Shinyanga yajitetea kuwa ya mwisho kielimu

Einstein

Senior Member
Dec 5, 2009
121
26
CHANGAMOTO mojawapo inayochangia kushuka kwa elimu ya msingi mkoani Shinyanga imeelezwa kuwa ni kutopatikana kwa ufumbuzi wa kupatiwa chakula cha mchana kwa wanafunzi.
Hayo yalibainishwa mwishoni mwa wiki na Diwani wa Kata ya Isaka, Gerald Mwanzia, katika kikao cha wadau wa elimu wa kata hiyo.

Alisema ukosefu wa chakula cha mchana katika eneo la shule unachangia kwa baadhi ya wananfunzi kuchelewa vipindi vya masomo pindi wanaporejea majumbani kwao kwa ajili ya kupata mlo wa mchana.
Katika kikao hicho ambacho pia kiliadhimisha miaka minne ya uongozi wa diwani huyo, alisema tatizo hilo limekuwa likimuumiza kichwa katika kulipatia ufumbuzi utakaowawezesha vijana kuhudhuria vipindi vya masomo kwa wakati na kwa ufanisi mkubwa.

"Ni fahari kwa kata yetu pindi ikiongoza mkoa mzima kwa ufaulu na hilo linawezekana ili mradi chakula cha mchana kipatikane katika mazingira ya hapohapo shuleni," alisema Mwanzia.

Hata hivyo, alisema jitihada kubwa zinahitajika kuhakikisha wawekezaji walioko Kata ya Isaka, likiwemo Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP ), wanaweka usaidizi katika kutatua tatizo hilo.
Mkoa wa Shinyanga kwa mara ya pili mfululizo umekuwa wa mwisho kitaifa katika matokeo ya kumaliza elimu ya msingi, jambo ambalo linawaumiza vichwa viongozi wa serikali wa mkoa na kufanya jitihada za kujinasua kutoka mkiani kwa mwaka huu.

source TANZANIA DAIMA
http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=12862

CHANGAMOTO mojawapo inayochangia kushuka kwa elimu ya msingi mkoani Shinyanga imeelezwa kuwa ni kutopatikana kwa ufumbuzi wa kupatiwa chakula cha mchana kwa wanafunzi.
Hayo yalibainishwa mwishoni mwa wiki na Diwani wa Kata ya Isaka, Gerald Mwanzia, katika kikao cha wadau wa elimu wa kata hiyo.

Alisema ukosefu wa chakula cha mchana katika eneo la shule unachangia kwa baadhi ya wananfunzi kuchelewa vipindi vya masomo pindi wanaporejea majumbani kwao kwa ajili ya kupata mlo wa mchana.
Katika kikao hicho ambacho pia kiliadhimisha miaka minne ya uongozi wa diwani huyo, alisema tatizo hilo limekuwa likimuumiza kichwa katika kulipatia ufumbuzi utakaowawezesha vijana kuhudhuria vipindi vya masomo kwa wakati na kwa ufanisi mkubwa.

“Ni fahari kwa kata yetu pindi ikiongoza mkoa mzima kwa ufaulu na hilo linawezekana ili mradi chakula cha mchana kipatikane katika mazingira ya hapohapo shuleni,” alisema Mwanzia.

Hata hivyo, alisema jitihada kubwa zinahitajika kuhakikisha wawekezaji walioko Kata ya Isaka, likiwemo Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP ), wanaweka usaidizi katika kutatua tatizo hilo.
Mkoa wa Shinyanga kwa mara ya pili mfululizo umekuwa wa mwisho kitaifa katika matokeo ya kumaliza elimu ya msingi, jambo ambalo linawaumiza vichwa viongozi wa serikali wa mkoa na kufanya jitihada za kujinasua kutoka mkiani kwa mwaka huu.

source TANZANIA DAIMA
http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=12862

Jamani tutafika?? Ni kweli huyu diwani ana uhakika, lunch ndiyo inayofelisha wanafunzi? Naomba mchango wenu..
 
Tumejazana kwenye uongozi watu ambao hatuna jipya la kuchangia kubadili mwelekeo wa mambo. Ni kutoa visababu tu kila tunaposhindwa as if sababu hizo ndio zinatupa majawabu ya matatizo yanayotusibu.
 
Ule mradi wa wafadhili wa EQUIP mbona uliipandisha Shinyanga sana kwenye elimu miaka mitatu iliyopita? Nini kimetokea?
Ina maana hatuweza kuendeleza hata tukishaonyeshwa njia?
 
Chakula?
Mbona jamaa ni wakulima na wafugaji wazuri sana, kama ni chakula tuwachangie then tuone miaka mitatu kama wataweza kujikongoja.
 
Back
Top Bottom