Shirika la Misaada la Uingereza la Who is Hussain limeingia katika Rekodi ya Dunia kwa kuandaa idadi kubwa zaidi ya uchangiaji damu

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121


Shirika la Misaada la Uingereza la Who is Hussain limeingia katika Rekodi ya Dunia kwa kuandaa idadi kubwa zaidi ya uchangiaji damu kwa siku.
1663655942399.png

Tukio hilo lililofanywa na Social Justice Charity, kupitia 'Who is Hussain', pamoja na NHS Blood and Transplant na Imam Hussain Blood Donation Camp, waliweka rekodi ya dunia ya kujitolea mnamo Agosti 27 mwaka huu na rekodi hiyo ilithibitishwa Septemba 17.

Rekodi ya awali ya dunia ya ilikuwa na wachangiaji 34,723 ilifanyika mwaka 2020, rekodi mpya iliyowekwa kwa kufikisha wachangiaji 37,018 kama ilivyothibitishwa na rekodi rasmi za dunia.

Harakati inayoitwa #GlobalBloodHeroes ilipokea michango kutoka maeneo 360, ikijumuisha vituo kote Uingereza na nchi nyingine 27, kama vile Argentina, Thailand na Iraki. Uchangiaji ulianza kutoka New Zealand na kuishia na watu waliojitolea kutoka Marekani.

Katika akaunti yao rasmi ya Twitter, ‘Who is Hussain’ wemeweka cheti rasmi cha rekodi ya dunia, cha "michango mingi ya damu kimataifa katika siku moja", na kuandika "Ni rasmi… #GlobalBloodHeroes".
 
Back
Top Bottom