Shirika la Nyumba (NHC) ni la matajiri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shirika la Nyumba (NHC) ni la matajiri

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Duma R. SIFFI, May 24, 2012.

 1. D

  Duma R. SIFFI Member

  #1
  May 24, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sikuamini machoni na masikioni baada ya kuhudhuria semina iliyohusisha mawakala kutoka NHC na Wafanyakazi wa St. Johns University of Tanzania a.k.a Mazengo compus. Kilichoniacha hoi ni kwamba wanatushauri tukanunue nyumba za Medeli residential apartment na bei ya ofa kama alivyosema mtoa mada ni Milioni 111 na point kazaa yaani Tsh. 111 milion. Swali ni je, 1. Kuna mfanyakazi gani wa St. John na mtanzania kwa ujumla anayeweza kununua hizo nyumba? 2. Atakuwa analipwa kiasi gani kwa mwezi? Nashindwa kuamini kuwa kwa hela za kihalali kabisa kama unaweza kuwa na hela kiasi hicho. Nadhani ipo haja ya kuishauri serikali yetu mara mbimbili
   
 2. D

  Duma R. SIFFI Member

  #2
  May 24, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sikuamini machoni na masikioni baada ya kuhudhuria semina iliyohusisha mawakala kutoka NHC na Wafanyakazi wa St. Johns University of Tanzania a.k.a Mazengo compus. Kilichoniacha hoi ni kwamba wanatushauri tukanunue nyumba za Medeli residential apartment na bei ya ofa kama alivyosema mtoa mada ni Milioni 111 na point kazaa yaani Tsh. 111 milion.
  Swali ni je,
  1. Kuna mfanyakazi gani wa St. John na mtanzania kwa ujumla anayeweza kununua hizo nyumba?
  2. Atakuwa analipwa kiasi gani kwa mwezi?

  Nashindwa kuamini kuwa kwa hela za kihalali kabisa kama unaweza kuwa na hela kiasi hicho. Nadhani ipo haja ya kuishauri serikali yetu mara mbimbili
   
 3. M

  MZAWATA JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 555
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  hawa ni wale wale tu, hawana jipya ni full ujambaz, mtanzania wa kawaida unapomtajia mi. 111 unamaanisha nn ss
   
 4. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Uliza mshahara wa DG ndo utajua shirika la nyumba la taifa lilikufa na mwenyewe...........
   
 5. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Uliza mshahara wa DG ndo utajua shirika la nyumba la taifa lilikufa na mwenyewe...........
   
 6. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,105
  Likes Received: 1,494
  Trophy Points: 280
  watu wengi hawajui nini madhumuni ya kuanzisha mashirika kama NHC BABA WA TAIFA alipokuwa akizungumzia usawa wa binadamu alihusisha mahitaji muhimu ya binadamu kama malazi,mavazi na chakula kwamba kila mtu bila kujali kipato chake anastahili kupata huduma hizo ndio maana shirika hilo lilianzishwa ili watu waweze kupata huduma hizo kwa bei nafuu na wengine wakiuziwa nyumba kwa bei nafuu na hata ubinafsishaji wa mashirika ulipoanza shirika hilo liliachwa kwa makusudi kwa sababu huduma yake bado ilikuwa bado inahitajika kwa jamii lakini kwa siku za karibuni limekuwa likijenga na kuuza na kupangisha nyumba kwa bei ambayo wananchi wengi wa kawaida hawawezi kuimudu na pia wamechangia kuharibu hata plan za mipango miji kwa kujenga nyumba sehemu ambako tayari nyumba zilikuwa zimejengwa bila kujali watu wanaoishi hapo watoto wao wanahitaji sehemu za kuchezea angalia nyum,ba walizopanga kujenga ubungo,keko na maeneo mengineyo kama serikali oilikuwa inataka kupata faida si wangebinafsha tu management au shirika badala ya kuliita shirika la umma bila kuwa na manufaa yoyote kwa umma
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  May 24, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Naona hujui kuwa Tanzania tuna "mortgage" financing iliyoanzisha na Jakaya Mrisho Kikwete.
   
 8. m

  mvunjamiwa JF-Expert Member

  #8
  May 24, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 455
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mortgage haiwezi kukidhi mahitaji ya watanzania wa kawaida. Masharti yake ni magumu. Issue ni accessibility. Raia wa kawaida na nyumba ya Milioni 100 wapi na wapi? Na wewe utakuwa ni kati ya hao mafisadi kupitia mradi huu wa ujenzi? Muda utafika kila kitu kitakaa wazi.
   
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Wewe una matatizo ya ufahamu. Mortgage financing inakuwezesha kununuwa hiyo nyumba kiukamilifu hata kama mshahara wako ni kima cha chini, kwa kuwa dhamana ni hiyo nyumba yenyewe.

  Hutoweza kupata mkopo wa kujenga nyumba mpya kama hauna dhamana za kutosha lakini utapata mkopo wa nyumba iliyo tayari kwa kuwa hiyo nyumba ndiyo dhamana yenyewe. Funguka kidogo wacha kulemaa kimawazo.
   
 10. mi_mdau

  mi_mdau JF-Expert Member

  #10
  May 24, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 563
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Acha kudanganya ribosome, ishu sio dhamana ishu ni bei ya hiyo nyumba kwa mtanzania. Mortgage ingekuwa inapunguza bei ni sawa, ila sana itapanda tu kwa sababu ya riba. Watanzania wangapi wenye hela za halali ambao sio matajiri wanaweza kulipia hizo nyumba. Bila aibu wanatangaza redioni eti mfanyakazi wa kawaida anawezakununua hizo nyumba!!
   
 11. ARV

  ARV JF-Expert Member

  #11
  May 24, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 304
  Trophy Points: 180
  Huwa nacheka kimyakimya nikisikia lile tangazo lao redioni kuhusu yule dogo mfanyakazi wa kawaida kama mimi eti amenunua nyumba pale mchikichini, baada ya kufuatilia bei kumbe ni MIL.186 BILA VAT? Tena kwa kijumba kilichoko ghorofa ya nne huko juu. DG wao mpya professional yake ni banker,nadhani hajui haya mashirika yaliundwa kwa misingi gani?anadhani yako kibiashara kama zilivyo benki.
   
 12. M

  Moony JF-Expert Member

  #12
  May 25, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 1,593
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mhhh.. ''mortgage finance"...
  Hivi kweli kama nyumba za mchikichini, marejesho yake benki ni shilingi milioni moja ++ ni wangapi wana mishahara ya kuweza kurudisha pesa hiyo???
  Halafu tazama hata wakiwa waaongea kwenye tv wanaongea kwa jeuri huku wakiwa wamevaa suti za bei mbaya, na hilo ni shirika la umma. Hizi ni mbinu za mafisadi tu kwani fatilia uone ni watu gani tayari wamenunua na wala hata hawajapitia benki. Hakuna jipya, waige mfano wa Kenya, nyumba za estates kibao na masharti yanayowezekana. Mchechu, akina "Maige", na wengine wengiwamenunua halafu watupangishe kwa dola. Mambo ni yale yale tu sijui BABA WA TAIFA Atatusaidiaje huko aliko?
   
 13. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #13
  May 25, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kwakweli bei ni kubwa na haimnufaishi mtu wa kawaida wa Tanzania moja kwa moja kama jinsi madhumuni ya kuanzishwa kwa shirika yalivyo. Hata hivyo, NHC wanajua kuwa bei zao ziko juu na haziwalengi watu wa kawaida. Wanachosema ni kwamba, kwa sasa wako katika hatua ya kutengeneza profit toka kwa watu wa daraja la juu ili at later stages waweze kumeet mahitaji ya mtanzania wa kawaida/kati.
   
 14. v

  vickitah Senior Member

  #14
  May 25, 2012
  Joined: Jun 18, 2010
  Messages: 152
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  Ni muhimu pia kujua problems za mortgage financing.. unakaa unalipa mkopo kwa miaka mingapi? si ni binadamu anything can happen na inaamaanisha ukikosa kipato hata kama umelipa nusu nyumba inabid ipigwe mnada ili deni lilipwe.. mortgage financing inaweka watu kwenye more risk ya kuingia kwenye umaskini na kupata stress especially km nyumba zenyew ni za bei hiyo.. kama mtu unalipa laki mbili kwa mwezi toka kwenye mshahara piga hesabu rahisi tu hapo itakuchukua miaka mingapi kulipa hilo deni kama sio miaka 50. mortgage financing sio kwa maskini kama unavyodhani mkuu.
   
Loading...