Shitukia Atanda, hukunifanyia utu lakini nilishangaa kusamehe

MILL8

JF-Expert Member
Aug 27, 2015
1,831
853
Ndio nilikuwa mgeni hata wiki sijamaliza toka tuhamie (Lusewa)Namtumbo, ilikuwa ni Jumatatu nimerudi toka shule nikiwa nimepumzika na braza hapo nyumbani.

Akaja msichana mmoja kakusanya vitoto vingi sana akawa anachungulia harafu wanacheka kwa dharau. Sikujua chochote ambacho wanataka braza akahisi labda mimi na huyo msichana tuna miadi alitoka na kuingia ndani, huyo msichana alivyo ona hivo akanisogelea akawa ananiporomoshea matusi hata sijui kosa langu. Eti mimi nimetuma mtu amwambie nitampa mchele wenye sukari

Akasema tena ataenda kunitangaza shuleni ili niaibike zaidi, kesho yake baadhi ya wanafunzi wa kiume wakawa wananitania "mchele wenye sukari" sikuwa na la kufanya ikumbukwe nilikuwa mgeni. Baada ya miezi kadhaa tukafanya mtihani matokeo yalipo toka nikashika nafasi ya pili, ndipo alipo badilika akawa ananisalimia akiniona anatabasamu lakini mimi sikuwa na habari nae mpaka tunamaliza shule.

Leo nimemkumbuka huyu binti #shitukia_atanda kama yumo humu JF au kama kuna mtu toka Lusewa
 
"Mchele wenye sukari" sasa tumekuelewa kwanini ulikua unatamani kupata mimba!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom