John Mwelele
Member
- Apr 16, 2016
- 18
- 17
Mei 10 2016, Timu ya wataalamu kutoka shirika la ndege la Etihad leo wametembelea abiria tisa waliolazwa baada ya Ndege aina ya EY474 ya shirika hilo kupatwa na msukosuko mkali katika anga la wazi ambapo walitoa huduma endelevu, ushirikiano na msaada.
Vile vile walikutana na wanafamilia kadhaa wa majeruhi na kuthibitisha kuwa shirika la ndege la Etihad litagharamia gharama zote za matibabu.
Kati ya majeruhi tisa ambao walikuwa wamelazwa, wengi wao wataruhusiwa kuondoka leo. Rais wa shirika la ndege la Etihad na Mkurugenzi Mkuu Bwana James Hogan amesema: “Rubani wetu na wafanyakazi wa ndege wanapaswa kupongezwa sana kwa utulivu wao na namna ambavyo walishughulikia tukio hili la aina yake kwa utaalamu mkubwa, na huduma waliyoionesha kwa abiria japo kuwa wengi wao walikuwa wamejeruhiwa. Ni ushahidi wa mafunzo ya kiwango cha juu yanayotolewa kwa wafanyakazi wetu ndio sababu athari za msukosuko ulipunguzwa. Wakati huo hakuna kabisa usalama wa ndege,abiria au wafanyakazi walioathirika.”
Shirika la ndege la Etihad linashirikiana kikamilifu na Mamlaka za Indonesia katika uchunguzi wao
- Mwisho -
Shirika la Ndege la Etihad lilianza shughuli zake mnamo mwaka 2003 na hadi kufikia mwaka 2015, ilikuwa limeshabeba abiria takriban milioni 17.6. Kutoka makao makuu yake huko Abu Dhabi, shirika hili linasafiri au limetangaza mipango ya kuhudumia wasafiri na mizigo kutoka vituo 117 huko Mashariki ya kati, Afrika, Ulaya, Asia, Australia na nchi za Americas. Shirika lina ndege aina ya Airbus na Boeing takriban 122, Zaidi ya ndege 204 zikiwa zimewekea oda, zikiwemo Boeing 71, Ndege 25 aina ya Boeing 787s, 25 aina ya Boeing 777Xs, 62 aina ya Airbus A350s na ndege 10 aina ya Airbus A380s.
Shirika la Etihad pia limewekeza katkia AirBerlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Jet Airways , Virgin Australia, pamoja na shirika lenye makazi Uswiss Darwin Airline, likifanya biashara kama Etihad Regional. Shirika la Ethihad, sambamba na airberlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Etihad Regional, Jet Airways na NIKI, pia hushiriki pamoja nkwatika washirika wa Etihad Airways, brand mpya inayowaleta kwa pamoja mashirika mengine ya ndege yenye uelewa sawa ili kutoa huduma bora zaidi kwa wateja, kuwapa wateja ratiba nzuri Zaidi na kuwazawadia wateja wakudumu.