Taifa na kupendekeza kwamba, njia bora ya kulinda Muungano wenye muundo wa serikali mbili, ni kuondoa marekebisho hayo katika Katiba ya Zanzibar.

Profesa Shivji ambaye alikuwa mzungumzaji mkuu, alifafanua kuwa wanaotaka serikali tatu hawajui historia ya Muungano na ni wanasiasa, ambao ni wavivu kusoma na hawataki kufanya uchambuzi kabla ya kuzungumzia jambo linalowafikia.

Tume ya Jaji Joseph Warioba ilipendekeza muundo wa serikali tatu kwa maelezo kuwa ndiyo utakaokuwa mwarobaini wa kero za Muungano.

Jumatatu wiki hii, wajumbe wawili wa Bunge Maalumu la Katiba, Tundu Lissu na Jussa Isamail Ladhu waliitisha mkutano wa waandishi wa habari mjini Dodoma na kumtuhumu Prof. Shivji kuwa anasaliti msimamo na machapisho yake aliyoyasimamia kwa zaidi ya miaka 30 iliyopita kwa lengo la kuifurahisha serikali na CCM. Lissu na Jussa walisema wanamshangaa Prof. Shivji kwa matamshi yake na kutoamini kama aliyoyasema ilikuwa ni kwa akili yake au alishinikizwa.

Lissu alisema msimamo wa sasa wa Profesa Shivji kwamba Muungano wa serikali mbili unapaswa kudumishwa, umeshtua kwa kuwa unapingana na maandiko yake aliyochapisha kwenye vitabu mbalimbali yakipinga muundo wa serikali mbili.

Lissu alisema mwaka 1990 Prof. Shivji alitoa mhadhara wa kiprofesa uliosababisha apewe u-profesa akizungumzia misingi ya kisheria na uhalali wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kusema kuwa ili makubaliano ya Muungano yaweze kupata uhalali, ni lazima yatungiwe sheria ya kuridhia makubaliano hayo na mabunge ya nchi washirika.

Jussa alisema machapisho ya Profesa Shivji ndiyo yaliyochangia kuamsha vuguvugu la Wazanzibari kudai haki kwenye muundo wa Muungano, hivyo anashangazwa na kitendo cha Profesa Shivji kuyageuka machapisho yake na kutangaza hadharani kuunga mkono muundo ambao alikuwa akiukosoa kwa miaka mingi.

Alisema kitendo hicho kimemkwaza kwa kuwa yeye ni miongoni mwa Wazanzibar waliompatia ushirikiano mkubwa wakati akifanya utafiti wa masuala ya Muungano Visiwani Zanzibar.
CHANZO: NIPASHE

:yield:

Shivji ni mhindi, ni mchumia tumbo tu! Tanganyika itajengwa na Watanganyika na si wahindi!
 
Shivji alisahau kusema yeye pia ni muumini wa ccm! Eti hakuhojiwa na tume, kwa nini hakwenda kutoa mawazo yake huko? Huyo prof. Anazidi kujichanganya zaidi na kujidhalilisha zaidi pia!
 
"Ndiyo maana, wachache wetu tulipendekeza tuwe na Bunge Maalum la kuchaguliwa na wananchi moja kwa moja. Lakini watawala wetu, pamoja na watawala watarajiwa na wengi wa wanaharakati, katika busara zao na kwa maslahi yao, hawakutilia maanani pendekezo letu. Tumepoteza nafasi ya kipekee ya kihistoria ya kuwa na Bunge Maalum la kuchaguliwa, jambo ambalo limetufikisha hapa tuliko" - Profesa Issa Shivji: Dhana na Maana ya Bunge Maalum la Katiba

Shivji alisahau kusema yeye pia ni muumini wa ccm! Eti hakuhojiwa na tume, kwa nini hakwenda kutoa mawazo yake huko? Huyo prof. Anazidi kujichanganya zaidi na kujidhalilisha zaidi pia!

Kwi kwiii Wahindi kwa kupenda UBWENYENYE! Alitaka tume imufuate nyumbani kwake.
 
Profesa Shivji alisema amekuwa muumini wa muundo wa serikali mbili tangu mwaka 1983 na kwamba, wanaosema amebadili msimamo wake ni waongo, kwani katika kipindi hicho walikuwa bado hawajazaliwa.

CHANZO: NIPASHE

:yield:

Hii ni kauli ya kisiasa. Hivi mwaka1983 Jussa na Lissu walikuwa hawajazaliwa?
Kwa Shivji mtu yeyote anayepaswa kuchallenge muundo wa muungano wa serikali 2 ni lazima awe alikuwa amezaliwa kabla ya hapo. Km atakuwa alikuwa amezaliwa km Lissu na Jussa, basi watajifanya hawajui.
JK alitumia kauli hiyohiyo. Je Njelu Kasaka ambaye ameendelea na msimamo wake wa serikali 3 hakuwa amexaliwa wakati wa muungano 'mtakatifu' wa serikali 2?
 
Shivji alisahau kusema yeye pia ni muumini wa ccm! Eti hakuhojiwa na tume, kwa nini hakwenda kutoa mawazo yake huko? Huyo prof. Anazidi kujichanganya zaidi na kujidhalilisha zaidi pia!

Kizee cha Kihindi sasa Hali si Hali , pesa ya kununuliwa imekachanganya,Maana kalipewa Ghafra kakiwa hakajipanga vizuri,Pia kilidhani Watanganyika bado wamelala Kama zamani. Warioba amekajibu sasa badala ya kuomba radhi yaishe,Kamezidi kujikanya kanyaga tu, hicho kizee hakina Jipya ,sana sana kinajishaua tu kuwafurahisha wale waliokinunua .
 
Hicho Kizee cha kihindi Kiludishe Pesa Maana kazi kiliyotumwa imekishinda,Watanganyika wamekishitukia mapema wamekiwahi.
 
Hii ni kauli ya kisiasa. Hivi mwaka1983 Jussa na Lissu walikuwa hawajazaliwa?
Kwa Shivji mtu yeyote anayepaswa kuchallenge muundo wa muungano wa serikali 2 ni lazima awe alikuwa amezaliwa kabla ya hapo. Km atakuwa alikuwa amezaliwa km Lissu na Jussa, basi watajifanya hawajui.
JK alitumia kauli hiyohiyo. Je Njelu Kasaka ambaye ameendelea na msimamo wake wa serikali 3 hIakuwa amexaliwa wakati wa muungano 'mtakatifu' wa serikali 2?
hicho kizee cha Kihindi kinadhani Watanganyika ni Wajinga Ndio Maana kilikuja na vigezo vya ajabu Kama hivyo, sasa kametambua Hakuna Mtanganyika mjinga tena, kila mtu yupo macho na Tanganyika.
 
Wengine huku mna-comment pasipo Kujua kuna Nini Nyuma ya Pazia. Ukiona msomi kaongea Ni JAMBO la kukaa kimya Na kuwaza au kutokuandika Chochote. Wasomi huongea Chini ya miamvuli miwili , Moja Ni nia Zao Za utashi unaotokana Na elimu zao Na pili Shinikizo la Watawala. Watawala wanatisha asikwambie Mtu!! Hakuna anaye penda Kifo, Ni rahisi ku-Sacrifice dignity yako Mbele ya jamii kuepusha mabalaa unayotishiwa Na watawala, Na frankly wasomi wengi sio majasiri Ni WAOGA sana.

Nikipima uzito wa Sentensi Za Mwanafalsafari huyu, utashi huu wa Kuongea sio WAKE. Lazima pana Shinikizo Nyuma Yake. NASEMA hivi kwa ushahidi wa Waziwazi Kwamba HAPANA Kati ya WANA-CCM au SERIKALI YA JMT Kiongozi yeyote ALIYE WAHI KUWA MUUMINI WA SERIKALI MBILI. Mwalimu Julius K. Nyerere HAKUWAHI Kuwa MUUMINI wa Serikali mbili. Msomi Na wasomi wote akiwemo Shimvi WANALIFAHAM HILI FIKA Kwamba Kwa wakati ule Ilimlazimu Mwalimu Na Cabinet zake kuridhia Muungano tata wa Serikali mbili lakini mchakato ukiwa kuelekea SERIKALI MOJA. Na Hii ndio Ndoto ambayo Mwalimu alipenda Itimie HATA kabla ya Umauti wake. Lakini Bado HATA Leo CCM wanaamini Ndoto Hii yaweza timia. So Mtu akisema Ni MUUMINI wa Serikali mbili ni Uongo Na WOGA tu Hakuna kitu Kama hicho. Ccm wote nadhani HATA wananchi Wote Ni Waumini wa SERIKALI MOJA.

Lakini TOKA Mwalimu atutoke tuwe wakweli tu michakato ya KUHARAMIANA kisiasa ikaanza kukua siku HATA siku within ourselves. Kuna UPANDE wa Muungano unaamini wakiwa wenyewe wanaweza Kufanya excellent kuliko Kuwa Na Muungano. Hali Hii ikapelekea UPANDE ule KUASI.. A COMPLETE open REBELLION. Hamwezi kujitengenezea Katiba Na Kujiita Nchi Na kusafirisha mamlaka Za Kidola huku Katiba mama IKIWEPO ISIYOWARUHUSU kutenda hivyo. Ni uvumilivu, utulivu Na Hekima Za Rais Wetu kuepusha Shari Na Umwagaji Damu ambao likely usinge Zuilika.

Wananchi kupitia TUME ya Mabadiliko ya Katiba tukasema, sisi Ni Ndugu kwanini Tugombane, embu Nyie kamateni fito hizi mjenge UPANDE wa kwenu Na sisi tujenge UPANDE huu wetu kisha wote tuweke PAA. Uamuzi huu una DHAMBI gani?!!???. Uamuzi wetu Wananchi hatutaki machafuko, hatutaki kugombana Na ndugu zetu, hatutaki kupoteza uhai wa Mtu yeyote. From point pai ya UASI Ninyi viongozi mlikuwa Na Uwezo wa kudhibiti lakini mliacha tuu kiasi Leo huwezi kuidhibiti. Kuendeleza Msemo wa Serikali moja au mbili Ni UCHOCHEZI wenye Lengo la kuvuruga Na Kiondoa AMANI ya Nchi Hii.

Hakuna ANAYE VUNJA MUUNGANO HAPA. Tunaimarisha MUUNGANO WETU.
 
Back
Top Bottom