Shirika La Misaada Afrika

Mlenge

R I P
Oct 31, 2006
2,125
2,291
Pana haja ya kuanzishwa (iwapo bado) shirika mahsusi wa kutoa misaada itokayo nchi za Afrika kwenda nje ya Afrika. Sikumbuki kusikia shirika la misaada la nchi yoyote ya Kiafrika. Kama lipo shirika la namna hiyo, basi halisikiki sana.

Wanufaika wa shirika hilo wanaweza kuwa Waafrika na binadamu wengine waishio kwenye sayari ya dunia, nje ya bara la Afrika. Hii itapendeza zaidi ikiwa kila nchi ya Kiafrika itakuwa na shirika la misaada kwa wananchi wa nchi nyingine isipokuwa nchi husika.

Mfano wa shirika kama hilo ni:






Kutoa Ni Moyo, Usambe ni Utajiri
 
Nadhani Tanzania tumeishaanza kutekeleza hili kama link hapa chini inavyofafanua :):):)
====
Kwanza kabisa, naunga mkono hoja ya kuanzisha shirika hili. Kisha napendekeza namna ninayodhani inafaa katika kuanzisha shirika hili kama ifuatavyo:

Ni rahisi kuanzisha shirika la misaada kwa nchi moja moja za kiafrika na baadaye mashirika haya yaungane huko mbeleni kuliko kuanza na shirika kubwa la misaada la Afrika moja kwa moja.

Sababu, kwanza itasaidia nchi husika kuondoa fikira potofu kuwa zenyewe haziwezi kutoa misaada bali ni wa kusaidiwa tu. Wananchi wengi wa kiafrika wasomi na wasiosoma bado wana fikra hii potofu. Pili, kwa upotofu huu wa fikra tukianzisha moja kwa moja shirika hili wabaya wetu kiuchumi watatuvuruga kirahisi na kuua kabisa ndoto na mipango madhubuti ya kuanzisha shirika hili....!

Bado nina kumbukumbu jinsi ndoto za kuwa na Africa Monetary Fund zilivyoyeyushwa kizembe kwa sababu ya upotofu wa fikira kuwa Afrika haiwezi kujitegemea na kisha kutoa misaada ng'ambo. Kwa taarifa tu, Comredi Ghaddaf ( R.I.P), mbali na mapungufu yake kama mwanadamu, alikuwa na lengo kama hili uliloanzishia uzi, mleta mada.
 
Mkuu TUJITEGEMEE , tuko pamoja.

Kwa kuanzia mataifa hayo ya Kiafrika yatakapoanzisha mashirika yao ya misaada, yajikite kutoa misaada (asilimia fulani ya jumla ya misaada watakayotoa) iwe nje ya bara la Afrika. Hii itasaidia kujenga utamaduni wa kutoa misaada.
 
Mkuu TUJITEGEMEE , tuko pamoja.

Kwa kuanzia mataifa hayo ya Kiafrika yatakapoanzisha mashirika yao ya misaada, yajikite kutoa misaada (asilimia fulani ya jumla ya misaada watakayotoa) iwe nje ya bara la Afrika. Hii itasaidia kujenga utamaduni wa kutoa misaada.
Naunga mkono hoja....tuanze kuwasaidia Haiti, Yemen, hata na Australia wanaopambana na moto kwa sasa, nakadhalika
 
Mkuu Mlenge
Mashirika ya kimataifa yana masilahi nyeti na nchi zao. USAID walisaidia kujenga visima kumbe walikuwa wana monitor nyendo za Ayaman Al Zawahiri baada ya kumuondoa OBL.

Kwa Afrika, tujiulize nchini tuna shirika gani la misaada ukiacha Red cross na Red crescent?

Tunakwendaje kusaidia kuzima moto ikiwa ''Fire brigade'' zetu ndizo hizi tunazozijua?

Wazo si baya ikiwa kutakuwa na shirika la misaada kwa nchi, kanda kabla ya kwenda Africa.

Tusijefiikiria shirika kama ''AU'' iliyojengewa HQ na Wachina!

Ningefikiria uwepo wa ''EAC AID'' Ikijishughulisha na majanga ya dharura.
Shirika liundwe na Watalaam wanaoweza kufanya kazi popote katika nchi hizo ikibidi.
 
Happy New Year Nguruvi3,

Tukianza na shirika la Afrika nzima, itabidi litegemee michango ya nchi wanachama tu. Mathalan, inaweza kusemwa, 1% ya michango yote ya nchi zanachama AU itapelekwa kwenye shirika la misaada la Afrika. EACaid ikiwapo basi iwe ni ya kusaidia nje ya EAC. Na sisi Waafrika tukusudie kuhusika na matatizo ya watu wengine, kwa kutoa kasehemu tu ka kidogo tulichonacho. Wenzetu wana mashirika ya misaada pamoja kwamba hawajamaliza matatizo yao. Wao wakichangia nyangumi, nasi tukachangia dagaa, wote tuko kambi moja.

Kadhalika, shirika la misaada la nchi ya Kiafrika inabidi lisaidie nje ya nchi husika pasipo kutegemea kurejeshewa fadhila.
 
Kadhalika, shirika la misaada la nchi ya Kiafrika inabidi lisaidie nje ya nchi husika pasipo kutegemea kurejeshewa fadhila
Kwa maelezo ya Nguruvi3 aliyotoa hapo juu, hao unaowaita " watoa misaada nyangumi" wanakuwa na malengo mapana ya kusaidia interest za nchi zao( wanatoa msaada ambao watapata faida). Hivyo na sisi kama tunaamua kutoa msaada dagaa kwa lengo lile la watoa msaada nyangumi, kuna uwezekano wakumezwa mazima tutakapo rudi " kambini" inayotujumuisha na hao watoa misaada nyangumi.

Kwa maelezo hayo hapo juu, Mkuu, inabidi tuwekane sawa. Hili shirika linalokusudiwa litakuwa " purely non profit ama non interest" kwa Afrika au nalo litakuwa na lengo na kuinufaisha Afrika msingi ule wa USAID kwa Marekani!? Jibu la swali ni muhimu sana kutolewa kabla hatujaanza mikakati ya kuanzisha shirika lenyewe. Kwani bila jibu hili tunaweza kuchanganyana huko mbele wakati shirika limeishaanza na kupelekea matatizo makubwa kwa nchi washiriki.

Niulize kidogo kwenye organs za AU hakuna organ inafanya kazi kama hizi za shirika linalokusudiwa !? (Nimepata jibu la swali hili )
- - -
Policy Sub-Committee of the Special Emergency Assistance Fund for Drought and Famine Relief in Africa

Purpose
The Sub-Committee of the Special Emergency Assistance Fund for Drought and Famine Relief in Africa oversees all matters relating to the operation of the Fund of the same name. Its mandate includes to:
• Act as the supreme organ of the Fund
• Determine the Fund’s operational policy including the criteria for approval of loans and the terms and conditions for withdrawals from the Fund
• Approve administrative and other expenses related to the operation of the Fund
• Select beneficiary countries and decide on the amounts of grants and loans
• Initiate effective measures for mobilising resources for the Fund from both public and private sources and including African and non-African sources
• Make recommendations regarding the management and administration of the
Fund’s resources by the African Development Bank
• Make recommendations regarding the Statute of the Fund and its rules and operating procedures
• Report on its activities annually to the AU Executive Council in consultation with the Chairperson of the Commission.

Evolution
The Sub-Committee originated in the Lagos Plan of Action recommendation to establish
a Special Emergency Assistance Fund for Drought and Famine in Africa. In the mid-1980s, the Council of Ministers called for the Fund to become operational and the OAU created an interim policy committee to act as the supreme organ of the Fund, determine policy and draw up the criteria for approval of loans or grants from the Fund. The Interim Policy Committee became the Sub-Committee of Special Emergency Assistance when the AU was created.

- - -
Kwa hiyo tuna pa kuanzia baada ya kukamilisha uanzishwaji wa mashirika ya misaada ya nchi wanachama wa AU.
 
jitegemee,

Pointi alizotoa Nguruvi3 na ulizozitoa, zina mashiko na ni za kuzingatiwa. In life there are two reasons for everything. Good reasons and real reasons. I am not sure reasons ninazozitoa ni good au ni real, lakini na sisi Waafrika ifike mahala tuingie uwanjani kucheza badala ya kuwa mpenzi msikilizaji wa matukio ya duniani hapa. Eneo la misaada ya nje ni kielelezo kimoja tu.

"Tuibe" playbook ya nchi zilizoendelea na sisi tupatiemo uelekeo wa kuchukua kwa yale tutakayoyaona ni ya maana. Nchi za Asia zinafanya hivyo mintarafu uhusiano na Afrika. Wamekwiba Playbook ya Wazungu na wao wakadumbukia uwanjani Afrika, beating Wazungu at their own game. Sasa hivi ni Waafrika tu ambao tumeachwa mbali katika hizi intercontinental geopolitical games.

Afrika ilikuwa playground ya Wazungu hasa wa Ulaya. Wa Marekani playground yao ilikuwa zaidi Amerika Kusini. Ni miaka 20 hivi iliyopita walipogeuzia macho yao Afrika, wakaanza kupigana vikumbo na wenzao wa Ulaya. Maneno ya mitaani, yapaswayo kupuuzwa, yanadai hata mabomu ya ubalozi wa Marekani yalikuwa na mkono wa Ulaya ili kuwakatisha tamaa Wamarekani waone Afrika hakuwafai. Maneno ya mitaani. Wote wamestukia Wachina wakizidi kete huku Afrika.

Wamarekani Wakishutumu Wachina

Wachina wakishutumu Marekani

 
Shirika La Misaada Afrika, jana limetoa msaada kwa taifa la China katika kupambana na ugonjwa wa Covid-19. Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi msaada huo, mwakilishi mkazi wa shirika alimwambia balozi wa China, apokee pole ya Waafrika kwa niaba ya Wachina wote.

"Kwa kweli msaada huu ni wenye thamani ndogo kifedha, lakini unawakilisha nia yetu njema ya kuonyesha tuko pamoja," alisema mwakilishi mkazi.

Shirika La Misaada Afrika lilikabidhi mablangeti, mabomba ya sindano na chupa kadhaa za dripu, miongoni mwa vitu anuai vilivyotolewa msaada toka kwa wananchi wa nchi mbalimbali Afrika.

NB: Habari hiyo hapo juu ni ya kufikirika. Lakini habari kama hii zingefaa kuwa za kawaida ikizingatiwa yanayotukia.
 
Back
Top Bottom