Afrika Kusini yaishitaki Israel

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
Afrika Kusini imewasilisha kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki ya (ICJ) iliyopo The Hague Nchini Uholanzi dhidi ya Israel kwa kile ilichokitaja kuwa ni vitendo vya “mauaji ya kimbari” katika ukanda wa Gaza.

Kesi hiyo katika ICJ inahusiana na madai ya ukiukaji wa Israel wa jukumu lake chini ya mkataba wa mauaji ya kimbari na kusema kuwa “Israel imejihusisha, inajihusisha na inatishia kushiriki zaidi katika vitendo vya mauaji ya kimbari dhidi ya Watu wa Palestina huko Gaza”.

Katika kesi hiyo, Afrika Kusini pia inasema Israel imekuwa ikichukua hatua ‘’ kwa lengo la kuwaangamiza Wapalestina katika Ukanda wa Gaza kama sehemu ya kundi pana la Taifa, rangi na kabila la Palestina

Hata hivyo Israel imepinga mashtaka hayo huku Msemaji wa Wizara yake ya mambo ya nje Lior Haiat akiandika yafuatayo kwenye ukurasa wa X ———> “Israel inakataa na kuchukizwa na kashfa inayoenezwa na Afrika Kusini na ombi lake’ kwa mahakama ya ICJ
 
Sera za Mazayuni na Makaburu chimbuko na msingi wake ni mmoja

ni Wa South Africa pekee katika kizazi cha karibuni wa naweza kueleza kwa ufasaha udhalimu ambao wao waliupitia kuanzia 1652-1994 yaani walihujumiwa kwa miaka 323 na Makaburu na Dunia ya kwanza iliwaunga mkono Makaburu kwa miaka yote na harakati zao za kujikomboa ziliitwa za kigaidi
Hata Hayati Nelson Mandela na wapiganaji wenzie walifadhiliwa kila kitu kutokea Tanzania hadi Wanawake wa kuwaliwaza ilimradi tu wajikomboe

Hayati Nelson Mandela kaondolewa kwmy orodha ya Watu hatarishi Duniani na CIA baada ya kustaafu Urais wa SA

Hiyo kesi haiwezi kuwafanya chochote Israel kwa kuwa Miamba ya Dunia ipo pamoja nayo lakini SA itakuwa imetekeleza wajibu wake wa kupinga udhalimu

hata sisi Tanzania 1965 tulisitisha uhusiano na Uimgereza kupinga Uamuzi wao wa kuwapa Mamlaka Weupe kule Zimbabwe japo tulijua kusitisha Mahusiano ya Mabeberu sie tungeathirika zaid kuliko wao lakin bado Mwl Nyerere aliendelea na msimamo wake kuonesha uungaji mkono harakati za kina Mugabe




Sent from my SM-G9500 using JamiiForums mobile app
 
Screenshot_20240103-195632_Gallery.jpg


Maneno ya Mstahiwa Mufti Mkuu wa Usultani wa Oman Sh. Ahmed Al khalili, kuhusu Africa ya Kusini, Allah amuhifadhi.
 
View attachment 2861157Maneno ya Mstahiwa Mufti Mkuu wa Usultani wa Oman Sh. Ahmed Al khalili, kuhusu Africa ya Kusini, Allah amuhifadhi.

Mods naomba uzi huu msiuhamishe wala kuufuta, Waislamu tunapitia wakati mgumu sana kwenye hii forum.
Njia pekee ni nyie kwenda vitani Gaza na sio kutoa matamko. Wapelestina mnaowatetea wameua ndugu zetu wawili tena kwa ukatili mkubwa mno. Hata hiyo mufti AKIENDA Palestine watamchinja tu
 
1,600 Israeli Soldiers Suffer from Combat Stress as Mental Health System Faces Collapse

January 2, 2024

By Palestine Chronicle Staff Israeli media reported that 1,600 soldiers show symptoms of combat stress reaction as the country’s mental health system faces collapse.

At least 1,600 Israeli soldiers show symptoms of combat stress reaction and 250 were discharged from service for this reason, according to Israeli media.

The Israeli news website Walla reported on Tuesday that “symptoms of battle combat stress reaction have appeared on at least 1,600 Israeli soldiers since the start of the ground operation in the Gaza Strip about two months ago”.
 
Israeli Officials Fear ICJ Could Charge Israel with Genocide in Gaza – Reports

January 1, 2024

By Palestine Chronicle Staff

Israeli officials are concerned that the Hague-based International Court of Justice (ICJ) will charge Israel with genocide in Gaza, Israeli media reported.

According to the Israeli newspaper Haaretz, “a senior legal expert dealing with the matter has in recent days warned IDF brass, including Chief of Staff Herzl Halevi, that there is real danger that the court will issue an injunction calling on Israel to halt its fire, noting that Israel is bound by the court’s rulings”.
 
Mimi ningekuwa sehemu ya mods.. ningeufuta huu uzi kabisa kwa sababu unawatuhumu mods kwamba wanaubaguzi kati ya posts za wakristo au watu wa dini zingine na waislamu, kwamba mods wanafuta sana post za wafuasi wa dini ya kiislamu. Hii ni tuhuma mbaya sana mods waliangalie hili. Au wakusamehe na usirudie tena kutaka kutugawa wakati kila siku tunajadiliana na waislamu wanaotuma post zao humu kama akina Alwaz, Malaria 2, nk.
Yaani kuwa mod tu ungekua na jazba namna hio

Sasa ungepewa ujumbe wa nyumba kumi ungekuaje

Hufai kuwa kiongozi popote pale kwahuo ukurupukaji ulokua nao
 
View attachment 2861157Maneno ya Mstahiwa Mufti Mkuu wa Usultani wa Oman Sh. Ahmed Al khalili, kuhusu Africa ya Kusini, Allah amuhifadhi.

Mods naomba uzi huu msiuhamishe wala kuufuta, Waislamu tunapitia wakati mgumu sana kwenye hii forum.
Hivi kwa nini hakuna hata nchi moja ya Kiarab/Kiislam iliyoweza kuwa na ujasiri kama wa RSA? Ina maana wote wanaiogopa Israel?

Hawa watu ni hopeless kabisa. Kusubiri kusifia badala ya kuchukua hatua ni udhaifu wa hali ya juu. Na hapa aliyetoa hii kauli ni Mufti wala siyo Serikali ya Ufalme wa Oman, Israel wakikohoa tu kuhusu hii kauli utasikia mfalme wa Oman anasema hatuhusiki na kauli ya huyu mufti kama Makonda alivyokanwa na Serikali kwenye issue ya ushoga.
 
Kuna mambo fulani yakihusisha Mungu muumbaji, watu wenye akili huchutama"

Israeli imetajwa hivyo na itaendelea kuwa hivyo hata kama mitazamo ya kibinadamu italidharau hilo

Na kwa sababu hiyo, nayaona mapigo ya Mungu kwa wasauzi yakizidi kuitesa ile nchi

Ubaguzi na kuuwana pamoja na mizozo ya kisiasa na uchumi, itawaandama milele,

Hili suala la SA kuipeleka Israeli ICC linamnyima nini zaidi ya Walebanoni kuwapeleka Israel ICC wenye udugu wa karibu zaidi na hao anaodhani wanaonewa huku akisahau kabisa aliyenzisha hizo fujo kuwa ndio Hamasi??

Kwa nini wasiwe Wamisiri, Moroco, UAE,Iraq na ama Oman huko anakotoka huyo Ostadh?
 
Hili suala la SA kuipeleka Israeli ICC linamnyima nini zaidi ya Walebanoni kuwapeleka Israel ICC wenye udugu wa karibu zaidi na hao anaodhani wanaonewa huku akisahau kabisa aliyenzisha hizo fujo kuwa ndio Hamasi??

S.A wanajitambua wale, na wameumia sana kwa mateso wanayopitia wapalestina tokea miaka mingi, ni mtu asie na huruma wala utu ndio atawasapoti hao magaidi wa kizayuni, na huo msemo wa kusema wasaidiwe na ndugu zao, badala ya S.A! Ni wewe tu na danganyika yako mmekaa kimya hata maandamano tu shida, jamaa watakata misaada sio?
 
Kama mnaleta nyuzi za kigaidi kwanini zisifutwe waislamu wangapi wameanzisha nyuzi kulaani mauaji ya Joshua na Clemence
Tena wengine walifurahia hayo mauaji
Ningekuwa mods Janjaweed wote mngekula ban.

Wakina nani wamefurahia, unaweza weka ushahidi hapa?

Imekuuma ya watanzania, ila mateso na mauwaji ya wasio na hatia nchini palestina kwa miaka mingi hayajakuuma, pole sana ewe myahudi mweusi.

Hamas wanaendelea kutembeza kichapo kwa jamaa zenu zionists
 
Back
Top Bottom