Shirika la Afya Duniani (WHO): Tanzania hakuna Ebola

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) na Kitengo cha Kupambana na Magonjwa kutoka Marekani (CDC), wamethibitisha kuwa Tanzania hakuna mlipuko wa ugonjwa wa ebola.

Uthibitisho huo umekuja baada ya Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kuruhusu kuchukua sampuli za wagonjwa waliodhaniwa kuwa na ebola na baada ya kupima wamethibitisha kuwa Tanzania hakuna ebola.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile jana alifanya mazungumzo na Mkurugenzi wa CDC wa Marekani, Robert Redfield aliyewasili nchini juzi kwa ajili ya kuangalia namna ya Marekani itakavyoweza kushirikiana na Tanzania katika kudhibiti magonjwa ya mlipuko.

Kutokana na mazungumzo baina ya pande hizo mbili jana imeelezwa kuwa hadi sasa Tanzania haina mgonjwa wa ebola.

Katika taarifa yake, Redfied alisema Marekani na Tanzania zitaendelea kushirikiana na kuisaidia Tanzania katika juhudi zake za kupambana na kudhibiti magonjwa ya mlipuko kupitia Global Health Security Alisema lengo kuu la Marekeani ni kuendelea kushirikiana na nchi marafiki kulinda usalama wa afya dunia.

Mbali na Tanzania Ofisa huyo atazuru nchi za Rwanda, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambako kumeripotiwa kuwa na ugonjwa wa Ebola.

Ofisa huyo amekuja nchini na kufanya mazungumzo na Dk Ndungulile, ikiwa ni siku chache baada ya serikali kutoa tamko kuwa hakuna mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alisema tetesi za kuwa ugonjwa huo upo nchini si za kweli na kwamba wagonjwa wawili ambao walihisiwa kuwa na ugonjwa huo vipimo vimeonesha kuwa hawana kitu.

Ummy alisema mpaka sasa hakuna mgonjwa aliyethsibitika kuwa na ugonjwa huo na kwamba serikali inaendelea kuchukua tadhari kudhibiti ugonjwa huo.

Kauli ya Waziri Ummy ilikuja baada ya kuenea tetesi kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, kuwa kuna mtu mmoja amefariki dunia kwa ugonjwa huo na wawili wamewekwa karantini.

Pia tetesi hizo zilichagizwa zaidi na waraka wa WHO na ule wa Umoja wa Mataifa (UN) ambao ulisema kuna tetesi za kuwa Tanzania kuna ugonjwa usiojulikana na kwamba wanachunguza tetesi hizo.

Alisema wagonjwa wawili ambao walihisiwa kuwa na ugonjwa huo mmoja kutoka Songea na mwingine Dar es Salaam, wamechukuliwa sampuli mara mbili kwa nyakati tofauti na vipimo vimeonesha hawana mambukizi ya ebola.

Tangu Agosti mwaka 2018, DRC ilivyobainika kuwa na mlipuko wa ugonjwa huo mpaka Agosti 12, mwaka huu, jumla ya wagonjwa 3,099 wamefariki dunia.

Kufuatia hali hiyo serikali imechukua tadhari kwa kununua vifaa vya mkononi vya kupima joto 2,700 na mavazi kinga na kusambaza katika mikoa ya Kagera, Mwanza, Kigoma, Rukwa Katavi na Dar es Salaam.

Pia, wametoa mafunzo kwa watumishi 460 na kwa upande wa ngazi ya jamii wametoa mafunzo hayo kwenye kada mbalimbali ambapo 264 ikiwemo waendesha bodaboda wamenufaika na mafunzo hayo.

Zaidi, soma;

Kuna mijitu akili zao zilishatekwa na wanasiasa!
Yani kwa jinsi yalivyo kuwa yanatoka mapovu kushinikiza selikali iseme kuna ebola..
Alafu na yule kigogo nae ndio kawashika akili kabisa.
 
Asante kwa taarifa
Mungu ni mwema siku zote!
 
Mijitu ilio ishiws Akili kichwani ilikuwa ikiombea Majibu yawe ni Ebole
Ajabu nalo limo humu humu Tanzania

Mungu ibariki Tanzania haya majanga atuepushie Mbari sana
 
AFADHALI wamesema wenyewe...juzi nilikuwa nasafiri kufika NCHIiii fulaniii (Jina kapuni) wakasema Tanzania kuna ebolaaa....nilikuwa mpoleee, wakanitazama mara tatu tatuuu...ikabidi niache anuani ya hoteli kwa ufwatiliaji
 
Hata hivyo sina imani na mabeberu, huwa hawana hasara kwa mtu asiye na faida kwao.
 
Back
Top Bottom