Shivji atema cheche kuhusu WEF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shivji atema cheche kuhusu WEF

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Boflo, May 9, 2010.

 1. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  *Adai WEF ni kuendeleza ubeberu
  Na Job Ndomba

  MAANDAMANO ya wanaharakati yaliyotakiwa kufanyika jana na kuishia katika Viwanja vya Mlimani city kunakofanyika mkutano wa Jukwaa la Uchumi la Dunia kwa Afrika (WEF) yamefanyika kwa namna yake ambapo yalianzia ndani ya Ofisi za Mtandao wa Jinsia Tanzania (TNGP) na kuishia nje ya viwanja vya ofisi hizo, huku Profesa Issa Shivji akimwaga 'cheche' akidai kuwa mkutano wa WEF ni wa kuendeleza ubeberu wa kibepari.


  Hayo yalitokea jana wakati wa jukwaa la wananchi wa Afrika liliandaliwa na wanaharakati hao ili lifanyike sambamba na Jukwaa la Uchumi la Dunia kwa Afrika linaloendelea Jijini Dar es Salaam kuanzia jana.

  Akizungumza katika Jukwaa hilo, Prof. Shivji alisema kuwa mkutano huo wa WEF hauna faida ya kimaendeleo kwa Afrika zaidi ya kuendeleza mfumo wa kibepari unaoendelea
  kunyonya nguvu na raslimali za waafrika.

  "Kwa ujumla mkutano huo hauna faida kabisa kwetu zaidi ya kuendeleza mikakati ya kibeberu na kibepari ya kuwanyonya Waafrika," alisema Prof. Shivji.

  Prof. Shivji alisema mkutano huo ni wa wababe wanaojiita CEOs wa makampuni ya kimataifa na makampuni ya kibepari na mashirika ya kimataifa kama benki ya dunia ambao wamejichukulia hatua ya kujadili hatma ya wengi, bila ya wao kusikilizwa na ndani yao kuna wapambe wasomi wanaotetea mfumo wao wa kibepari.

  "Ukweli wa mkutano huo ni kwamba, ni wa uchumi wa kibeberu na kibepari na watu wa Afrika hawana budi kuelewa kwa undani na kwa ufasaha mfumo huo ambao unatawala duniani na kusimamiwa na hao wanaokutana kule Mlimani City.

  "Hatuwezi kuzungumzia ukombozi wa mnyonge na wazalishaji wadogo bila kuelewa mfumo huo ambao kihistoria na sura yake mpya ni ubepari mamboleo na sababu waafrika tunaguswa moja kwa moja na mfumo huo," alisema.

  Alisema mfumo huo ni unyang'anyi unaolindwa na sheria iliyowekwa na wenyewe na kwa Afrika kumekuwa na mfumo huo kwa karne tano.

  Prof. Shivji alisema kutokana na mifumo kama hiyo kumekuwa na mpasuko wa kitabaka ambao umeonekana kukua na kuwa na matabaka mawili katika taifa moja, yaani waliokuwa nacho na wasiokuwa nacho.

  "Mwenyezi Mungu hakuumba matajiri kwa upande mmoja na maskini kwa upande mwingine, wala mabepari kwa upande mmoja na wafuta jasho kwa upande mwingine, hayo ni matokeo ya kihistoria," alisema.

  Aliongeza kuwa ukweli ni kwamba ubepari leo hauhitaji Waafrika bali unahitaji Afrika na kwamba hawana haja ya watu bali wanahitaji vitu, rasilimali na ardhi.

  Akizungumzia suala la maandamano alisema kuyazuia ni kuwanyima watu haki ya msingi ya kutakiwa kutoa sauti zao ili ziweze kusikika.

  Hata hivyo, licha ya maandamano hayo kuanza na kuishia katika eneo hilo la umbali mfupi lakini yalikuwa na mbwembwe za aina yake huku yakiongozwa na mabango yaliyokuwa yamesheheni ujumbe wa aina mbalimbali.

  Mbwembwe hizo ni pamoja na kuwa na kuongozwa na sanamu lilikuwa limevalia kanzu kubwa lenye maandishi 'Viongozi wa Afrika ni wazalendo au vibaraka'.

  Aidha mabango mengine yalikuwa yakisomeka 'Ubinafsishaji ni ukoloni mamboleo', 'wawekezaji hawatufai waondoke', 'Vita barani Afrika ni mbinu za kuchota rasilimali zetu', na 'wanawake ni wakuzaji wa uchumi katika jamii'.

  Awali akifungua mkutano wa Jukwaa hilo mbadala, Mkurugenzi wa Action Aid International Tanzania, Bi. Aida Kiangi alisema lengo kubwa la jukwaa hilo ni kujadili kwa mapana na kutoa mapendekezo kwa viongozi wa mkutano wa WEF juu ya nini
  kifanyike ili kuona jamii ya Waafrika inanufaika na uwekezaji pamoja na kuwa na usawa katika ukuaji wa uchumi.

  Bi. Kiangi alisema ni dhahiri kwamba kumekuwa na ukuaji wa uchumi kwa nchi za Afrika lakini wanaonufaika na ukuaji wa uchumi huo ni wachache na hivyo ni muhimu kujiuliza
  ni nani ananufaika na uchumi huo.
   
 2. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2010
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kama "RAHISI" wetu na viongozi wetu barani Afrika wangekuwa wanajua hili basi mambo yangekuwa tofauti katika sekta nyingi.Nimefuatilia baadhi ya sessions za WEF na nilifurahishwa sana na namna ambayo Prof. Tibaijuka alikuwa anazungumzia masuala mbalimbali yaani alionekana ana mtazamo mpana zaidi juu ya utatuzi wa matatizo ya Afrika.Mungu ibarika Tanzania!Mungu ibariki Afrika!
   
 3. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  nyerere hakukoswa kumshatapu huyu prof. akae sumbawanga miaka saba bila kutoka nje ya mkoa huo,....kifungo cha nje hicho kinaitwa. huyo prof hana jipya...ndo huyo aliyekuwa anaandamana sana akiwa na prof haroob othman aliyekufa wakiwalaani waisrael...ndo uyouyo aliyekuwa anasema hakuna Mungu kwa kuiga dini za warusi, alipoona aibu akakimbilia kwenye waislamia....atoke zake hapa. nafikiri wanauchumi humu ndani mnatakiwa kumsaidia kielimu na kimawazo uyo prof ili aelewe. mimi kanifundisha pale udsm miaka mingi iliyopita lakini, namfahamu vilivyo..
   
 4. P

  PELE JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 229
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nadhani anayepaswa kusaidiwa hapa ni wewe ambaye unabwabwaja bila mpango na si Prof Shivji.
   
 5. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #5
  May 9, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  wewe na shivji wote wawili mnahitaji msaada tena wa haraka.
   
 6. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #6
  May 9, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,060
  Trophy Points: 280
  Kwa wanaomfahamu Shivji wanasema hakuna mbaguzi wa rangi kama huyu nchi hii yaani ni mbaguzi mkubwa kiasi kwamba anaweza kutoa roho mwanae yeyote ataetaka kuolewa au kuolewa na mtu mweusi!!!! anayosema ni kwa ajili ya umaarufu tu hayako moyoni!!
   
 7. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #7
  May 9, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Sidhani kama unaweza kudai kuwa unamfahamu VILIVYO kwa kigezo ati alikufundisha udsm. Kama kweli na wewe ni msomi basi badala ya kumshambulia yeye binafsi si ungejibu hoja alizotoa? Kama haya ndiyo matokeo ya kufundishwa pale udsm basi inasikitisha. Heri sisi ambao tulikimbia umande.

  Amandla......
   
 8. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #8
  May 9, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mwingine huyu. Ati kwa wanaomfahamu! Kwani mtu kutaka mwanae aolewe au aowe mtu wa kwao imekuwa ndio ubaguzi wa rangi? Acheni fitna na uzushi. Jibuni hoja zake ama sivyo mnyamaze. Mnataka kutuharibia jamvi.

  Amandla......
   
 9. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #9
  May 9, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hahahhahah naishia kucheka tu! Umemaliza kila kitu! Asante
   
 10. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #10
  May 9, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  nijibu hoja za nini? hivi ukiwa barabarani ukaanza kurushiana mawe na chizi, si watu watasema na wewe chizi? utajikuta wote mmekamatwa mmepelekwa kwenye clinic ya watu insane bure. ninamfahamu shivji, kama wewe haumfahamu unachobisha nini? hana lolote, mbaguzi, na alijifanya kuwatetea walanguzi wa nchi wa kihindi kipindi kile ndo maana nyerere alimshatap. hana lolote prof yule nakwambia.
   
 11. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #11
  May 9, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,060
  Trophy Points: 280
  Asante mkuu, nchi hii wanafiki kama kina Shijvi ni rahisi sana kuaminika! sijui tukoje!! huya mhindi mbaguzi hafai!
   
 12. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #12
  May 9, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  kwa wale wanaokumbuka, alipigwa kifungo cha ndani sumbawanga miaka saba bila kutoka, nyerere kiboko aisee.
   
 13. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #13
  May 9, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,060
  Trophy Points: 280
  Hivi ee? nilikuwa sijui..
   
 14. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #14
  May 9, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Msomi unakataa kujibu hoja? Halafu unataka kujilinganisha na Shivji! Kufundishwa na mtu si kumfahamu. Au alikushikisha mwaka? Hii biashara ya kumuita kila mtu mwenye rangi tofauti anayetukosoa, won,t fly anymore. Jibu hoja. Kama hauwezi, waachie wale walioenda shule na kuelimika wamkosoe Profesa. Mnatupotezea wakati.

  Amandla......
   
 15. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #15
  May 9, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  haya nimekuachia wewe msomi fundi mchundo wa udsm ujibu. ungekuwa msomi si mgewapiku wachina kujenga majengo na barabara hapo tz, au ufundi mchundo wenu mnajifunza kutengeneza majiko ya mkaa? na vinu vya kukobolea unga wa muhogo?
   
 16. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #16
  May 9, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Unamsifia Nyerere kwa kumgandamiza raia wa nchi yake? Udhalimu ni udhalimu in udhalimu. Kama Nyerere alifanya hicho unachodai alifanya basi nae anastahili kulaaniwa kwa kitendo hicho.

  Amandla.......
   
 17. n

  nndondo JF-Expert Member

  #17
  May 9, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 534
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na huyu aliyesema watu wasituharibie jamvi, jadilini hoja acheni kutambiana na keleta u punch humu, wewe utamjue shivji kwa kufundishwa nae somo moja ktk miaka mitatu? Nadhani forum kuwe na namna ya ku censor majadiliano ya people yatupwe yaletwe ya issues only ama sivyo tutakata tamaa
   
 18. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #18
  May 9, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Wewe ndiye uliyedai kuwa ulisoma udsm. Mafundi Mchundo hawaendi Chuo Kikuu na kweli kazi yetu ni kutengeneza majiko bora ya mkaa. Sasa wewe uliyeenda shule , onyesha basi hiyo shule yako. Au ulikuwa unatudanganya kuwa ulifundishwa na Profesa udsm? Ona aibu wakati mwingine.

  Amandla......
   
 19. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #19
  May 9, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  umeenda chuo kujifunza kutengeneza majiko ya mkaaa...humm mbona siwaelewi, topic ni ipi hapa, kuna bifu nini?
   
 20. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #20
  May 9, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,558
  Likes Received: 1,912
  Trophy Points: 280
  Kwanini alifungwa miaka saba? Je ni kwasababu ya ubaguzi?Ama ni makosa ya kiutendaji?Sumbawanga alikuwa kikazi?ningeshukuru kama ungenielimisha kwenye hili....Sijawahi kusikia hii issue,kimsimamo anaonekana sawa na mwalimu haswa kuhusina na ubepari na haki za wafanyakazi bila kusahahu classes, ila sijui walikorofishana wapi?Na hilo la ubaguzi other than hayo ya kutotaka mwanae aolewe na mtu mweusi kuna jingine unaloweza kutolea mfano?Since umesema unamfahamu,amekufundisha nk.
   
Loading...