Shirika la Posta Tanzania lakutana na Jukwaa la Wahariri wa Habari Tanzania

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
SHIRIKA LA POSTA TANZANIA LAKUTANA NA JUKWAA LA WAHARIRI WA HABARI TANZANIA.

Mwandishi wetu, Dar es salaam
Leo 29 Julai, 2021.

Shirika la Posta Tanzania likiongozwa na Kaimu Postamasta Mkuu Ndugu Macrice Daniel Mbodo limefanya Mkutano na Jukwaa la Wahariri wa Habari Tanzania lengo ni kuwaeleza historia ya Shirika hilo pamoja Mpango kazi wa Shirika hilo. Shirika la Posta limetumia fursa kufikisha ujumbe kwa Wananchi kupitia kwa Wahariri mbali mbali wa Vyombo vya Habari Nchini.

Akizungumza na Wahariri wa Habari Kaimu Postamasta Mkuu Ndugu Macrice Daniel Mbodo ameeleza kuwa Shirika la Posta Tanzania lilianzishwa kwa sheria Na 19 ya Mwaka 1993 ambapo Rasmi Shirika la Posta lilizaliwa tarehe 01, Jan 1994 baada ya kuvunjwa kwa Shirika la Posta na Simu Tanzania. Historia inaeleza kwa upande wa Tanganyika Huduma ya Posta na Simu zilianzishwa mnamo mwaka 1893 chini ya Idara ya Posta na Simu ya Serikali ya Kikoloni ya Kiingereza.

Majukumu ya Msingi ya Shirika ni pamoja na Kutoa Huduma za Posta ndani na Nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kutosheleza mahitaji ya Kitaifa ya Huduma za Posta za Viwanda, Biashara na Jamii kwa Ujumla ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kutoa huduma za kutuma na kulipa fedha kwa njia ya hawala za Posta ( Money Order, Posta Order) au kwa kutumia njia nyingine zinazoonekana zinafaa ndani na nje ya Nchi.

Aidha Kaimu Postamasta Mkuu Ndugu Macrice Daniel Mbodo aliendelea kwa kuelezea sehemu ambazo Shirika la Posta limewekeza. Shirika la Posta limewekeza katika maeneo Makuu matatu ikiwemo,
Mtandao wa Shirika, Majengo na Viwanja vya upangishaji 167 na Hisa katika Benki ya Posta ( Kwasasa ni TCB)

Mwisho Kaimu Postamasta Mkuu Ndugu Macrice Daniel Mbodo alimalizia kwa kuelezea Mwelekeo wa Shirika la Posta kwasasa, Shirika la Posta kwasasa litajikita katika vipaumbele vikuu vitano 5 ikiwemo Huduma za Usafirishaji ( Courier Services), Huduma Pamoja, Duka Mtandao, Mifumo ya Tehema ya kutolea huduma za Shirika kwa Wananchi pamoja na kuboresha muonekano wa Majengo.

IMG_20210729_195941_175.jpg

IMG_20210729_195757_538.jpg

IMG_20210729_195757_540.jpg

IMG_20210729_195757_541.jpg

IMG_20210729_195757_618.jpg
 
. Historia inaeleza kwa upande wa Tanganyika Huduma ya Posta na Simu zilianzishwa mnamo mwaka 1893 chini ya Idara ya Posta na Simu ya Serikali ya Kikoloni ya Kiingereza.
Mwaka 1893 nchi hii ilikuwa chini ya ukoloni wa Mjerumani, huyo Postamasta Mkuu arudi akasome na ajifunze upya historia ya shirika hili
 
Shirika la Posta Tanzania likiongozwa na Kaimu Postamasta Mkuu Ndugu Macrice Daniel Mbodo limefanya Mkutano na Jukwaa la Wahariri wa Habari Tanzania lengo ni kuwaeleza historia ya Shirika hilo pamoja Mpango kazi wa Shirika hilo. Shirika la Posta limetumia fursa kufikisha ujumbe kwa Wananchi kupitia kwa Wahariri mbali mbali wa Vyombo vya Habari Nchini.

Akizungumza na Wahariri wa Habari Kaimu Postamasta Mkuu Ndugu Macrice Daniel Mbodo ameeleza kuwa Shirika la Posta Tanzania lilianzishwa kwa sheria Na 19 ya Mwaka 1993 ambapo Rasmi Shirika la Posta lilizaliwa tarehe 01, Jan 1994 baada ya kuvunjwa kwa Shirika la Posta na Simu Tanzania. Historia inaeleza kwa upande wa Tanganyika Huduma ya Posta na Simu zilianzishwa mnamo mwaka 1893 chini ya Idara ya Posta na Simu ya Serikali ya Kikoloni ya Kiingereza.

Majukumu ya Msingi ya Shirika ni pamoja na Kutoa Huduma za Posta ndani na Nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kutosheleza mahitaji ya Kitaifa ya Huduma za Posta za Viwanda, Biashara na Jamii kwa Ujumla ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kutoa huduma za kutuma na kulipa fedha kwa njia ya hawala za Posta ( Money Order, Posta Order) au kwa kutumia njia nyingine zinazoonekana zinafaa ndani na nje ya Nchi.

Aidha Kaimu Postamasta Mkuu Ndugu Macrice Daniel Mbodo aliendelea kwa kuelezea sehemu ambazo Shirika la Posta limewekeza. Shirika la Posta limewekeza katika maeneo Makuu matatu ikiwemo,

Mtandao wa Shirika, Majengo na Viwanja vya upangishaji 167 na Hisa katika Benki ya Posta ( Kwasasa ni TCB)

Mwisho Kaimu Postamasta Mkuu Ndugu Macrice Daniel Mbodo alimalizia kwa kuelezea Mwelekeo wa Shirika la Posta kwasasa, Shirika la Posta kwasasa litajikita katika vipaumbele vikuu vitano 5 ikiwemo Huduma za Usafirishaji ( Courier Services), Huduma Pamoja, Duka Mtandao, Mifumo ya Tehema ya kutolea huduma za Shirika kwa Wananchi pamoja na kuboresha muonekano View attachment 1873620View attachment 1873622View attachment 1873621
IMG-20210729-WA0334.jpg
 
Back
Top Bottom